Najuta kumtia umasikini Mama yangu

Najuta kumtia umasikini Mama yangu

Aisee, mda mwingine na mimi napata haya mawazo.....

nimekuelewa sana, pole

jua tu kwamba mbali na yote hayo, mama yako hajutii uwepo wako kwenye maisha yake


Mimi huwa nasema tushukuru kwa hii mechanism ya ku adapt mambo ambayo tumeumbwa nayo otherwise mambo mengine katika maisha ni majuto makuu.

Yes, anaweza kuwa anajivunia uwepo wake kwenye maisha yake lakini hiyo haifuti ukweli mchungu kuwa kupitia yeye maisha yake yameharibika mno.
Na maybe kila akiwaona wenzake waliko husikitika sana.

Kuna mwanamke mmoja namfahamu niliwahi pewa stori yake kuwa alikuwa na akili sana darasanie. Alifanya mitihani yake na kufaulu vizuri sana
Kumbuka ni zamani sana miaka ya 80 huko.
Sasa ile anatakiwa aende chuo baada ya matokeo mazuri,ikagundulika kuwa ana ujauzito.
Shule ikawa basi. Leo classmates wenzake wana magari na kazi nzuri lakini yeye yupo tu with no hope. And the sad thing ni kwamba wapo within the same city.
She saw them ride as she conduct her entrepreneurship activities by the side of the road.
 
Thread yote hii hujamzungumzia baba kabisa.

Watoto wa mama mnapenda sana kudeka.

Ndio nyie mnapaswa kuitwa JUNIA.
Kuna muda wa kina baba Huwa wanakosea sana. Hivyo kwakuwa nimeamua kujilaumu mwenyewe sijapenda sana kumzungumzia baba kwasababu ingepelekea Mimi kumlaumu.

Itoshe TU kusema kuwa Kuna vitabia vya kiarabu ambayo vimekuja kututia UMASIKINI sana sisi waafrika. Yani hatujaona jambo jema kuliiga Zaidi ya kuoa wake wengi. Mwisho wa siku familia inamshinda😭😭😭

Mkuu Nina mengi ya kuzungumza ila Leo nilitaka kujilaumu mwenyewe ili nisinge mbele.​
 
Mimi nadhani vijana mliozaliwa 90s muwashukuru sana wazazi wenu, hasa mliozaliwa kwa "bahati mbaya", ni kipindi ambacho vijana wengi walichoropoa mimba hatari. So mama yako aheshimiwe sana.

Don't dwell in the past, pambana.
 
Mimi nadhani vijana mliozaliwa 90s muwashukuru sana wazazi wenu, hasa waliozaliwa kwa "bahati mbaya", ni kipindi ambacho vijana wengi walichoropoa mimba hatari. So mama yako aheshimiwe sana.

Don't dwell in the past, pambana.
Shukrani sana boss.
 
Hatima ya maisha yako unayo wewe mikononi mwako, wewe ndiye mwenye jukumu la kuiandaa kesho yako na ya wanao.

Japo changamoto zipo nyingi sana tu Ila bado zichukulie tu kama sehemu ya masomo magumu unayojifunza na unapaswa kuyafaulu ili uvuke.

Kazi na sala, huku ukitoa sadaka/zaka hata kwa hicho kidogo unachokipata, utashangaa namna milango ya fursa inavyofunguka yenyewe.

Kila laheri chief....chukua hatua sasa usingoje siku nyingine.
Nitajitahidi sana. Asante boss
 
Mama yake kusoma na mkurugenzi mtendaji wa nmb shule ya msingi.. kwake dogo ndio anaona walipaswa leo kuwa na maisha sawa.

Anasahau kujiuliza je sekondari form 1 walifaulu shule sawa sawa.

Stori yake inaonesha mama hakufaulu kwenda form one. Ndio maana akatafutiwa kozi ya type writer.

Ila hasemi kama bosi wa NMB alifaulu mtihani wa la saba na kuchaguliwa kwenda shule ya vipaji maalumu kilakala kuanza form one. Gap la mama yake na mtu anaemtolea mfano lilianza zamani sana.
Amesema wamesoma darasa moja na ni wa kijiji kimoja.
Mama anatakiwa amlilie Mtendaji msaada kama itawezekana. Kijana ana cheti, sio ngumu sana kumsaidia ikiwa tu ana moyo wa kusaidia
 
Nashukuru sana. Hata hivyo najivunia kuwa na mzazi. Ila najutia kuwa nashindwa kutatua matatizo ya mzazi wangu badala yake yeye ndio ananitatulia matatizo yangu. Hii kwangu ni aibu sana.​
Aibu bila kuikwepa itafuatia fedhea,sasa wewe endelea kulalamika wakati hata kubeba deli la vitumbua alivyo choma mama yako ukauze hutaki eti kisa wewe ni msomi mjinga.
 
Baba na Mama yangu wanaishi pamoja. Lakini kama baba angesimama kama baba. Akaacha ya Dunia akailea familia yake bila kuoa oa wake wengi nadhani Hadi Leo hii nisinge lalamika.

Hivyo sijataka sana kumlaumu yeye kwani simpendi. Na hata ningeeleza na kumtaja kusinge badili ukweli. Kwa ufupi na yeye Bado yupo serikalini ana cheo Fulani Cha kati. Ila Hana msaada wowote.

Mpaka hivi sasa ana watoto 15 Kwa wanawake Zaidi ya 6 Kwa mshahala wa 1m ataiongoza familia yake kanani kweli baba kama huyu...?​
Wapende wazazi wako.
 
Back
Top Bottom