Najuta kumtia umasikini Mama yangu

Najuta kumtia umasikini Mama yangu

Mama yako ndiye aliye jitafutia Umaskini.

Kwani yeye alikuwa hajui kwamba anatakiwa kusoma?

Kwa nini alipata mimba, kama alikuwa anajua anahitaji kukazana maishani?

Yeye ndiye ajute kwa uzembe wa makosa yake.

Wewe huna hatia, Ulikuwa hujui lolote.

A child is born with no state of mind.

Acha kujipa presha zisizo na mantiki.

Kila mtu atabeba msalaba wake.
 
Baba alipaswa kumsaidia. Kwanini alaumu kufeli kwa mama yake wakati baba yupo?
Baba na Mama yangu wanaishi pamoja. Lakini kama baba angesimama kama baba. Akaacha ya Dunia akailea familia yake bila kuoa oa wake wengi nadhani Hadi Leo hii nisinge lalamika.

Hivyo sijataka sana kumlaumu yeye kwani simpendi. Na hata ningeeleza na kumtaja kusinge badili ukweli. Kwa ufupi na yeye Bado yupo serikalini ana cheo Fulani Cha kati. Ila Hana msaada wowote.

Mpaka hivi sasa ana watoto 15 Kwa wanawake Zaidi ya 6 Kwa mshahala wa 1m ataiongoza familia yake kanani kweli baba kama huyu...?​
 
Mkuu, wew hujahusika kabisa kumtia umaskin mama yake, ni mama ako alitaka starehe ambazo ndio zimemtia umaskini, angeshika kitabu asingekuwa masikini,

Sorry kwa maneno makali
Nakazia

Dunia haina huruma kwa uzembe wa mtu.

Ukizingua umezingua, Lazima ubebe msalaba wako.

The world is not for the weak.
 
Mama yake kusoma na mkurugenzi mtendaji wa nmb shule ya msingi.. kwake dogo ndio anaona walipaswa leo kuwa na maisha sawa.

Anasahau kujiuliza je sekondari form 1 walifaulu shule sawa sawa.

Stori yake inaonesha mama hakufaulu kwenda form one. Ndio maana akatafutiwa kozi ya type writer.

Ila hasemi kama bosi wa NMB alifaulu mtihani wa la saba na kuchaguliwa kwenda shule ya vipaji maalumu kilakala kuanza form one. Gap la mama yake na mtu anaemtolea mfano lilianza zamani sana.
Ulicho kisema ni kweli. Ila hata mh Rais mwenyewe anakiri kuwa elimu yake haijanyooka ni ya kuunga unga. Kama mama angepata ajira enzi hizo.

Angesoma na kupata ajira asinge ishia kwenye uskretari. Na hata daraja angepanda pia

Hivi unajua hata mh. Mizengo Pinda alikuwa secretary TU pale ikulu miaka hiyo kabla wewe na Mimi atujamfahamu...!​
 
Kila levo ya maisha ina changamoto zake heshimu changamoto zako,,Pambana na changamoto zako,,Tatua changamoto zako ili kuruhusu changamoto nyingine kutokeza nazo ni hivyohivyo mpaka mwisho wa Dahari,, wengine wapo kwenye hivyo viyoyozi lakini hawana hata hizo mimba wala watoto nao wanajuta kivyaovyao!!
 
Baba na Mama yangu wanaishi pamoja. Lakini kama baba angesimama kama baba. Akaacha ya Dunia akailea familia yake bila kuoa oa wake wengi nadhani Hadi Leo hii nisinge lalamika.

Hivyo sijataka sana kumlaumu yeye kwani simpendi. Na hata ningeeleza na kumtaja kusinge badili ukweli. Kwa ufupi na yeye Bado yupo serikalini ana cheo Fulani Cha kati. Ila Hana msaada wowote.

Mpaka hivi sasa ana watoto 15 Kwa wanawake Zaidi ya 6 Kwa mshahala wa 1m ataiongoza familia yake kanani kweli baba kama huyu...?​
Mshahara wa 1m Kwa zaidi ya miaka 20 au 25 serikalini?

Mzee inabidi arudi shule kwanza japo ya uzeeni sio mbaya ili apate kutengeneza mafao na vyeo vya mwisho mwisho
 
Kila levo ya maisha ina changamoto zake heshimu changamoto zako,,Pambana na changamoto zako,,Tatua changamoto zako ili kuruhusu changamoto nyingine kutokeza nazo ni hivyohivyo mpaka mwisho wa Dahari,, wengine wapo kwenye hivyo viyoyozi lakini hawana hata hizo mimba wala watoto nao wanajuta kivyaovyao!!
Shukrani sana. Nitaheshimu changamoto zangu. Na nitazifanyia kazi Kwa juhudi kuzitatua.​
 
Hapana Huwa ananipa sana matumaini. Ila Mimi nikijiangalia sioni kama nitajipata😭😭😭 mbele naona giza​
Usikubali kukata tamaa au hiyo hali ikupate hata ukiona huoni muelekeo usiache kupambana na muombe sana Mungu wako kwa bidii kila siku.

Kazi na sala iwe desturi kwako, ukiona giza limekuwa zito ujue mapambazuko yapo karibu.
 
Mshahara wa 1m Kwa zaidi ya miaka 20 au 25 serikalini?

Mzee inabidi arudi shule kwanza japo ya uzeeni sio mbaya ili apate kutengeneza mafao na vyeo vya mwisho mwisho
Huo mshahala ameupata hivi karibuni tu na amebakiza miezi michache awapishe wengine ofisini. Huku akiwa Hana ata mtoto mmoja alie ajiriwa 😭😭😭 ndio maana siku taka kuzungumza habari za baba yangu​
 
Fanya kazi kijana,angalau wewe una huyo mzazi,ambao tulikuwa parent and homeless tulitoboa baada ya kuacha kulalamika bali tukawekeza kwenye kutatua tatizo.
Nashukuru sana. Hata hivyo najivunia kuwa na mzazi. Ila najutia kuwa nashindwa kutatua matatizo ya mzazi wangu badala yake yeye ndio ananitatulia matatizo yangu. Hii kwangu ni aibu sana.​
 
Mawasiliano yake yanapatikana, pambana na kama hili litakushinda basi wewe huna roho ya upambanaji

Mtoto wa kwanza Kwa mama, ina wezekana ni wa pekee Hana mwingine ndio maana ukiandika kuna vingi watu wana kuringanisha navyo
Yap Hana mtoto mwingine. Nitajitahidi
 
Huo mshahala ameupata hivi karibuni tu na amebakiza miezi michache awapishe wengine ofisini. Huku akiwa Hana ata mtoto mmoja alie ajiriwa 😭😭😭 ndio maana siku taka kuzungumza habari za baba yangu​
Hatima ya maisha yako unayo wewe mikononi mwako, wewe ndiye mwenye jukumu la kuiandaa kesho yako na ya wanao.

Japo changamoto zipo nyingi sana tu Ila bado zichukulie tu kama sehemu ya masomo magumu unayojifunza na unapaswa kuyafaulu ili uvuke.

Kazi na sala, huku ukitoa sadaka/zaka hata kwa hicho kidogo unachokipata, utashangaa namna milango ya fursa inavyofunguka yenyewe.

Kila laheri chief....chukua hatua sasa usingoje siku nyingine.
 
Back
Top Bottom