Najuta kwa madhambi niliyoyafanya nikiwa Chuo Kikuu, naomba Mungu watoto wangu wasipite njia ile

Najuta kwa madhambi niliyoyafanya nikiwa Chuo Kikuu, naomba Mungu watoto wangu wasipite njia ile

Jemima Mrembo

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2021
Posts
2,864
Reaction score
8,328
Ukiwa kama mzazi naomba usome na kuelewa nini huwa kinatokea kwenye mabweni ya wanachuo wengi wa kike.
Nilipokuwa chuonI UDSM, niliishi Mabibo hostel kabla sijapata mwanaume aliyenipangia nyumba. Pale hostel nilijifunza mambo mengi mabaya, machafu na ya hovyo.

Nikiwa pale nilijifunza usagaji, upo very addictive. Imenichukua miaka mingi kuweza kuishinda dhambi hiii kwani hata nyumbani licha ya kwamba niko kwenye ndoa, nilikuwa nawashawishi wasichana wangu wa kazi, nawafundisha mchezo huo huku nikiwalipa donge nono kwa kuniburudisha na kunitunzia siri.

Mbali ya kusagana bado, nilikuwa na mabwana wengi tu nikiwa chuo. Chuoni nilijifunza ulevi, uvutaji sigara na bangi na mambo mengine. Licha ya kwamba nimekulia kwenye familia ya wacha Mungu, nikiwa chuo nilijifunza ushirikina. Nikajifunza maisha ya kwenda kwa waganga ili kupata dawa za mvuto kwa wanaume.

Chuo nilitoa mimba nyingi sana. Nilikuwa mlevi wa pesa, nilikuwa tayari kufanya lolote ili niwe na pesa. Nimeshawahi kusafirisha madawa ya kulevya mara kadhaa, nashukuru sikukamatwa.

Wazazi, watoto wenu huko vyuoni sio watakatifu kama wanavyoonekana. Wengi wanaharibika wakiwa chuoni. Kama hamna umuhimu wa binti yako kukaa hostel, kaa naye nyumbani ili awe salama.
 
Back
Top Bottom