Nakumbusha: Kutembea kwa miguu ndio zoezi bora na salama, kukimbia ni kujizeesha kwa hiyari

Nakumbusha: Kutembea kwa miguu ndio zoezi bora na salama, kukimbia ni kujizeesha kwa hiyari

Kwa kweli watu wamepotoshwa sana kuhusu mazoezi na hata wanaharibu miili yao!!

Wajasiliamali wanaojiita trainers wanawaongopea sana watu kwenye haya mazoezi....wanajikuta wanafanya mazoezi kuliko uwezo wa miili yao!!.....

Trainers hawatofautishi mazoezi ya wanamichezo ambao wapo active na watu wa kawaida......unakuta ni mchaka mchaka tu.......

Ndio maana wengi wao baada ya kuwa fit wanakuwa na injuries za kutosha kwenye miili yao na kujiongezea matatizo.......

Asilimia 70 ya fitness ipo kwenye diet na 30 ndio mazoezi......kitu ambacho ma trainers hawawaambii watu Kwa kuwa watakosa kamisheni za kwenye gym au wateja wao watawakimbia!!

Lakini pia sio lazima ufanye mazoezi kila siku za wiki inashauriwa at least mara tatu kwa wiki kutokana na life style yako.....lakini pia mazoezi ambayo yapo recommended na watu wataalamu ni kama vile Push ups, squats, pull up, Burpees, mountain climb nk...... unaweza kuongeza na dumbbells kwa ajili ya kuongeza resistance......
View attachment 3456037
Umeongea points, kupungua ni kusimamia ukilacho ujue,mazoezi inapigiwa promo ili watu wauze exercises equipments zao.
Kiukweli una mwanga na huna to go tongo hizi
 
mnao tubeza wakimbiaji et tunazeeka mapema poa tu, mtuache tuzeeke, sura zetu zikose nuru haina shida,

Nyie msiopenda kuzeeka endeleeni kunawiri, endeleeni kutembea,

ila naamini kuzeeka kuna sababu nyingi zaidi ya hizo mlizotaja,

kesho asubuhi na mapema nakata km 2.

MAZOEZI HUJENGA AFYA
 
Tembea KWA miguu umbali wa kukutosha.
Kama Kuna vilima na miinuko itakuwa Bora zaidi.

Kama huna muda, paki gari yako mbali au shuka KITUo kimoja au viwili kabla ya eneo lengwa Tembea KWA miguu kikakamavu.

Utanishukuru.
Mwili utabaki Bora na IMARA na mvuto hautapotea kama mkimbiaji na zile apps zao za mabio.

Ni hilo tu.

Mtumishi Matunduizi
Ukiwa pekupeku, viatu mkononi, ni bora zaidi. Nyayo zigusane na kusuguana na ardhi/udongo. Tukumbuke kuwa mwili ni udongo na unajengwa kwa udongo. Hata ukichakaa utarudi kuwa udongo.
 
Hao wanaoongea hivyo ni wale wazembe. Kijana mdogo tumbo hilo mitako hio. Hawa tukisimama nao wao ndio wanaonekana wazee ila humu wanasema kinyume. Kama unaweza kimbia mwili wemyewe utakwambia sasa tembea. Yaani kijana una 29 au 35yrs unasema kutembea ni mazoezi? Kutembea ni ytaratibu wa maisha ya kila siku. Acheni uzembe.
 
Neno ''mazoezi'' lina maana ya kitu kinachofanyika kila mara kwa mara. BTW mimi sikusema kutembea hakuna faida na wala sikusema unakimbia mara ngapi kwa mwezi. Ni crush point ya jamaa kuwa kutembea ni bora kuliko kukimbia. Yaani ndivyo alivyofanya conclusion kitu ambacho ni uongo. Aina ya mazoezi ni kitu ambacho kinachangangiwa na mambo mengi na huleta matokeo tofauti. Kwa mfano mtu mzee kukimbia kunaweza kusiwe na faida kwake kama kutembea kwa sababu kukimbia kunaweza ''kuumiza'' baadhi ya viungo na ikawa hasara badala ya faida.
Yeah, linaweza kuwa na maana hiyo lakini haimaanishi watu wote watazingatia hiyo maana

Changamoto kubwa ya mazoezi kwa watu wengi ni consistency...mazoezi kadri yanavyokuwa magumu ndio Ku maintain consistency inakuwa shida, so chagua mazoezi ambayo unaeeza kuyafanya kila siku bila shida yoyote

Halafu pia ukiwa unafanya mazoezi magumu lazima pia uwe unakula mlo quality unaoweza kuwezesha mwili Ku endure hayo mazoezi
 
Kwanza anza kupunguza uzito kama una kilo nyingi-(overweight) kwa kupunguza vyakula vya wanga na sukari ,soda .Baada ya hapo ,anza mazoezi ya kutembea at least km 2 kila siku kwa miezi sita ,ndio unaweza kuanza zoezi la kukimbia ,kuogelea nk
Yes mke wangu mtu wa mazoezi sana aliambia kama ulivyo post kwa sasa natembea kama km saba.
 
Mimi nakimbia 10Km to 11Km mara tatu kwa wiki ,jumatatu jumatano na ijumaa pamoja na push ups 150 daily hii program imenisaidia sana kushusha weight pamoja na kuu-shape mwili japokuwa sikuwa na manyama uzembe ila nilikuwa na kakitambi fulani mchongoko sasa hivi hakaonekani japo naonekana afya imeyumba but kwa wanaojua wananisifu.

Miezi mitano nyuma nilikuwa na kg 86.4 nimepima majuzi nimefika 69.7 naitafuta 65 niliyokuwa nayo zamani kabla sijawa mzembe so ushauri wangu mazoezi ni afya yako kama pumzi inakuruhusu kimbia kama tia maji tia maji wewe tembea tu lakini kutembea sioni ikikupa matokeo chanya mapema usisahau pia mpangilio wa chakula.
Tembea mzee, hayo mazoezi umeshakata mafuta sawa,, ku maintain mazoezi bila kuupa mwili stress pia ni vizuri zaidi, unakuwa na muonekano mzuri bila kukakamaa lakini bado una afya na nguvu..Mimi sijawahi kimbia, natembea kivulini wakati wa jion, ila kwa miaka mingi uzito wangu unacheza kwenye 67 mpaka 71, urefu mita 1.73, nipo lean, sina kitambi, pumzi ya kutosha....sio unafanya mazoezi mwili unakakamaa kama wanariadha wa kimbulu, una miaka 32 unaonekana kama una miaka 50
 
Hao wanaoongea hivyo ni wale wazembe. Kijana mdogo tumbo hilo mitako hio. Hawa tukisimama nao wao ndio wanaonekana wazee ila humu wanasema kinyume. Kama unaweza kimbia mwili wemyewe utakwambia sasa tembea. Yaani kijana una 29 au 35yrs unasema kutembea ni mazoezi? Kutembea ni ytaratibu wa maisha ya kila siku. Acheni uzembe.
Hakika mkuu,, waache uvivu
 
Tembea KWA miguu umbali wa kukutosha.
Kama Kuna vilima na miinuko itakuwa Bora zaidi.

Kama huna muda, paki gari yako mbali au shuka KITUo kimoja au viwili kabla ya eneo lengwa Tembea KWA miguu kikakamavu.

Utanishukuru.
Mwili utabaki Bora na IMARA na mvuto hautapotea kama mkimbiaji na zile apps zao za mabio.

Ni hilo tu.

Mtumishi Matunduizi
hapana unakosea, lengo kuu la kukimbia ni kuhakikisha damu ilazunguka round nyingi mwilini kwa haraka, kukimbia ni zoezi muhimu sana bila hili zoezi mabaki ya mafuta hunasa kwenye ukuta za mishipa na huja kusababisha matatizo makubwa ya mafuta
 
Ukiwa pekupeku, viatu mkononi, ni bora zaidi. Nyayo zigusane na kusuguana na ardhi/udongo. Tukumbuke kuwa mwili ni udongo na unajengwa kwa udongo. Hata ukichakaa utarudi kuwa udongo.
Research shows walking barefoot, or grounding, is good for us. When we touch the Earth, our bodies absorb electrons. These electrons lower inflammation and stress, and boost blood flow, according to the World Health Organization (WHO). Grounding also helps our nervous system work better.
  • My take; this is one of the factors on high longevity of peasants vs urban dwellers
 
Ukiwa unakula vizuri na kunywa maji mengi ukipiga mazoezi (sports) mwili unajengeka vema na hata ngozi inanawiri kama ulikuwa mweusi utajikuta automatical unaanza kun'gaa. Ila kama hauzingatii lishe na kunywa maji mengi hapo unauchosha mwili kwa mazoezi ni sawa na kujinyanyasa.

Mazoezi si mpaka utoke nje uwanze kutembea au kukimbia unaweza kujifungia zako chumbani kama kuna nafasi. Anza kwa kuruka kamba, unapiga squater, push up, unaruka mchakamchaka yaani ni mwendo wa HOME WORKING OUT.
Pia kama unauwezo wa kununua trademill, ukiweka ndani hauhitaji outdoor walk or joging most of the time
 
hapana unakosea, lengo kuu la kukimbia ni kuhakikisha damu ilazunguka round nyingi mwilini kwa haraka, kukimbia ni zoezi muhimu sana bila hili zoezi mabaki ya mafuta hunasa kwenye ukuta za mishipa na huja kusababisha matatizo makubwa ya mafuta
Zingatia chamgamoto za age, mtu achague; kukimbia, brisk walk, kutembea kwa baisikeli, kunyanyua uzito etc, mazoezi yanakuwa customised kulinga na age+physical wellbeing
 
Zingatia chamgamoto za age, mtu achague; kukimbia, brisk walk, kutembea kwa baisikeli, kunyanyua uzito etc, mazoezi yanakuwa customised kulinga na age+physical wellbeing
lengo la mazoezi ni kukuweka fit kabla umri haujakutupa mkono, kuanza mazoezi uzeeni ni uongo: mwili hufika kikomo cha ukuaji kuanzia miaka 30 mpaka 35, hivo basi kama ulikua mtu wa mazoezi nyuma basi afya haitakusumbua kwenda mbele baada ya miaka 35 kama hukuweka afya vizuri na ukomo wa ukuaji umefika basi hali yako ni mbaya
 
Back
Top Bottom