Uchaguzi 2020 Nalipongeza Jeshi la Polisi kwa 'fair play' ya leo kwenye mkutano wa Tundu Lissu mjini Morogoro

Uchaguzi 2020 Nalipongeza Jeshi la Polisi kwa 'fair play' ya leo kwenye mkutano wa Tundu Lissu mjini Morogoro

Kuna baadhi ya hawa ma kada wa Lumumba yaani ma RC na DC wanaojiita ati wakuu wa ulinzi na usalama wa maeneo yao ndiyo wanatuharibia jeshi letu la police.

Police wanaelewa majukumu na miaka ya kazi yao, tafadhali tusiwatwike lawama hizi.
 
Jiandae kupokea matokeo ya kura kiduchu atakazopata kwa moyo huo huo
 
Debe tupu haliachi kutika wenzie wagombea wote fomu wanajaza kimya kimya yeye kelele haziishi!!!

Huyo anayepitisha kimya kimya ametumia miaka mitano kujinadi na kujibrand peke yake. Huku wengine wakipigwa kufuli la kushirikishwa shughuli zozote za kisiasa na kijamii.

Tundu kupitisha fomu ya kuomba udhamini na kusalimia kidogo wananchi imekua nongwa
 
Hilo jeshi la polisi sijui limegawanyika nchi hii, wapo waelewa na wapo wale wenzangu na mimi, au labda leo ndio siku yao ya kupewa mishahara ndio maana wamekuwa na furaha, maana yake nikimkumbuka yule aliemkamata Sugu kule Mbeya juzi, hata siwaelewi hawa polisi wetu.
Kwa mtizamo wangu jeshi LA polisi Tanzania halina tatizo na vyama vya upinzani tatizo in wakuu was Mikoa na Wilaya ambao wao ndiyo wenyeviti wa ulinzi na usakama Mkoa na Wailaya.

Sasa linapokuja swala la kuwaminya wapinzani au kuwaacha waendelee na shuguli zao hutegemea utashi na busara za mwenyekiti wa usalama eneo husika.

Mfano Mbeya yupo bwana Chelamila ambaye anaona mkoa was Mbeye ni mali ya ccm, na wengine hawana haki na Uhuru was kufanya siasa. Mkuu was usalama akitoa hamri polisi hana namna zaidi ya kutekeleza hamri hiyo ambayo kutokana na sheria za jeshi lazima watii hamri ya mkubwa wao. Sasa ukifika Mkoa au Wailaya ambayo mkuu wake so mshari mambo huenda barabara.
 
Upinzani katika nchi hii hawajawahi kuwa chanzo Cha vurugu

Ila uoga wa watawala na wanasiasa uchwara wa upande ule ndio hupandikizwa taswira mbaya dhidi ya upinzani

Upinzani hawana silaha ,hawana jeshi,hawana Usalama lakini waogopewa why ?

Fear of unknown

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa ninaamini jeshi letu la police wakitaka kufanya kazi kwa weledi wanaweza.
Kwahiyo naamini hata JPM akiamua, haki itatendeka.
 
Sasa vyombo vya habari vya nje si vitakosa habari!
[emoji2088][emoji2088][emoji2088][emoji2088][emoji2088][emoji2088]
 
Mleta Mada badili kichwa kisomeke wakazi wa Iringa mjini kuweka Iringa Ni upotoshaji!!! Wa vijijini hawapo hapo
Sheria ya Uchaguzi inamtaka kila aliyependekezwa kugombea Urais apate wadhamini kadhaa toka maeneo kadhaa mawili yakiwa Zanzibar ndani ya muda fulani basi. Hata watunga Sheria wangekuwa wajinga kama wewe wakataka wadhamini watoke kwenye Kata kadhaa na Vijiji kadhaa vya kila eneo, kutokana na muda wangekwama kwasababu barabara na madaraja ya Magufuli hayapitiki yameenda na maji na madege yame- park Dar(Chato?) na treni ya kisasa SGR bado iko Kibaha. So far Mh. Lissu is doing fine. Wajinga walete mengine maana wanaleta kila mbinu ya kumkwamisha wanakwama wenyewe!
 
Unataka kusema MNA mpango wa kumfungia nje msiyempenda? Kwa nini msiwaache Wananchi waamue maana mlisema mnakubalika sana na mtashinda kwa 99.99% katika uchaguzi kama mlivyoshinda SM?
Nimeandika nahisi so, sijui vikao VYENU vya kuwakata warudishao majina ya wadhamini huwa mnafanyaje..!
 
Back
Top Bottom