Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
sio mpenzi wa jf na hafagilii mitandao mitandao hii so hakuna noma.
Mwamba huyu alikutana na demu wa kishua yaan kishua haswa, mwana ni un employee kwa sasa, kama ujuavyo mjini maisha ni gharama na mapenzi ni gharama haswa, sasa hakujua kama huyu binti ni wakishua yaan mama baba tajiri ni zali tu nazani, ila baadae ndo akastuka demu anakaa kwao ghorofani ndo akajua kile kina kirefu sasa mbinu za kivita zinahitajika.
Demu wazazi wazungu wazungu hawana hiyana, so akawa anampeleka mshikaji hapo kwao, kamtambulisha na nini, mwana nae mchangamfu sana, uongo mwingi, akawachangamkia sana wazazi yaani akifika kwao na demu ni anazungumza na kila mtu pale ana msifia kila mtu pale.
Sasa siku moja kamkuta mama mkwe ana umwa miguu imevimba, mshikaji bila haya bila uoga akaomba mafuta ya masaji, akaanza kumkanda bi maza na kumchua vizuri mbele ya familia yote, baba mkwe anashangaa iki nini? demu kapigwa butwaa, kaka zake wanashangaa ebhana hii kali, mwana yuko bize anamkanda bi mkubwa miguu huku ana mwambia "wewe ni mama angu mzazi siwezi kuona unateseka iv na mie kijana wako nipo hapa".
sasa ikawa ile familia ata itake nini, msela atajitolea kwa asilimia 100, akija iv mchana akamkuta baba mkwe amekaa kwenye sofa anatizama tv anaenda kwenye friji anamletea mzee maji anamwambia "baba kunywa maji mchana huu mwanadamu analoose maji mengi mwilini", alaf anampa demu care ya ajabu, akiwa home kwao pale ata mtu alalamike bando limemuishia yeye anasema ngoja nikakuchukulie vocha dukani na anaenda haigizi. sasa katengeneza dependency ya ajabu, familia nzima inamtegemea mno.
Sasa imefikia point familia nzima inamuamini haswa, baba mkwe siku hizi anamtuma mwana akamchukulie kodi kwenye nyumba zake za wapangaji huko tabata na mwana ni muaminifu haswa.
Ananiambia january hapo anaanza kazi shirika flani iv la mafuta lipo kigamboni, baba mkwe kamconnect, na anaishi kwao na demu safi kabisa na wazazi wa demu wameshamwambia demu kwamba hato olewa na mtu mwingine isipokua huyu na wazee wana mcount kama blessing mpya kwenye familia yao.
Hitimisho
Vijana igeni mifano, mambo yakiwa hayaeleweki wewe jizime data tu, swallow ur pride. Habari hii ni ukweli kwa asilimia 100, ni hapa hapa dar, hakuna neno ata moja la uongo nililo liongezea, nimeshuudia kwa macho yangu na sasa ata huyu demu wake ni rafiki angu pia.
Utaolewa bure acha ujinga na uvivu.Muulize mwana, kama hapo home kuna demu mwingine na mimi ni nizame.
Na hapo n jobless,sijui [emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]...bando limemuishia anasema ngoja nikufuatie VOCHA DUKANI... Hehehe family ya kishuaa hii ety?
We umeolewa mara ngapi mkuu?Utaolewa bure acha ujinga na uvivu.
Sijawahi kufikiri achia mbali kuolewa. Mie nimemuoa mama yako ndo maana naitwa father of all.We umeolewa mara ngapi mkuu?
Nakubaliana nawe kama wahusika ni wachaga, wapare, wakikukuyu na wengine kama hao. Ila kama baba ni mhaya, Mnyakyusa, Mha, Msukuma, Mkurya, na wengine kama hao somo halieleweki.Kimsingi kama anaelewana na Baba mkwe... Na kama wanapiga Kazi fresh, me sioni tatizo... Na huenda huyo binti labda ni wa pekee kwenye familia....
Haya maisha uki complicate Sana utaumia....
Na kujenga uaminifu na watu wakakuelewa si Jambo rahisi
Vijana wajanja sana siku hizi.
Unafeli wapi hujaja mpaka sasa?Rich kid? Nakuja
Nikiwaambiwa To yeye She is a Man muwe mnanielewa sawa Unique Flowerwakiwa mafia bora kujikataa mazima
Young God's and Goddess,Shida binadamu tumeumbwa na ego
Jamani sio kujizima data huko huko, yupo frequency Gani sijui [emoji36]
wala siyo umasikini ni roho yake tu nzuriUmaskini ni kitu kibaya sana. Kataa umaskini
Usiongeze walk kupunguza neno baadae uzi ufungwe.Ukitaka kufanikiwa sometimes kubali kuwa mtumwa....japo wanaokutumikisha nao wawe wastaarabu....wakiwa mafia bora kujikataa mazima