Namtetea mtoto wa Simbachawene, askari wachunguzwe

Magufuli alikuwa strict disciplinarian. Baada ya kifo cha Magufuli,tunamuona mtoto wake Joseph ni mnene sana. Sasa Magufuli alikuwa mnafiki?
 

Polisi Tanzania hawawezi kuacha kuomba rushwa kwenye lolote. Niliwahi kuandika nyuzi hizi:

Jeshi la Polisi na hasa Trafiki lifumuliwe na kuundwa upya

Ajali Barabarani: Tuzijue sababu, kuepuka upotoshwaji
 
Mnataka kumdalilisha baba yenu kwa Mara nyingine (kama ulichoandika ni kweli lakini)
 
Huyu dogo kama atapelekwa gereza la keko basi tuhesabu maumivu Kwa familia yake kwasababu Kwa jinsi alivyo na mwili mteketeke sijui kama atasalimika
 
Hao askari wanatakiwa washtakiwe kwa kumpiga picha bila idhini yake.
Mbona wakiwa wanapokea rushwa hawajipigi picha.
Sasa wamenipa warrant wa kuwapiga picha pindi nikiwapa buku mbili halafu narusha mtandaoni
 
Hakuna la kushangaza askari kuomba rushwa imekuwa kama tamaduni zetu ila hili la kusema mimi mtoto wa fulani hizi ndio tabia anatakiwa ajieleze je yeye kwa sababu mtoto wa fulani sheria haimuhusu au? si angekataa tu kuwapa ila kujitapa mimi baba yangu ni fulani inabidi aeleze ilikuwa nini dhumuni. Baba yake bado yuko kwenye siasa na ana ndoto nyingi na uhakika halafu unaenda kumuharibia mzee.
 
Jirecord na usambaze video ndio tutaamini kama wewe ndio mtoto wa yule askari.....bila hivyo basi ongeza mchai chai na tangawizi bila kusahau mdalasini chai izidi kunoga
 
Unalea upuuzi wewe
 
Mambo mengine ni kujinyamazia tu na kuzidi kujipambania. Sasa issue kama hii unakutana watu wanabishana kabisaa. Ila kuna viumbe na viumbe
Mambo ya kawaida tu haya
Yanatokea na waelewe dogo
Alikuwa mtungi ile siyo akili
Yake

Ova
 
Huyo kijana ni rude, huo utetezi ni wa mfa maji, mtoto wa waziri na makosa ya rough driving wapi na wapi, yeye awajibike kwa kosa alilokamatiwa
 
Imeandikwa vizuri ila umeharibu kwenye hitimisho la watoto wa viongozi KUPEWA heshima, kila raia anastahili heshima bila kujali nafasi yake
 
Wote wawajibishwe...Askari na huyo Mlevi wafikishwe kwenye mamlaka husika na kila Muhusika apate adhabu stahili.
 
waziri angesema uchunguzi ufanyike askari wa hii nchi ni waonevu sana kupita maelezo.mpaka kijana wake kutamka hayo maneno kuna jambo au kitu alitaka kufanyiwa na hawa askari wetu wa hovyo.
 
Hii ni kashfa tosha inayoweza kumuwajibisha Mtu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…