Namwombea msamaha Paul Makonda, ni damu changa iliyozikwa mapema

Namwombea msamaha Paul Makonda, ni damu changa iliyozikwa mapema

Hali ya usalama kwa Dar sio nzuri na raia wanaishi kwa mashaka mithili ya raia wa Ukraine waliopo kwenye vita vikali.

Makonda yupo serious na maisha ya wananchi wake ndio maana alipambana kukaboliana uhalifu wa kila namna.

Sasa ni wakati muafaka kumshawishi mama yetu Rais Samia amrejeshe Jembe mchapakazi Paul Makonda.
Kwa hiyo una hamu ya kubadilisha uhalifu? Panyaroad wawe replaced na makonda
 
Kama lipo la kumkumbusha Samia, ni kuagiza serikali imfungulie makonda mashtaka ya jinai uhujumu uchumi nk, sawa na Sabaya.

Seikali imekuwa na kigugumizi katika hili hadi watu tunahisi mengine yasiyofaa
Mbona serikali na DPP Kweka wameshindwa kuthibitisha mashtaka yao na wamebaki kutekeleza uonevu dhidi ya Sabaya?
 
Hali ya usalama kwa Dar sio nzuri na raia wanaishi kwa mashaka mithili ya raia wa Ukraine waliopo kwenye vita vikali.

Makonda yupo serious na maisha ya wananchi wake ndio maana alipambana kukaboliana uhalifu wa kila namna.

Sasa ni wakati muafaka kumshawishi mama yetu Rais Samia amrejeshe Jembe mchapakazi Paul Makonda.
Angekuwa amefariki kama ilivyo mapenzi ya Mungu Inakuwaje hapo???Tuache Uzuzu. Mungu ndo anajua nani anatufaa kwa muda huu kuwa mkuu wa mkoa, Nchi etc. Tena Kuna Tetesi siku hizi za karibuni anapelekwa Mahakamani kwa madudu yake aliyoyafanya akiwa kiongozi
 
Pia Sabaya aachiwe kama Mbowe alivyosamehewa kesi ya ugaidi.
 
Hali ya usalama kwa Dar sio nzuri na raia wanaishi kwa mashaka mithili ya raia wa Ukraine waliopo kwenye vita vikali.

Makonda yupo serious na maisha ya wananchi wake ndio maana alipambana kukaboliana uhalifu wa kila namna.

Sasa ni wakati muafaka kumshawishi mama yetu Rais Samia amrejeshe Jembe mchapakazi Paul Makonda.
Yaani tumkumbushe Rais Samia amrejeshe Madarakani Mtu anayezidi Matendo yanayofanywa na 'Panya Road nchini? No it can't be......!!!!!!!
 
Hali ya usalama kwa Dar sio nzuri na raia wanaishi kwa mashaka mithili ya raia wa Ukraine waliopo kwenye vita vikali.

Makonda yupo serious na maisha ya wananchi wake ndio maana alipambana kukaboliana uhalifu wa kila namna.

Sasa ni wakati muafaka kumshawishi mama yetu Rais Samia amrejeshe Jembe mchapakazi Paul Makonda.
Inawezekana wewe ni makonda
 
Mimi Makonda ni mdogo wangu kiumri na hata kiutumishi. Nilikuwepo wakati akihudumu kama mkuu wa mkoa wa Dar. Ni kijana shupavu asiyeyumba katika jambo analoliamini.

Makonda alisaidia sana Jiji la Dar kuwa salama alikimbizana Sana na wauza madawa pamoja na waliotelekeza watoto. Alilimudu Jiji kwelikweli alikuwa mbabe na wakati mwingine mnyenyekevu.

Hotuba zake zilikuwa za kiume kweli kweli mamlaka yake ilimfanya avuke mipaka na kuwa mtu wa amri na visasi Makonda akiamua kumsakama mtu alikuwa haangalii cheo chake au umaarufu wake wengi walikimbia Dar na kufunga biashara zao

Kwa sababu ya kumuogopa Makonda, maduka, mahoteli, yalifungwa Kwa kumkimbia Makonda, labda alijua atakuwa mkuu wa mkoa milele inasemekana hata viongozi wa juu yake hakuwa akiwapa heshima yao Kwa sababu tu alikuwa na mawasiliano ya Moja Kwa Moja na JPM.

Hicho ndio kinamgharimu Leo, walioshika madaraka ni wale alikuwa akiwadharau sana wakati ule wa mwendazake pamoja na yote Mimi naamini tayari amejifunza na tusimuache apotelee kusikojulikana umri wa Makonda bado ni mdogo Sana , mamlaka imsamehe na impe nafasi nyingine. Mimi na mwamini na nimemiss sana heka heka za Paulo, mamlaka imesamehe huyu mwamba asimame Tena awatumikie watanzania na abadilike

Mimi mganguzi namwombea msamaha Paulo Makonda, natamani kumuona Tena katika uongozi na majukumu ya kitaifa, bado ni mtoto na ni kijana, huenda Kuna makosa aliyafanya Kwa sababu ya mihemuko ya ujana.

Naamini amekuwa naiomba mamlaka imkumbuke bado ni mbegu changa tusimzike ila tumfufue na kumfunda Ili aendelee kuitumikia nchi yetu. Narudia Tena namwombea msamaha Paulo Makonda Kwa yote yaliyopelekea apotelee kusikojulikana

Mimi mganguzi kazi yangu ni kuganga Kila jeraha

Kwa population na vipaji walivyo navyo vinana there is no room for second chance in Tanzania.
 
Back
Top Bottom