Nani anamlinda Gekul? DPP asema hana mpango wa kuendelea na kesi
Sasa Mbowe alipopigwa 'Nolle' , alikuwa analindwa na nani?

Kesi hewa hii, haina kichwa wala miguu. dpp kaona tabu tu kaamua kuitema
 
View attachment 2854504

====

Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya Babati, Victor Kimario ameieleza Mwananchi Digital kuwa kesi hiyo imetajwa leo Jumatano Desemba 27, 2023 mbele yake na ameifuta baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kuwasilisha taarifa ya kutokuwa na nia ya kuendelea nayo.

Kesi hiyo ilifunguliwa na Hashimu kupitia kwa wakili Peter Madeleka chini ya kifungu cha 128(2) na (4) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA), kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2022.

Soma pia:

1) Audio: Emmanuel Gekul akitoa vitisho vya kutaka kumdhuru anayedaiwa kusambaza Video ya kijana aliyefanyiwa ukatili na Pauline Gekul

2) Mbunge Pauline Gekul akamatwa na Jeshi la Polisi akijaribu kutoroka nchini kuelekea nchini Kenya

3) Mbunge Pauline Gekul atakiwa kufika Mahakamani Disemba 27, 2023 kujibu tuhuma dhidi yake
Hivi kuna mbunge yeyote aliyewahi kuhukumiwa kwa makosa yanayohusiana na raia? Kuna waliowahi kuwapiga watu vibao na hakuna kilicho endelea.
 
Hana mpango wa kuendelea Na kesi kwani aliifungua yeye?
Kama hataki, amemwambie hakimu kwamba anajitoa lakini aliye ifungua aendelee nayo...
Nafikiri judge pia alikosea kukubari kiufuta kama vile Ni yeye DPP aliyeifungua... mfunguaji kesi ndio mwenye dhamana ya kuifuta- sijui DPP Ana Gundu gani ya kuifuta...
Kama rufaa itasikilizwa kutokana Na kifungu cha 128-basi DPP atakuwa hana kazi Tena Maana wanasheria wa kujitegemea watakitukia kifungo hicho kufanya kazi za Dpp siku za mbeleni... analinda ugali wake huyo...
 
Mungu ni mnene,,,uonevu wao ni wa mda tu ndo maana tunawachukulia kama watoto vile,,,kushindwa kutenda haki ni upumbavu na siyo ujinga hata. Mda mwingine muelewe ya kuwa tupo duniani kwa muda na hatujui kesho yetu. Huku ndo kulewa madaraka.
Walikuwepo madikteta na magaidi kama akina Iddi Amin,Hitler,Osama Sadam Husein lakini waliishia kufa vifo vya aibu. Kilio cha maskini adhabu yake ni kubwa mno siku zote,,,MJIREKEBISHE KABLA MUNGU HAJANYOOSHA MKONO WAKE.
Hao unaowaita magaidi walithibitishwa na mahakama zipi kwamba ni magaidi?

Huwezi kumwita mtu mwizi, gaidi ama jina lolote lile kama chombo chenye mamlaka ya kumthibitisha hakijathibitisha.
 
Usisahau kwamba pasipo na uadilifu kila la hovyo na la kihuni utaliona.Madhalimu watafsnya watakavyo.Watalindana katika batili zao.Sheria watakua na 'hiari' nazo na watafanya watakavyo.Wateule watakaa kimya na mambo yatendelea kama kawaida.Na ndio maana kuna siku ya UADILIFU,mbele ya HAKIMU MUADILIFU.Acha walindane na kucheka kwa muda tu ila watakataana siku hiyo na watalia sana kilio kisicho na mwisho.
 
DPP ndio anaye own mashtaka. Infact yeye ndioa anayepeleka mashtaka mahakamani. Kazi ya mahakama ni kusikiliza parties na kutoa hukumu. DPP akiamua kuondoa shitaka mahakamani, huwezi kusema ameingilia mamlaka ya mahakama. Mamlaka yepi kwanza!
 
View attachment 2854504

====

Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya Babati, Victor Kimario ameieleza Mwananchi Digital kuwa kesi hiyo imetajwa leo Jumatano Desemba 27, 2023 mbele yake na ameifuta baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kuwasilisha taarifa ya kutokuwa na nia ya kuendelea nayo.

Kesi hiyo ilifunguliwa na Hashimu kupitia kwa wakili Peter Madeleka chini ya kifungu cha 128(2) na (4) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA), kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2022.

Soma pia:

1) Audio: Emmanuel Gekul akitoa vitisho vya kutaka kumdhuru anayedaiwa kusambaza Video ya kijana aliyefanyiwa ukatili na Pauline Gekul

2) Mbunge Pauline Gekul akamatwa na Jeshi la Polisi akijaribu kutoroka nchini kuelekea nchini Kenya

3) Mbunge Pauline Gekul atakiwa kufika Mahakamani Disemba 27, 2023 kujibu tuhuma dhidi yake
CCM ndo inayomlinda
 
Dogo huenda amepoozwa na uchawi wa kizungu !
Watu wapo wapo tu kwa sasa !
Mambo si mambo !!
Ila inasikitisha sana.
Iwe ni kweli kwamba dogo alizamishwa chupa au u iwe ni story ya kutunga, bado inasikitisha...
Utu wa mtu unatumika vibaya, thamani ya mtu inavunjwavunjwa just to serve political interests za watu.
Kwamba mtoto wa kiume anajisingizia kuzamishwa chupa sehemu ya haja kubwa? Halafu mwendesha mashitaka badala ya kupigania misingi na maadili yeye anapoteza nia ya kuendelea na jukumu lake hilo!!
 
Rais hakuwa sahihi kutengua uteuzi wa Gekul kwa tuhuma hizi?
Unajua maana ya Tuhuma.?

Alimtengua Sabaya pia, lakini si amekutwa hana hatia.

Amemvua uwaziri sababu ya kashfa hiyo, sasa sheria imefuata mkondo .
DPP kaona haieleweki eleweki hearsay nyingi kaamua kuitupa.

Shida nini hapo??
 
Ni mambo ya ajabu sana na sijawahi ona popote duniani hivi huyo Dpp anasema hana nia ya kuendelea na kesi kwani yeye ndiye mlalamikaji?Watu wakisema tuna katiba mbovu tuwe tunaelewa
 
Jalada la Gekul linaweza kuwa kati ya majalada makubwa yaliyowahi kuwasilishwa ofisi ya DPP. Kulisoma tu na kutoa ushauri wa kisheria limechukua zaidi ya mwezi. Bado kuna mchakato wa kuandaa charge sheet, lisajiliwe mahakamani , kesi ianze kusikilizwa . Hii kesi unadhani endapo itapelekwa mahakamani itachukua miaka mingapi?

Kama kesi moja inachukua muda mrefu kiasi hiki, tume ya haki jinai iliundwa kufanya nini? Mbona hakuna chochote kimebadilika katika mfumo wa haki jinai? Lini Tanzania tutakuwa na mfumo wa haki jinai unokaribiana na Kenya?
 
Hao unaowaita magaidi walithibitishwa na mahakama zipi kwamba ni magaidi?

Huwezi kumwita mtu mwizi, gaidi ama jina lolote lile kama chombo chenye mamlaka ya kumthibitisha hakijathibitisha.
Wew ni mmoja wao eh?
Acha kutapa tapa,,, kama vipi badilikeni, msinyanyase masikini,,, mtalaaniwa hadi vizazi vyenu.
 
Maneno mazito sana haya. !
Mwenye masikio na asikie !!!
Time is running out 🙏🙏
Yaan vinajiona kama vile hawafi wanqvyokqza kuonea watu wa hali ya chini,,, shame on you,,, Ee Mungu fanya kitu kwa hawa wanaonyanyasa wenzao kwa kigezo cha vimali na madaraka flan flan.
 
Back
Top Bottom