Nani anaweza kuwa CDF mpya wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama?

Nani anaweza kuwa CDF mpya wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama?

Luteni Jenerali Mathew Mkingule ni Mnadhimu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi wa 14 tangu alipoteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa awamu ya sita Mhe. Samia Suluhu Hassan tarehe 21 Agosti, 2021.

Luteni Jenerali Mathew Mkingule alijiunga na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania tarehe 21 Februari, 1995 na kuhudhuria kozi ya afisa mwanafunzi na kupata kamisheni mwaka 1995 kuwa Luteni Usu.

Luteni Jenerali Mathew Mkingule alihudhuria kozi mbalimbali ndani na nje ya nchi ikiwemo Kenya.

Katika kulitumikia Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania, Luteni Jenerali Mathew Mkingule alishika nyadhifa mbalimbali ikiwemo Naibu Mkurugenzi wa Bajeti na Usimamizi wa Fedha, Mkurugenzi wa Fedha za Umma na Hesabu, Mkurugenzi wa Bajeti na Usimamizi wa Fedha na baadae kuwa Mdhibiti Mkuu wa Fedha Makao Makuu ya Jeshi.

Luteni Jenerali Mathew Mkingule ametunukiwa medali mbalimbali

Miaka 40 ya JWTZ

Comoro

Miaka 50 ya Uhuru

Miaka 50 ya Muungano

Miaka 50 ya JWTZ

Utumishi Mrefu

Utumishi Uliotukuka
CV inatosha alishahudumu nafasi nyeti jeshini
 
Anafuatia Brigedia General Marco Elisha Gaguti
View attachment 2253944

Jamaa anakubalika na wananchi kila alikopita anzia akiwa mkuu wa wilaya buhigwe kigoma, akaenda kua RC kagera na sasa mtwara jamaa anapiga kazi sana na hana majivuno sema rank yake labda itakua mbali maana ma meja general mbele yake wako kibao lakini jamaa ni kiongozi mzuri
 
..Abdalah Twalipo alikuwa Mkuu wa mkoa, na Kanali, akapandishwa cheo kuwa Maj Jenerali na mkuu wa Majeshi.

..Ernest Mwita Kyaro alikuwa Maj Jenerali akapandishwa cheo kuwa Jenerali na kuteuliwa mkuu wa majeshi.

..Kuna ripoti ya CIA[ majasusi wa Marekani ] inasema Twalipo hawakuiva na Mnadhimu mkuu aliyemkuta hivyo ikalazimisha ateuliwa Mnadhimu mkuu mwingine.

..Cdf Ernest Kiaro aliteuliwa kwa pamoja CoS Kiwelu ambaye alikuwa promoted kuwa Luteni Jenerali.
Enzi hizo jeshi lilikuwa young ila sasa hivi sidhani kama itawezekana ateuliwe aliye chini ya rank ya meja jenerali.
 
Enzi hizo jeshi lilikuwa young ila sasa hivi sidhani kama itawezekana ateuliwe aliye chini ya rank ya meja jenerali.

..I agree with you 100%.

..wakati Kanali Twalipo anateuliwa jeshi lilikuwa dogo. Wakati huo Cdf alikuwa na cheo cha Maj Jeneral na Cos alikuwa na cheo cha Brigedia, siku hizi wanaita Brigedia Jenerali.

..Kwa hiyo iliwezekana Kanali kuruka ngazi ya Brigedia na kuwa Meja Jenerali na kuteuliwa kuwa Cdf.

..Sasa hivi jeshi letu limekuwa kubwa ambapo Cdf ni Jenerali, na Cos ni Luteni Jenerali. Katika mazingira hayo Cdf mteuliwa lazima atatoka ktk ngazi ya Luteni Jenerali au Meja Jenerali.
 
CDF ni huyu ameanza kazi anasubiliwa kuthibitishwa
Screenshot_20220608-141213_WhatsApp.jpg
 
Kufatia habari ya jana ya kustaafu kwa General Mabeyo ndani ya JWTZ, basi kama kawaida yetu sio mbaya tukafanya bashiri ya nani anaweza akawa CDF mpya.

Kwakuwa JF ni uwanja mpana, ina wadau wengi na wengine ni wa huko huko jikoni, sio mbaya tukapendekeza jina la CDF mpya kwa kuzingatia uweledi wake katika kuchapa kazi.

Mimi nampa nafasi kubwa Luteni Jenerali Mathew Mkingule kuwa CDF mpya.

Lakini pia kwenye korido anatajwa Luteni Jenerali Yakubu Mohamed balozi wa Tanzania nchini Uturuki.

Japo pia mzee wa infantry, Meja Jenerali Mwaisaka anapigiwa chapuo.

Vilevile, Meja Jenerali Rajab Mabele naye anaweza akawa CDF mzuri tu kwa utendaji wake mzuri wa kazi huko JKT.

Japo pia kuna minong'ono kuhusu Meja Jenerali Suleimani Mzee kufatia kazi ya kutukuka huko Magereza.

Ila watu wasimua-underrate Meja Jenerali Mbuge lolote linaweza kutokea. Japo kwasasa ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera.

Brigedia Jenerali J.J. Mwaseba mkuu wa chuo cha TMA naye anatajwa japo atakuwa yupo nyuma sana kwa rank kulinganisha na hao wenzake.

NB:
Uzi huu haumlengi kumpigia mtu yoyote promo!!

Viva JWTZ
Viva Tanzania
Mohamed mcherengwa
 
APPLICATION FOMU ZIMESHATOKA KWANI?
 
CDF wa sasa ukumbuke wakati Mwamnyange anafikia umri wake wa kustaafu hakukuwa na Luteni jenerali. JPM ilimbidi amwongezee muda Mwamnyange ndiyo Mabeyo akapandishwa kutoka Meja jenerali hadi Luteni jenerali. Alihudumu kwa mwaka mmoja ndiyo akaja kuwa na cheo hicho.

Sijui wewe unaseme ingewezekana vipi, ilihali hata yeye mwenyewe alifuata taratibu kumpandisha CDF mabeyo. Usiongee usivyovijua
Kwa hiyo tunakubaliana kuwa sharti ufikie cheo cha luteni jenerali ndio unaweza kuwa cdf...
 
Back
Top Bottom