Nani anaweza kuwa CDF mpya wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama?

Kufatia habari ya jana ya kustaafu kwa General Mabeyo ndani ya JWTZ, basi kama kawaida yetu sio mbaya tukafanya bashiri ya nani anaweza akawa CDF mpya.

Kwakuwa JF ni uwanja mpana, ina wadau wengi na wengine ni wa huko huko jikoni, sio mbaya tukapendekeza jina la CDF mpya kwa kuzingatia uweledi wake katika kuchapa kazi.

Mimi nampa nafasi kubwa Luteni Jenerali Mathew Mkingule kuwa CDF mpya.

Lakini pia kwenye korido anatajwa Luteni Jenerali Yakubu Mohamed balozi wa Tanzania nchini Uturuki.

Japo pia mzee wa infantry, Meja Jenerali Mwaisaka anapigiwa chapuo.

Vilevile, Meja Jenerali Rajab Mabele naye anaweza akawa CDF mzuri tu kwa utendaji wake mzuri wa kazi huko JKT.

Japo pia kuna minong'ono kuhusu Meja Jenerali Suleimani Mzee kufatia kazi ya kutukuka huko Magereza.

Ila watu wasimua-underrate Meja Jenerali Mbuge lolote linaweza kutokea. Japo kwasasa ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera.

Brigedia Jenerali J.J. Mwaseba mkuu wa chuo cha TMA naye anatajwa japo atakuwa yupo nyuma sana kwa rank kulinganisha na hao wenzake.

NB:
Uzi huu haumlengi kumpigia mtu yoyote promo!!

Viva JWTZ
Viva Tanzania
Rekebisha kichwa cha Habari CDF ni mkuu wa majeshi ya ulinzi.... Majeshi ya usalama Yana wakubwa wake
 
..hata mimi naona ni vigumu kumruka CoS wa sasa hivi Lt.Gen.Mkingule.

..vinginevyo itabidi wateuliwe Cdf na Cos wapya.

..iliwahi kufanyika wakati wa Kiaro[cdf] na Kiwelu[cos], na Mboma[cdf] na Sayore[cos].
Mara nyingi CoS anayeteuliwa muda mfupi kabla ya CDF kustaafu huwa anaandaliwa tu kuwa CDF mpya. Mifano inayoonyesha trend hiyo ni pamoja na George Waitara, Davis Mwamnyange, na huyu Venance Mabeyo.
Jeshini kuwa cdf siyo kujenga madaraja tu bali ni elimu nzuri, weledi na ujuzi na uzoefu mkubwa wa uongozi wa kijeshi,uzalendo, uaminifu na sifa nyinginezo zilizotukuka seniority na taswira yake jeshini.
Inaonekana kuwa hulijui jeshi kwa hivyo hata hujui kuwa jeshini kuna kitu kinaitwa Field Engineering. Kuhusu unachoita "uongozi wa kijeshi, uzalendo, uaminifu na sifa zilizotukukua jeshini" ni wazi pia kuwa hujui kwamba mtu hawezi kuwa Major General bila kuwa na sifa hizo.
 
Kufatia habari ya jana ya kustaafu kwa General Mabeyo ndani ya JWTZ, basi kama kawaida yetu sio mbaya tukafanya bashiri ya nani anaweza akawa CDF mpya.

Kwakuwa JF ni uwanja mpana, ina wadau wengi na wengine ni wa huko huko jikoni, sio mbaya tukapendekeza jina la CDF mpya kwa kuzingatia uweledi wake katika kuchapa kazi.

Mimi nampa nafasi kubwa Luteni Jenerali Mathew Mkingule kuwa CDF mpya.

Lakini pia kwenye korido anatajwa Luteni Jenerali Yakubu Mohamed balozi wa Tanzania nchini Uturuki.

Japo pia mzee wa infantry, Meja Jenerali Mwaisaka anapigiwa chapuo.

Vilevile, Meja Jenerali Rajab Mabele naye anaweza akawa CDF mzuri tu kwa utendaji wake mzuri wa kazi huko JKT.

Japo pia kuna minong'ono kuhusu Meja Jenerali Suleimani Mzee kufatia kazi ya kutukuka huko Magereza.

Ila watu wasimua-underrate Meja Jenerali Mbuge lolote linaweza kutokea. Japo kwasasa ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera.

Brigedia Jenerali J.J. Mwaseba mkuu wa chuo cha TMA naye anatajwa japo atakuwa yupo nyuma sana kwa rank kulinganisha na hao wenzake.

NB:
Uzi huu haumlengi kumpigia mtu yoyote promo!!

Viva JWTZ
Viva Tanzania
Mimi sijui mambo ya kijeshi sijapita hata huko maJKT ila ukiteuliwa kuwa ubalozi ujue unatengwa na siasa za ndani mara nyingi ni neutralisation of threats....Huyo Yacoub sijui Yakuba alitolewa kwa sababu maalumu maana alikua na ujamaa na bwana yule, na alikua timu ya kina Bashiru
 
Mkuu hii haina mjadala! Nadhani kinachozingatiwa ni Seniority katika ngazi ya juu kijeshi.
 
Back
Top Bottom