Nani anaweza kuwa CDF mpya wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama?

Nani anaweza kuwa CDF mpya wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama?

The new Coming CDF mostly likely akawa huyu Jenerali
 
Kufatia habari ya jana ya kustaafu kwa General Mabeyo ndani ya JWTZ, basi kama kawaida yetu sio mbaya tukafanya bashiri ya nani anaweza akawa CDF mpya.

Kwakuwa JF ni uwanja mpana, ina wadau wengi na wengine ni wa huko huko jikoni, sio mbaya tukapendekeza jina la CDF mpya kwa kuzingatia uweledi wake katika kuchapa kazi.

Mimi nampa nafasi kubwa Luteni Jenerali Mathew Mkingule kuwa CDF mpya.

Lakini pia kwenye korido anatajwa Luteni Jenerali Yakubu Mohamed balozi wa Tanzania nchini Uturuki.

Japo pia mzee wa infantry, Meja Jenerali Mwaisaka anapigiwa chapuo.

Vilevile, Meja Jenerali Rajab Mabele naye anaweza akawa CDF mzuri tu kwa utendaji wake mzuri wa kazi huko JKT.

Japo pia kuna minong'ono kuhusu Meja Jenerali Suleimani Mzee kufatia kazi ya kutukuka huko Magereza.

Ila watu wasimua-underrate Meja Jenerali Mbuge lolote linaweza kutokea. Japo kwasasa ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera.

Brigedia Jenerali J.J. Mwaseba mkuu wa chuo cha TMA naye anatajwa japo atakuwa yupo nyuma sana kwa rank kulinganisha na hao wenzake.

NB:
Uzi huu haumlengi kumpigia mtu yoyote promo!!

Viva JWTZ
Viva Tanzania
Yakubu Mohamed Kishastaafu tayari, Corridor Gani hiyo inamtaja ?
 
Hv polisi na askari magereza kwa cheo chochote kile watakachokuwanacho hawawezi kukalia kiti cha u-cdf!?
But mwanajeshi yyte kwa vyeo vyao wanaweza kukalia nafasi ya juu kabisa ya IGP ama mkuu wa magereza ni sawa hapo ama mimi ndio najichanganya!
mwenye uelewa atufafanulie please
Yeah mkuu hakuna polisi wala magereza anayeweza kukalia nafasi yoyote ile ya jeshi

Ila mwanajeshi kuanzia cheo cha brigedia jenerali aweza kuwa mkuu wa jeshi lolote kati ya polisi au magereza nk

JWTZ ndiyo jeshi senior kuliko majeshi yote
 
Humu watu hata protokali za jeshi hawazijui
Yani mtu ni brigedier general au major general awe cdf halafu aachwe lieutenant general?
Enzi za mwendazake ofcourse ingewezekana hata segeant kuwa cdf

Inawezakana wewe pia hujui. Yaani major general ashindwe kupewa promotion mseleleko na kufanywa CDF. Imeshawahi kutokea huko nyuma.

Jeshi letu halina tu full generals and lieutenant generals wengi kwa wakati mmoja; otherwise, hakuna military leadership skills ambazo Lieutenant General na General wanazo, lakini experienced Major General hana. Shida ni size ndogo ya jeshi letu!
 
Luteni, Meja, Brigedia (Jenerali).

Hivi anaweza kuteuliwa mtu ambaye sio rank ya Luteni Jenerali direct akawapita walio juu yake?

..Abdalah Twalipo alikuwa Mkuu wa mkoa, na Kanali, akapandishwa cheo kuwa Maj Jenerali na mkuu wa Majeshi.

..Ernest Mwita Kyaro alikuwa Maj Jenerali akapandishwa cheo kuwa Jenerali na kuteuliwa mkuu wa majeshi.

..Kuna ripoti ya CIA[ majasusi wa Marekani ] inasema Twalipo hawakuiva na Mnadhimu mkuu aliyemkuta hivyo ikalazimisha ateuliwa Mnadhimu mkuu mwingine.

..Cdf Ernest Kiaro aliteuliwa kwa pamoja CoS Kiwelu ambaye alikuwa promoted kuwa Luteni Jenerali.
 
Humu watu hata protokali za jeshi hawazijui
Yani mtu ni brigedier general au major general awe cdf halafu aachwe lieutenant general?
Enzi za mwendazake ofcourse ingewezekana hata segeant kuwa cdf
CDF wa sasa ukumbuke wakati Mwamnyange anafikia umri wake wa kustaafu hakukuwa na Luteni jenerali. JPM ilimbidi amwongezee muda Mwamnyange ndiyo Mabeyo akapandishwa kutoka Meja jenerali hadi Luteni jenerali. Alihudumu kwa mwaka mmoja ndiyo akaja kuwa na cheo hicho.

Sijui wewe unaseme ingewezekana vipi, ilihali hata yeye mwenyewe alifuata taratibu kumpandisha CDF mabeyo. Usiongee usivyovijua
 
..Mabeyo alitakiwa astaafu baada ya kufikisha miaka 60 mwaka 2016/17.

Cc nyabhingi
Kwa cheo alichonacho unastaafu kwa miaka 65
Usikariri umri wa kustaafu ni miaka 60, kwenye majeshi haipo hivyo. Kwenye jeshi kustaafu kunategemea na cheo chako
 
Kwa cheo alichonacho unastaafu kwa miaka 65
Usikariri umri wa kustaafu ni miaka 60, kwenye majeshi haipo hivyo. Kwenye jeshi kustaafu kunategemea na cheo chako

..hapana.

..kuna waliostaafu baada ya kufikisha miaka 60.

..yaani siku waliyofikisha miaka 60 walikabidhi ofisi za watu.

..Mwamunyange kazaliwa 1959, Mabeyo 1956.
 
kwani kwa sasa tuna ma Ltn General wangapi na major Grn wangapi?
 
..Abdalah Twalipo alikuwa Mkuu wa mkoa, na Kanali, akapandishwa cheo kuwa Maj Jenerali na mkuu wa Majeshi.

..Ernest Mwita Kyaro alikuwa Maj Jenerali akapandishwa cheo kuwa Jenerali na kuteuliwa mkuu wa majeshi.

..Kuna ripoti ya CIA[ majasusi wa Marekani ] inasema Twalipo hawakuiva na Mnadhimu mkuu aliyemkuta hivyo ikalazimisha ateuliwa Mnadhimu mkuu mwingine.

..Cdf Ernest Kiaro aliteuliwa kwa pamoja CoS Kiwelu ambaye alikuwa promoted kuwa Luteni Jenerali.

Sarakikya na Twalipo hao ni outliers. Walikuwa viongozi wa jeshi changa na military career progression yao obviously haikuchukua ule mkondo wa kawaida!
 
Back
Top Bottom