Nani anaweza kuwa CDF mpya wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama?

Nani anaweza kuwa CDF mpya wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama?

Luteni Jenerali Mathew Mkingule ni Mnadhimu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi wa 14 tangu alipoteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa awamu ya sita Mhe. Samia Suluhu Hassan tarehe 21 Agosti, 2021.

Luteni Jenerali Mathew Mkingule alijiunga na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania tarehe 21 Februari, 1995 na kuhudhuria kozi ya afisa mwanafunzi na kupata kamisheni mwaka 1995 kuwa Luteni Usu.

Luteni Jenerali Mathew Mkingule alihudhuria kozi mbalimbali ndani na nje ya nchi ikiwemo Kenya.

Katika kulitumikia Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania, Luteni Jenerali Mathew Mkingule alishika nyadhifa mbalimbali ikiwemo Naibu Mkurugenzi wa Bajeti na Usimamizi wa Fedha, Mkurugenzi wa Fedha za Umma na Hesabu, Mkurugenzi wa Bajeti na Usimamizi wa Fedha na baadae kuwa Mdhibiti Mkuu wa Fedha Makao Makuu ya Jeshi.

Luteni Jenerali Mathew Mkingule ametunukiwa medali mbalimbali

Miaka 40 ya JWTZ

Comoro

Miaka 50 ya Uhuru

Miaka 50 ya Muungano

Miaka 50 ya JWTZ

Utumishi Mrefu

Utumishi Uliotukuka
Na huyu ndio CDF Mpya
 
Atawekwa muislam kutoka zenjii

Sent from my itel A509W using JamiiForums mobile app
jinsi gani unavyoonekana mbaguzi na mdini, mtoa mada kauiliza nani hajauliza dini wala wapi anatoka.kwani Zanzibar kuna shida gani au muislamu tatizo nini? na kwani akiwa muislamu ubaya nini maana hawajawahi shika nafasi hiyo
 
Habari,

Mama kipenzi RAIS SAMIA, mama unayeupiga mwingi.

Kwa maslahi mapana ya taifa hili, nakuomba umpandishe cheo Brigedia Generali Marco Gaguti kutoka hapo alipo mpaka Generali mkuu na umkabidhi kijiti cha U CDF.

Amekuwa akifanya vizuri tangu akiwa DC Buhigwe, RC Kagera mpaka sasa akiwa RC Mtwara mpakani hali shwari, wale wahuni waliokuwa wakivamia vijiji wakitokea Msumbiji kuja kuua na kuchinja raia kama kuku sasa wameufyata.

bby.jpg
 
Mabeyo aongezewe mkataba wa angalau miaka 2. Jamaa bado ni kakamavu sana, halafu hana makuu, yuko simple sana!
 
Kwa hiyo tunakubaliana kuwa sharti ufikie cheo cha luteni jenerali ndio unaweza kuwa cdf...
Hiyo ni lazima ufike kwa hivi sasa. Ilitokea awamu ya kwanza Brigadia akawa CDF kutokana na dharura tu. Ila kisheria ni hadi apitie na wote walipitia. Ila usimsingizie Mwenda zake inawezekana kwake, wakati haikutokea na yeye alifuata taratibu. Awamu ya kwanza ndiyo ilitokea
 
Kama inawezekana kurukishwa basi Brigedia prof. Kohi anatosha. Au general Marwa. Ni vema jeshi likaongozwa na wenye jeshi lao.

Sent from my itel W6004P using JamiiForums mobile app
 
Ila gaguti alionewa kupelekwa kuwa RC, na CDF ajaye ni MUISLAM weka bold hayo maneno tena toka VISIWANI ..........ila hizi ndoto jamani 😂😂😂😂
Nina Bet hivi. Mkingule anapando alipo Mabeyo na Suleiman Mzee anarudi jw kuchukua nafasi ya Mnadhimu Mkuu nafasi aliyopo Mkingule kwa sasa. Kwanza itakuwa ime balance suala la dini. Hiyo ya pili asipochukuwa Mzee basi atachukuwa jamaa mmoja anaitwa Othman.
 
Back
Top Bottom