Nani muasisi wa kula mara tatu kwa siku?

matunduizi

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2018
Posts
7,968
Reaction score
19,368
Hii ya kula mara tatu kwa siku naona kama imetapakaa dunia nzima. Nini chanzo au kunasupportive doc yoyote ya kitaalam.

Watu walitakiwa kula wanapohisi njaa na hisia hizo zitakapofikia hatua ya kuona kama nguvu zinawapungua.

Kwenye vitabu vya dini hatuoni mungozo wa mtu ale mara ngapi.

Binafsi nineamua kula ninapoona kama napungukiwa nguvu. Mambo ya Breakfast, Lunch au Dinner sioni msingi wake, ni kama mkakati wa kupoteza muda. Yaani karibu masaa matatu kwa siku unatumia kula tu.

Kama mtu huhisi njaa, acha kula unapoteza muda na pesa. Kula unapohisi unajaa na nguvu inapungua maana njaa nyingi nazo huwa ni feki na saikolijia za kurithi.

Hivyo unaweza kula mara moja,
Mbili au hata mara moja kwa siku mbili kama unaona uko fiti.

Chanzo
Mimi mwenyewe.

Ni hilo tu.
 
Hii ya kula mara tatu kwa siku naona kama imetapakaa dunia nzima. Nini chanzo au kunasupportive doc yoyote ya kitaalam.

Watu walitakiwa kula wanapohisi njaa na hisia hizo zitakapofikia hatua ya kuona kama nguvu zinawapungua.

Kwenye vitabu vya dini hatuoni mungozo wa mtu al3 mara ngapi.

Akina "workaholics" wanaweza kufa kwa njaa. Mtu anapokuwa busy sana anaweza asihisi njaa.
 
Kuna watu wanakula zaidi ya milo mitatu.

Nilishawahi kuambiwa na mtu mmoja kutoka Denmark kuwa kule kwao, Milo inaweza ikawa zaidi ya mara tatu kutegemeana na uwezo wa mtu kifedha.

Wanaanza na mlo wa Asubuhi, wanakula na kushiba. Baada ya hapo, wanakula kila baada ya masaa mawili na kuendelea. Na kadiri muda unavyosonga mbele, ndivyo aina na kiasi cha chakula kinacholiwa hubadilika.

Jioni/Usiku hula chakula kidogo tu, tena chepesi. Kwa hiyo wao muda wa kula na kushiba ni Asubuhi.
 
Akina "workaholics" wanaweza kufa kwa njaa. Mtu anapokuwa busy sana anaweza asihisi njaa.
Njaa mkuu mimi naona ni suala la kisaikolojia zaidi ya uhalisia.
Niliwahi kusoma kitabu kimoja kinasema saizi ya tumbo ni ndogo sana kama sox tu, ila sisi watu weusi tunaona ni kama kisado.

Poa mtu akiwa na uhakika wa kula chochote wakati wowote uwezekano wa kuhisi njaa mara kwa mara ni mdogo. Nadhani kiwango cha njaa kiko proportional na uwezekano wa kula.

Wataalam wa lishe wanaweza kuingilia kati kusaidia.
 
Back
Top Bottom