Nani muasisi wa kula mara tatu kwa siku?

Nani muasisi wa kula mara tatu kwa siku?

Hii ya kula mara tatu kwa siku naona kama imetapakaa dunia nzima. Nini chanzo au kunasupportive doc yoyote ya kitaalam.

Watu walitakiwa kula wanapohisi njaa na hisia hizo zitakapofikia hatua ya kuona kama nguvu zinawapungua.

Kwenye vitabu vya dini hatuoni mungozo wa mtu ale mara ngapi.

Binafsi nineamua kula ninapoona kama napungukiwa nguvu. Mambo ya Breakfast, Lunch au Dinner sioni msingi wake, ni kama mkakati wa kupoteza muda. Yaani karibu masaa matatu kwa siku unatumia kula tu.

Kama mtu huhisi njaa, acha kula unapoteza muda na pesa. Kula unapohisi unajaa na nguvu inapungua maana njaa nyingi nazo huwa ni feki na saikolijia za kurithi.

Hivyo unaweza kula mara moja,
Mbili au hata mara moja kwa siku mbili kama unaona uko fiti.

Chanzo
Mimi mwenyewe.

Ni hilo tu.
Kweli hili ni tatizo la kisaikolojia
 
Biblically, Milo ni miwili Tu.

“Kunguru wakamletea mkate na nyama asubuhi, na mkate na nyama jioni, akanywa maji ya kile kijito. ”
— 1 Wafalme 17:6 (Biblia Takatifu)
 
Njaa mkuu mimi naona ni suala la kisaikolojia zaidi ya uhalisia.
Niliwahi kusoma kitabu kimoja kinasema saizi ya tumbo ni ndogo sana kama sox tu, ila sisi watu weusi tunaona ni kama kisado.

Poa mtu akiwa na uhakika wa kula chochote wakati wowote uwezekano wa kuhisi njaa mara kwa mara ni mdogo. Nadhani kiwango cha njaa kiko proportional na uwezekano wa kula.

Wataalam wa lishe wanaweza kuingilia kati kusaidia.
It's true that ukiwa na uhakika wa kula njaaa wala haikuzongizongi
 
Biblically, Milo ni miwili Tu.

“Kunguru wakamletea mkate na nyama asubuhi, na mkate na nyama jioni, akanywa maji ya kile kijito. ”
— 1 Wafalme 17:6 (Biblia Takatifu)
Aisee hii nilikuwa sijui licha ya kusoma hiyo story ya Mtishbi mara nyingi.

Hapa alikuwa analishwa na Mungu moja kwa moja kupitia kunguru sio kjd. Hii ndio ntaitumia kqma default yangu. Asubuhi na jioni.

Hii ya milo mitatu imeanzia ulaya tena kwa sababu za kianasa tu.
 
Kuna watu wanakula zaidi ya milo mitatu.

Nilishawahi kuambiwa na mtu mmoja kutoka Denmark kuwa kule kwao, Milo inaweza ikawa zaidi ya mara tatu kutegemeana na uwezo wa mtu kifedha.

Wanaanza na mlo wa Asubuhi, wanakula na kushiba. Baada ya hapo, wanakula kila baada ya masaa mawili na kuendelea. Na kadiri muda unavyosonga mbele, ndivyo aina na kiasi cha chakula kinacholiwa hubadilika.

Jioni/Usiku hula chakula kidogo tu, tena chepesi. Kwa hiyo wao muda wa kula na kushiba ni Asubuhi.
Hii sure mkuu, usiku unaenda kulala kwa nini utupie vitu vizito? Energy created = energy destroyed kama nipo sahihi, sasa mtu anaenda kulala with a lot of energy ndo maana tunaota ndoto ambazo hazina uhalisia
 
Hii sure mkuu, usiku unaenda kulala kwa nini utupie vitu vizito? Energy created = energy destroyed kama nipo sahihi, sasa mtu anaenda kulala with a lot of energy ndo maana tunaota ndoto ambazo azina uhalisia
Kulala tumbo limejaa matonge mia ya ngunga (ugali) ndio chanzo cha ndoto za kukimbizwa na na simba kkoo, unaishia kuwasilumbua wakina Mwamposa kuna mtu anataka kukuloga.

Tumbo nalo linatakiwa kulala kama viungo vingine.
 
Aisee hii nilikuwa sijui licha ya kusoma hiyo story ya Mtishbi mara nyingi.

Hapa alikuwa analishwa na Mungu moja kwa moja kupitia kunguru sio kjd. Hii ndio ntaitumia kqma default yangu. Asubuhi na jioni.

Hii ya milo mitatu imeanzia ulaya tena kwa sababu za kianasa tu.
Kabisa kaka, mi pia nilifurahi kuiona from the bible. Eliya alilishwa na Mungu mwenyewe two times a day.

Lakini pia, tunashauriwa kula mlo wa jioni kabla ya jua kuzama.
 
Kabisa kaka, mi pia nilifurahi kuiona from the bible. Eliya alilishwa na Mungu mwenyewe two times a day.

Lakini pia, tunashauriwa kula mlo wa jioni kabla ya jua kuzama.
Mara ya kwanza nasikia, tulikuwa kwenye mkutano flani wa kiroho mzee mmoja akasema mtu anatakiwa kufunga mambo ya kula kuanzia saa 11 had 12 jioni kama atachelewa. Wote tulimcheka, siku hizi ndio nimejua yule mzee alikuwa sahihi.
 
Saa 11 ipi,ya jioni au alfajiri?
 
Saa 11 ipi,ya jioni au alfajiri?
Jioni aisee.
Hata US wanalalamika kuwa utaratibu wa kula mara tatu uliletwa na wakoloni kutoka England. Kabla ya hapo natives wa kule walikuwa wanakula wanaposikia njaa.
Hata huko ulaya na kabla ya mapinduzi ya viwanda, na watu kwenda shule walikuwa wanakula mara mbili. Msosi mkubwa mida ya saa tanotano asubuhi na jioni. Baadae walipoanza kwenda mashuleni na kuajiliwa wakaanza kuwa wanabeba Luncheon au kamkate flani kwa kukazia mchana hali ikiwa mbaya.
 
Walifuata sequence za jua na digestion system inachukua almost masaa ma4 so ukizidisha mara 3 inakua saa12 ambayo ni siku nzima y daylight.
 
Mpuuzi ni aliyeweka utaratibu wa kulala usiku, kwanini tusiwe tunalala nchana halafu usiku ndo shuguli ziendeleee.
 
Nami nauliza Ni nani muasisi wa kutembea kwa miguu miwili? Maana sioni umuhimu wake ni bora mtu utembee kwa miguu na mikono kuna uafadhali
Haujazuiliwa kufanya hivyo, lakini sisi tutaendelea vile tumefundishwa.
 
Picha lilianzia kwenye majira, asubuhi, mchana, jioni. Kila fungu lina mlo wake.
 
Mpuuzi ni aliyeweka utaratibu wa kulala usiku, kwanini tusiwe tunalala nchana halafu usiku ndo shuguli ziendeleee.
Mbona wenzako wapo kazini sasa hivi? Nilipo, ni kawaida watu kuanza kufanya kazi kuanzia saa kumi na mbili Jioni hadi saa kumi na mbili Asubuhi. Baada ya hapo ndiyo wanalala kujiandaa kwenda kazini Jioni.

Na wewe unaweza kufanya hivyo.
 
Back
Top Bottom