Nani muasisi wa kula mara tatu kwa siku?

Nani muasisi wa kula mara tatu kwa siku?

Kuna Hali unaweza kupitia maishani ukajikuta kula sio kipaumbele chako Cha kwanza...hata Mimi Kuna kipindi nilikuwa nakula mara 1 ndani ya masaa 24 na sikuwa nafeel bad Wala nini

Maisha haya nyie acheni tu​
 
Ni kweli mkuu.
Kuna watu njaa wanasikia asubuhi, ikifika mchana wanasikia, na usiku hata kama matumbo yamejaa. Kwa sababu wakuwa programmed hulq mida hiyo dangu babu na mababu.
Huu nao no utumwa, hata kama mazingira ya kula mara moja kwa masaa 24 yakipita, bado sio sahihi kurudi kwenye default ya mara tatu kwa siku.
 
Nami nauliza Ni nani muasisi wa kutembea kwa miguu miwili? Maana sioni umuhimu wake ni bora mtu utembee kwa miguu na mikono kuna uafadhali
 
Hii ya kula mara tatu kwa siku naona kama imetapakaa dunia nzima. Nini chanzo au kunasupportive doc yoyote ya kitaalam.

Watu walitakiwa kula wanapohisi njaa na hisia hizo zitakapofikia hatua ya kuona kama nguvu zinawapungua.

Kwenye vitabu vya dini hatuoni mungozo wa mtu ale mara ngapi.

Binafsi nineamua kula ninapoona kama napungukiwa nguvu. Mambo ya Breakfast, Lunch au Dinner sioni msingi wake, ni kama mkakati wa kupoteza muda. Yaani karibu masaa matatu kwa siku unatumia kula tu.

Kama mtu huhisi njaa, acha kula unapoteza muda na pesa. Kula unapohisi unajaa na nguvu inapungua maana njaa nyingi nazo huwa ni feki na saikolijia za kurithi.

Hivyo unaweza kula mara moja,
Mbili au hata mara moja kwa siku mbili kama unaona uko fiti.

Chanzo
Mimi mwenyewe.

Ni hilo tu.
hata mimi naungana na wewe, ratiba ya kula mara tatu kwa siku nilishaachana nayo, nakula muda wowote ninapojisikia njaa. Kuna mtindo wangu wa kula nauita full tank
 
Mwasisi alikuwa Profesa Mslalenjaa Mtakula Tatu.

Huyu ni kati ya wasomi wachache sana hapa Bongo waliobobea masomoni Urusi (enzi hizo zile za Juliasi wakati ikiitwa Umoja wa Kisovieti USSR).

Profesa huyo alifanikiwa kufuzu na kutunukiwa PhD 8 kwa wakati mmoja. Na tangu hapo hakuwahi kurudi Tanzania wala kusikika tena duniani.
 
Kuna watu wanakula zaidi ya milo mitatu.

Nilishawahi kuambiwa na mtu mmoja kutoka Denmark kuwa kule kwao, Milo inaweza ikawa zaidi ya mara tatu kutegemeana na uwezo wa mtu kifedha.

Wanaanza na mlo wa Asubuhi, wanakula na kushiba. Baada ya hapo, wanakula kila baada ya masaa mawili na kuendelea. Na kadiri muda unavyosonga mbele, ndivyo aina na kiasi cha chakula kinacholiwa hubadilika.

Jioni/Usiku hula chakula kidogo tu, tena chepesi. Kwa hiyo wao muda wa kula na kushiba ni Asubuhi.
huo mtindo wa kula utajaza choo haraka sana
 
hata mimi naungana na wewe, ratiba ya kula mara tatu kwa siku nilishaachana nayo, nakula muda wowote ninapojisikia njaa. Kuna mtindo wangu wa kula nauita full tank
Fulltank imekaaje hiyo mkuu
 
Kula mara tatu kwa siku asili yake ni ulaya na sisi tumerithi tu kama matokeo ya ukoloni.
Hayo mambo yameanza karne ya 17.
Mfano Breakfast imeanza kuwa popular karne ya 19 ulaya baada ya industrial revolution. Watu ilibidi wale ili wawahi kwenye ajira wakiwa na kitu tumboni.
 
Hao wanafki tu vitabu vya din mbona vimeandikwa wanawake na wanyaze makanisani na kufunika vichwa vyao tena agano jipya lakini hawafuati?
Dinner inaonekana ilikuwa ni ubunifu wa wamama wakizungu, ambao walikuwa wako bored nyumbani wakati waume zao wameenda kwenye ajira. hahaha

Hii ya kula mara tatu kwa siku naona kama imetapakaa dunia nzima. Nini chanzo au kunasupportive doc yoyote ya kitaalam.

Watu walitakiwa kula wanapohisi njaa na hisia hizo zitakapofikia hatua ya kuona kama nguvu zinawapungua.

Kwenye vitabu vya dini hatuoni mungozo wa mtu ale mara ngapi.

Binafsi nineamua kula ninapoona kama napungukiwa nguvu. Mambo ya Breakfast, Lunch au Dinner sioni msingi wake, ni kama mkakati wa kupoteza muda. Yaani karibu masaa matatu kwa siku unatumia kula tu.

Kama mtu huhisi njaa, acha kula unapoteza muda na pesa. Kula unapohisi unajaa na nguvu inapungua maana njaa nyingi nazo huwa ni feki na saikolijia za kurithi.

Hivyo unaweza kula mara moja,
Mbili au hata mara moja kwa siku mbili kama unaona uko fiti.

Chanzo
Mimi mwenyewe.

Ni hilo tu.
Mwana naona umeliangalia hili kiroho zaidi (naturally).Kufuata ratiba(muda)ni tabia ya ubongo (akili)....yaani ni tabia ya kibinadamu zaidi na sio asili.
Kwenye asili hakuna muda maalum wa kufanya kitu fulani...hakuna saa wala siku,kuna nyakati/matukio tu.
Waangalie viumbe wengine kama wanyama mbuzi,ngo'mbe nk..au hata ndege na wadudu. Hawali kwa kufuata wakati. Wakati wengine wanakula utakuta wengine wameweka pozi tu,au wanafanya mambo mengine.
Hii ya kufanya kitu kwa kufuata hali/muitikio wa mwili (maumbile kwa ujumla) ni tamu sana.
Japo naamini wengi wanakula kwa kufuata huo mtirirko kwa sababu ya uchumi....

Na sio kula tu hata kuoga,,,unapaswa kuoga pale tu unapojisikia kuoga. Kuoga kwa kufuata ratiba ni utumwa mwingine....
 
Back
Top Bottom