Nani muasisi wa kula mara tatu kwa siku?

😁😁😁😁😁😁dah umenichekesha sana sio siri
 
Huu ndio utaratibu. Kuna mdau wangu aliwahi kufukuza mke kisa kagoma kumpikiq ugali dagaa saa saba usiku. Jamaa alisikia njaa kali kitandani mama akagoma kwenda jikoni kukorofisha mambo.
Nasimama na huyo mama! Yaani saa mbili amekula tu fresh saa saba anataka mtoto wa watu akapike kama sio uchawi ni nini! Ilifaa akajipukie.
 
Picha lilianzia kwenye majira, asubuhi, mchana, jioni. Kila fungu lina mlo wake.
Mbona alasili imerukwa mkuu. Hapo ilotakiwa ipigwe angalau supu kama ishu ni majira hahaha
 
Ni muhimu kula milo mitatu kwa ajili ya afya bora, na mara moja moja unaweza kula milo miwili au mmoja mara chache zaidi. Kikubwa ni kuepuka kula mara kwa mara na pia kupunguza matumizi ya sukari na wanga iliyo kobolewa. Pia katika hiyo milo mitatu zingatia kiasi sio mpaka ushibe sana. Zingatia pia uzito na urefu wako viwiane, pia kuepuka kitambi ni hatari kwa magonjwa ya moyo na mishipa ya damu.
 

Soma kumhusu mtu mmoja anaitwa Abu l-Hasan 'Ali Ibn Nafi au kwa jina lengine ziryab aliishi karne ya 9 ndiye aliyefundisha utamaduni wa kula mara tatu kwa siku kwa vipindi vitatu tofauti na milo tofauti kwa kila kipindi na ndiyo ukawa utaratibu wa maeneo mengi duniani jamaa alizunguka nchi nyingi ila elimu yake kubwa aliifundisha spain kipindi hicho inaitwa al-andalus na elimu hiyo ikaenea kwa watu wa ulaya na mataifa ya mbali mno mfano kuoga , kutumia manukato , kuvaa nguo kutokana na misimu mfano baridi, joto, kipupwe n.k , muziki hasa magitaa (spanish codes and progressions) , matumizi ya shampoo (tuite shampoo maana alichanganya mafuta ya manukato na baadhi ya michanganyiko mingine aliyojua yeye ili kupata kimiminika kutakachozipa nywele afya na kunukia vizuri).


Unaweza kupitia hizi source

1. Ziryab - Wikipedia
2. The History of Ziryab and the Three Course Meal
 
Apokee Maua yake
 
Ubarikiwe
 
Aisee waasisi ni wazazi wangu kwani wao ndiyo walionifundisha mimi na wenzangu kula mara 4 au zaidi kwa siku!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…