Naomba kuelekezwa dawa ya kutuliza maumivu ya jino

Ahsante,limetulia ngoma usiku,

Nipo bubu tu hapa,sitamani hata kula siku ya leo.
Pole, nikajua tyr ushalifanyia MAFEKECHE.. nenda hospital waliamulie nini cha kulifanya, maumivu ya jino ni mabaya sana.
 
Pole sana
 
Uongo unataka kuuza tu dawa za kienyeji ambazo Hazina uthibitisho
Udhibitisho upi? Hivi,kabla hizo dawa za kizungu hazijaja,watu walikuwa hawaugui nankutibiwa kwa hizo dawa?
Je,leo hii si wapo wanaojitibu kwa hizo na wanapona?
Kwa nini mnaamini katika kazi na akili za wazungu tuuuu! Huenda aliemuelekeza ana udhibitisho
 
Nenda kaonane na Dentist, watanzania sijui kwann hatujali afya zetu.
 
Jino huwa lina dawa moja tu mkuu. Moja tu!I

Kaling'oe
 
1.tumia Goffen kama suluhisho la muda mfupi

2.Suluhisho la muda mrefu nenda kwa dakatari wa kinywa na meno
 
Uking'oa jino bacteria uhamia jino lingine,zipo dawa zinafanya vzuri kutibu meno bila kung'oa wacheck Modern traditional clinic,Wana dawa nzuri ya kusukutua
Nilikuwa na jino lililotoboka nikawa nalipuuzia. Lilikuwa linauma na kuacha. Watu walikuwa wananiambia ukitoa jino moja, ugonjwa unahamia kwenye jino jingine. Siku moja lilianza kuuma kwenye saa 5 ya usiku. Sikulala na sitasahau hiyo siku. Sikulala hata kidogo na mpaka kufika asubuhi nilikuwa hoi, usoni nimechoka kama mtu aliyeumwa miezi kadhaa. Saa 12 nilishatoka nyumbani kwenda hospital. Jino likatolewa. Mpaka sasa imepita miaka zaidi ya 20 na nashukuru, meno mengine yote ni mazima, na ile sehemu iliyotolewa jino ilishafunga kwa meno mengine kutanuka.
 
Maumivu ya jino ni shida,usiku sijalala hata kidogo na hapa naogopa ata kula yaani.
 
Ila karafuu inachimba jino Dr aliniambia, jino langu lilitoboka nikafanya hiyo root canal
 
Ila karafuu inachimba jino Dr aliniambia, jino langu lilitoboka nikafanya hiyo root canal
Ni kweli ila kutumia kwa Wiki mbili hakuna shimo litakalo chimbika hata baking soda inachimba ukitumia zaidi ya wiki 2. Ila Hio monkey brand inarudisha shimo la jino na kuwa zima kama mwanzo.
 
Dawa ya jino likiuma huwa ni kuling'oa... sijawahi kuamini dawa nyingine..

Me nilishawahi kushauriwa nisukutue mkojo wangu wakati linauma...hakuna kilichosaidia...

Nikaenda kung'oa....
 
Dawa ya jino likiuma huwa ni kuling'oa... sijawahi kuamini dawa nyingine..

Me nilishawahi kushauriwa nisukutue mkojo wangu wakati linauma...hakuna kilichosaidia...

Nikaenda kung'oa....
No
Sshv hiyo ni njia ya mwisho kabisa
Ukiwaona walio kwenye kitengo chao hawakushauri kulitoa kwanza
 
Kipenzi dawa ya jino ni kung'oa, ukifanya root canal jiandae kwa maumivu mara nne ya hayo baada ya mda.. Fanya tu maamuzi magumu uliondoe
Nimeshang'oa 5 mpk hapa🙌🙁
Ss mpk niwe mzee itakuwaje?
Na situmiii dawa za kawaida tena Wala mswaki wangu siwezi tumia hii ya kawaida
Mswaki mi kabla sijalala ni lzm kuliko Muda wowote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…