Naomba kujua kwanini ukimtolea Mwenyezi Mungu Fungu lake la 10% kutoka katika Mshahara wako huku ukiwa na Furaha nae hukubariki maradufu?

Naomba kujua kwanini ukimtolea Mwenyezi Mungu Fungu lake la 10% kutoka katika Mshahara wako huku ukiwa na Furaha nae hukubariki maradufu?

Sasa ndio naamini wazungu walituachia Biblia na wao wakaondoka na madini yetu, bado wanakuhadaa uwape tena sehemu ya kumi.
 
Hiyo pesa wanakula wajanja kilaini bila ya jasho.
Kikubwa umemtolea Mwenyezi Mungu na anaona hivyo utaendelea Kubarikiwa nae hata kama hao Wajanja wako wataila huku wakisubiria Laana yao ambayo itawala Kizazi na Kizazi.
 
Sasa ndio naamini wazungu walituachia Biblia na wao wakaondoka na madini yetu, bado wanakuhadaa uwape tena sehemu ya kumi.
Kwani hiyo Hela naitoa katika Mshahara wako au wangu Mimi GENTAMYCINE? Nasubiria jibu lako Wewe Zozola ( Mjinga ) sawa?
 
Aliyekuzaa.
Swali liinamachaguo mawili tu,

Aliyenizaa mm hayupo hapa JF

Hivyo hawezi kuwa certified fool hapa JF.

Ni vyema kuwa na busara na majibu unayoyatoa.

Sadaka unazotoa tu zinaweza kukupa haki ya kuwa certified fool wa JF.

Habari za kuhadaa watu watoe sadaka kwa moyo wao mmoja sio fair..

Pamoja na kuhubiri humu, bado unataka kutukana watu pasina sababu.

This is insane.
 
  • Dislike
Reactions: 511
Malaki 3:10

Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema BWANA wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la.
 
Asante sana Kwako uliyenipa hii Elimu kwani tokea nianze Kufululiza kuhudhuria Ibada zangu Kanisa Katoliki na Kumtolea Mwenyezi Mungu Fungu lake la Kumi ( 10 ) Maajabu yanayonitokea ya Kimafanikio, Baraka na Neema huwezi kamwe kuyapata kwa Mganga wa Kienyeji au wale Waganga Watatu wa Madhabahuni Kawe, Kimara Temboni na huyu mpya wa Buza kwa Lulenge.

Ukiona kila Mwezi unatoa Fungu la Kumi Kanisani Kwako halafu huoni Mafanikio yoyote yale jua hiyo Hela unaitoa huku ukiwa na Usununu ( Hasira ) Moyoni mwako au Wewe ni Mchanganya Maombi na Mzururaji tukuka wa Kutwa kwa Waganga wa Kienyeji.

Akhsante Mungu kwa BARAKA zako!!!
Huu ni Utaratibu wangu wa miaka kuna kipindi niliacha nikawa juani mbaya. Miaka ya hivi karibuni tena kwakweli namuona Mungu Sana,na Kibiblia tunatoa kwasababu tunampenda Mungu kwahiyo tunatoa kwa Furaha
 
Back
Top Bottom