Naomba kuongea na wadogo zangu wa kike wenye kutafuta ndoa

Ushauri mzuri sana yaani kuchagua mume ni kasheshe lakin kunamtu akikutongoza tu kabla hamjapata vizuri anaanza kuulizia mshaharawako sasa huyo mume kweli au umeme 😀
 
Chelewa kuolewa lakini olewa na mtu sahihi.. Si wali nazi wala si mwanaume suruali wala si yule anayepumua tuu
Hapa umepotosha mabinti/wakina dada. Mwanamke kuolewa haitajiki kujijenga kiuchumi kama mwanaume. Anavyohitajika kuwa navyo ni miaka kuanzia 18,heshima,maadili na clean past. Kutokea hapo waoaji watamwona tu. Akikaa tu kwenye njia ya hivyo vigezo tajwa sio rahisi kupita 25 akiwa ajaolewa.

Hiyo ni natural devine tu. Ukiona mwanamke anafika 30 hajaolewa, hana familia wala meaningful relationship that means somewhere somehow she stepped out of nature alignment.

Mwanamke kuchelewa kuoelewa kuna athari nyingi sana kama kudhohofika kwa kiwango cha kutengeneza chemistry na mumewe kwa sababu ya kubeba kumbukumbu za maex wake na trauma za mahusiano yake ya nyuma, hitilafu za uzazi inaeleweka mwanamke umri unavyosegea na ufanisi wa kushika mimba unapungua n.k..

Kwaiyo suluhisho ni kuwasisitiza wakae kwenye natural alignment yaani heshima na maadili ndoa itawafata tu. Lakini kuwaambia ni bora wachelewe kuolewa hii ni hatari sana kwa mwanamke. Time is very cruel to women
 
Hili somo halimuhusu kila mtu, ila tumechambwaa😂😂
 
Sensa ya Taifa
Sensa mashuleni
Sensa vyuoni
Takwimu vizazi na vifo
Naomba kuuliza, hivi ni kweli wanawake tupo wengi kiasi hiki, na wanachukua takwimu kianzia umri upi? Maana wanaume na wanawake kuna utofauti katika ukuaji, wanawake wanakuwa haraka sana kuliko wanaume! mabinti wa 2010 wataonekana wakubwa kuliko vijana wa 2010! Ndio maana ni rahisi kukuta huyo binti anashea bwana na mmama wa 80s ila sio kijana kuwa na hao wamama!

Sasa kama mtoto wa 2010 yupo tayari kuwa mke, je kijana wa 2010 yupo tayari kuwa na mke? Hapo ndipo mtafutano wa ndoa unapokuwa kasheshe! Ndio wanawake wakubwa wanakuwa challenged kuchagua sana(too picky)wanaume! Nipigie hesabu kuanzia wanawake wenye 40s na wa mwaka wa mbele ambao hawana ndoa na wanazisaka kwa nguvu!(hali zote) Matokeo yake yanaleta mada kama hii hapa!

I stand to be corrected!
 
Wadogo zangu, Mabinti mnaoenda Chuo naomba niwasihi mambo haya machache.

1. Usisahau asili yako,
Kumbuka familia yako iliyokulea na kujitahidi kukufikisha hapa. Piga simu nyumbani mara kwa mara, usijaribu kuiga maisha ya wengine. Asili yako ndiyo nguzo yako.

2. Uhuru wa chuo ni baraka na hatari
Hakuna mtu wa kukufuatilia – unaweza kulala, kula, kwenda upendavyo. Lakini uhuru huu unaweza kukupoteza masomo au maadili yako ikiwa hautaangalia.

Changamoto kuu utakazokutana nazo Fedha zinazokosekana (ada, chakula, malazi, HESLB huchelewa).

Msongo wa masomo, mapenzi, na kutengana na familia.
Shinikizo la kimapenzi/kingono kutoka wavulana (epuka mimba au magonjwa ya zinaa).

Usalama usiku nje ya chuo.
Ulevi, sherehe, na dawa za kulevya zinazoweza kuanza kwa “kikombe kimoja”.

Zingatia masomo na afya yako kwanza.
Jifunze kuweka bajeti na ratiba ya kusoma.
Chagua marafiki wanaokusukuma mbele, si wanaokushinikiza sherehe.

Jilinde: weka mipaka katika uhusiano, usikubali unyanyasaji wowote.

Tumia huduma za chuo (counselor, clinic, maktaba).

Jenga stadi za ziada (kompyuta, ujasiriamali) mapema.
Kaa karibu na Mungu kwa nguvu.

Wadogo zangu, chuo ni mazoezi ya maisha yenu yote. Simameni imara, kumbukeni lengo lenu la kuhitimu na kuwa wanawake wenye tija. Mungu awalinde na awape busara.
 
Hii dhana ya wanawake kuwa wengi kuliko wanaume huwa mnaitoa wapi hivi mnafwatiliaga takwimu za dunia kweli 🤣 au nivijiweni tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…