Naomba kuongea na wadogo zangu wa kiume walio kwenye ndoa na wanaotarajia kuingia kwenye ndoa

Naomba kuongea na wadogo zangu wa kiume walio kwenye ndoa na wanaotarajia kuingia kwenye ndoa

My brother, mambo yamebadilika sana.
Na sisi nikubadilika kuendana nayo.
Ndio wakati sasa wa kuadopt ndoa za mkataba.

Ndoa ni kitu mtu hawezi kukuelewa kabisa kabla hajaingia.

Ndio asili yake. U cannot tell.
 
9: Hii iko kiroho zaidi, ijue familia ya mwenzio vizuri. Kuna kitu kinaitwa roho ya mitaala. Kuna wakati unakuta mmeoana wote mmetoka familia zenye mitaala ndoa kudumu inakua kazi sana. Cse zile roho zinakuvuta uishi maisha walioishi wazazi wako ya kuoa na kuacha.
 
Nyongeza ndoa ni ya watu wawili mume na mke na nyie ndio wenye mamlaka ya kuamua muiendeshe vipi ili muwe na furaha wote wawili hamna haja ya kuangalia ndoa nyingne wanachofanya ili muishi kwa amani fanyeni kinachowaridhisha ninyi
 
NB: Talaka zimekuwa nyingi kwakuwa ndoa nyingi hazina maandalizi ya kutosha

Hii mada ilikuwa ije weekend lakini naona nakumbushwa Sana hivyo sina budi kuileta usiku huu. Maana mchuzi wa umbwa hunywewa wa moto Nitajitahidi kufupisha ili isichoshe kusoma

Ndoa za leo zinatakiwa kwenda nazo kwa tahadhari kubwa kwakuwa vijana wa sasa wanadhani wanajua zaidi kuliko wazazi. Na huko tuendako kile kiapo cha "Nitakupenda hadi kifo kitakapotutenganisha" kitabadilika na kuwa "nitakupenda hadi talaka itakapotutenganisha"

Ndoa za zamani zilidumu kwakuwa wanandoa waliandaliwa vizuri na wazazi na infact hata wachumba walitafutwa na wazazi

Zile ndoa hazikuwa kwa ajili ya waoaji tu bali kuunganisha familia ama koo mbili baada ya urafiki ama ukaribu wa muda mrefu wa wazazi wa pande zote mbili... Ndoa hizo zilichukua hadi miaka 10 mpaka kuja kuoana.. Maana wachumba walikuwa spotted tangu shule za msingi

Vigezo vilivyoangaliwa kwa msichana wakati huo pamoja na vingine hivi ndio vilikuwa vya msingi
1. Usichana wake(bikira)
2. Heshima
3. Uchapakazi
4. Vipawa/vipaji
5. Uzao wake
6. Ukaribu wa familia
7. Magonjwa ya kimwili ya kurithi na yale ya kiroho
Hayo mambo Saba yalizingatiwa Sana.. Lakini baadae yakaanza kukengeukwa.. Masharti na vigezo vikawa vinapungua kila uchao

Tukatoka kwenye hitaji la bikira mpaka mtoto. Kwamba hata kama hana usichana wake basi asiwe kazalishwa..

Tukatoka hapo tukaingia hapa! hata kama kazaa lakini kama afya iko sawa AIDS negative sawa
Tukatoka huko tukaingia kwenye elimu kipato na ajira.. Kwakuwa sasa ukimwi sio ishu tena, MTO to ndio kabisa.. Bikira sahau, elimu pia na sasa ni ajira na kipato

Kwahiyo sasa tembeeni na biti hiyo lakini lazima kwenye vile vigezo Saba bado vingi vinahitaji uzingativu
1. Bikira si sana kwakuwa siku hizi zinatoka kwa njia nyingi.. Lakini vilevile ukimpata mwenye nayo mchunguze vema.. Mabinti wengi siku hizi hulinda mlango mkubwa na kuuacha mdogo wazi.. Ni heri umpate aliyelinda mdogo akaacha wazi mkubwa! Zingatieni sana hilo

2. Mwenye maono na ndoto za kujenga familia bora... Baadhi huja kwenye ndoa si kwa mapenzi bali kutafuta ahueni ya maisha na kuchuma

3. Mchapakazi, mwenye kujituma, msafi na mwenye kujali

4. Mwenye kutoka kwenye familia iliyo elimika(achana na utajiri au umaskini), familia inayojitambua, wasio na vimelea vya ushirikina, laana za ukoo, magonjwa ya kurithi na magonjwa ya kiroho
Hii point number nne ni muhimu sana kwakuwa imevunja ndoa nyingi sana!

5. Mchunguze mtarajiwa wako kama sio sex maniac ama kama hana dalili za ukhanithi wa kike.. Ni muhimu awe moderate.. Na ni muhimu kumchunguza anapenda nini mnapokuwa faraghani.. Style nk.. Utajifunza mengi hapo.. Ngono ni sehemu ya ibada kwenye kiapo cha ndoa.. Hivyo pamoja na kusemwa mapenzi ni uchafu.. Lakini kuna usafi wa kimwili na kiroho pia.. Pa mtumba sawa lakini at least use grade one au two.. Lisiwe lonya..

6.. Zingatia sana hii point hapa! Chumbia/oa binti wa imani yako ama inayokaribiana na yako... Chumbia/oa wa kabila lako ama anayekaribiana na kabila lako.. Hapa muingiliano wa imani na tamaduni umevunja ndoa nyingi sana!
7.. Chumbia mwanamke wa kawaida, mwenye vigezo vya kawaida.. Wanawake wazuri sana hawafai/hawawezi ndoa.. Ni pambo la wengi litakutesa.. Chumbia mwenye tabia zinazorekebishika.. Aliyeshindikana kwa tabia fulani jitenge naye atakutesa. Kwa mfano, hasira, uchoyo, wivu majungu rohombaya nk

8. Unachumbia/kuoa mtu utakayeishi naye miaka yote mpaka kifo... Hivyo una mengi ya kufanya.. Epuka uchumba wa miezi sita mwaka mmoja.. Kumfahamu walau nusu inakuhitaji si chini ya miaka mitatu
Vilevile si kwamba unaoa supermarket kwamba utakuta kila kitu humo.. Vingine utapaswa kuongeza taratibu.. Unaoa mtu ambaya hamkuwa wote tangu udogoni hivyo kuna kipindi cha mpito cha kurekebishana ili mfiti.. Sometimes ni kipindi chenye changamoto zake.. Stay focused.. Show your support, love and caring
Mfahamu January yake mpaka December kila mwezi.. Wiki yake Monday to Sunday.. Siku yake kukicha mpaka kukichwa
Nitaendelea
Kuna formula hapo ingefatwa sijui kama watu wangeoa au kuolewa upareni hasa kwenye ukoo wenu wa Mshana
 
Back
Top Bottom