Mtangoo
JF-Expert Member
- Oct 25, 2012
- 6,167
- 5,613
Nitakupa maandiko mengi tu maana nina hakika husomi Biblia bali huwa wanakuhadithia wanachotaka ukisikie. Kila mstari nitakaoweka nitakuuliza swali la ufahamu. Usiandike majibu yake hapa, ni maswali ya kujiuliza na kujijibu mwenyeweUnaweza nipa andiko lolote kweny Bible yenu yesu yy mwenyewe akijiita mim ndie mungu ,nipe Hilo andiko yey akijiita sio paulo
Yohana 5:15 - 18 (Ukiweza soma sura nzima upate utamu wa hii habari)
"Yule mtu akaenda zake, akawapasha habari Wayahudi ya kwamba ni Yesu aliyemfanya kuwa mzima. Kwa sababu hiyo Wayahudi wakamwudhi Yesu, kwa kuwa alitenda hayo siku ya sabato. Akawajibu, Baba yangu anatenda kazi hata sasa, nami ninatenda kazi. Basi kwa sababu hiyo Wayahudi walizidi kutaka kumwua, kwa kuwa hakuivunja sabato tu, bali pamoja na hayo alimwita Mungu Baba yake, akijifanya sawa na Mungu."
Swali la kujiuliza: Kwa nini Wayahudi walizidi kutaka kumwua Yesu?
Luke 5:18-23
"Na tazama, wakaja watu wanamchukua kitandani mtu mwenye kupooza; wakataka kumpeleka ndani na kumweka mbele yake. 1Hata walipokosa nafasi ya kumpeleka ndani kwa ajili ya lile kundi la watu, walipanda juu ya dari wakampisha katika matofali ya juu, wakamshusha yeye na kitanda chake katikati mbele ya Yesu.
Naye alipoiona imani yao, alimwambia, Ee rafiki, umesamehewa dhambi zako. Basi, wale waandishi na Mafarisayo wakaanza kuhojiana wakisema, Ni nani huyu asemaye maneno ya kukufuru? N’nani awezaye kusamehe dhambi isipokuwa Mungu peke yake? Na Yesu alijua hoja zao, akajibu akawaambia, Mnahojiana nini mioyoni mwenu? Lililo jepesi ni lipi? Kusema, Umesamehewa dhambi zako, au kusema, Ondoka, uende? Lakini, mpate kujua ya kwamba Mwana wa Adamu anayo amri duniani ya kusamehe dhambi
Swali la kujiuliza: Kama ni Mungu pekee ana amri ya kusamehe dhambi, na Yesu anasema alifanya maksudi ili wajue ana amri ya kusamehe dhambi, Yesu anasema yeye ni nani?
Yohana 8:48-59
"Wayahudi wakajibu, wakamwambia, Je! Sisi hatusemi vema ya kwamba wewe u Msamaria, nawe una pepo? Yesu akajibu, Mimi sina pepo; lakini mimi namheshimu Baba yangu, na ninyi mwanivunjia heshima yangu. Wala mimi siutafuti utukufu wangu; yuko mwenye kutafuta na kuhukumu. Amin, amin, nawaambia, Mtu akilishika neno langu, hataona mauti milele. Basi Wayahudi wakamwambia, Sasa tumeng’amua ya kuwa una pepo. Ibrahimu amekufa, na manabii wamekufa; nawe wasema, Mtu akilishika neno langu, hataonja mauti milele. Wewe u mkuu kuliko baba yetu Ibrahimu, ambaye amekufa? Nao manabii wamekufa. Wajifanya u nani? Yesu akajibu, Nikijitukuza mwenyewe, utukufu wangu si kitu; anitukuzaye ni Baba yangu, ambaye ninyi mwanena kuwa ni Mungu wenu. Wala ninyi hamkumjua; lakini mimi namjua. Nikisema ya kwamba simjui, nitakuwa mwongo kama ninyi; lakini namjua, na neno lake nalishika. Ibrahimu, baba yenu, alishangilia kwa vile atakavyoiona siku yangu; naye akaiona, akafurahi. Basi Wayahudi wakamwambia, Wewe hujapata bado miaka hamsini, nawe umemwona Ibrahimu? Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambia, Yeye Ibrahimu asijakuwako, mimi niko. Basi wakaokota mawe ili wamtupie; lakini Yesu akajificha, akatoka hekaluni.
Maswali ya kujiuliza:
1. Ibrahimu aliionaje siku ya Yesu wakati aliishi miaka mingi kabla ya kuzaliwa Yesu kama Yesu hakuwepo kabla ya kuzaliwa?
2. Kama Yesu alikuwako kabla ya Ibrahimu kama mwenyewe anavyosema, ni mwanadamu wa aina gani huyu?
3. Unajua jina la Mungu wa Wayahudi ni NIKO? Kwa nini Yesu hakusema kabala ya Ibrahimu nilikuwako ambayo ni gramatically correct akasems kabla ya Ibrahimu NIKO?
3. Kwa nini waliokota mawe ili wamwue? Ni kosa gani alifanya kwenye mazungumzo kustahili kupigwa mawe mpaka kufa?
Luka 22:66 - 71
"Hata kulipokucha, walikutanika jamii ya wazee, na wakuu wa makuhani, na waandishi, wakamleta katika baraza yao, wakisema, Kama wewe ndiwe Kristo, tuambie. Akawaambia, Nijapowaambia, hamtasadiki kabisa. Tena, nikiwauliza, hamtajibu. Lakini tangu sasa Mwana wa Adamu atakuwa ameketi upande wa kuume wa Mungu Mwenyezi. Wakasema wote, Basi, wewe ndiwe Mwana wa Mungu? Akawaambia, Ninyi mwasema kwamba mimi ndiye. Wakasema, Basi, tuna haja gani tena ya ushuhuda? Maana, sisi wenyewe tumesikia maneno ya kinywa chake"
Swali la kujiuliza: Kwa nini Yesu alikubaliana na walichosema Wayahudi kuwa Yeye ni Mwana wa Mungu? Na Kwa nini Wayahudi walichukulia huu ni ushahidi wa Yeye kukufuru na kustahili kifo?
Bonus:
Yohana 19:6 - 7
"Basi wale wakuu wa makuhani na watumishi wao walipomwona, walipiga kelele wakisema, Msulibishe! Msulibishe! Pilato akawaambia, Mtwaeni ninyi basi, mkamsulibishe; kwa maana mimi sioni hatia kwake. Wayahudi wakamjibu, Sisi tunayo sheria, na kwa sheria hiyo amestahili kufa, kwa sababu alijifanya kuwa Mwana wa Mungu"
Swali la kujiuliza: Je kwa nini Wayahudi waliona ni kosa linalostahili kifo kwa Yesu kujiita Mwana wa Mungu?
Hayo yakutoshe kwa sasa. Sihitaji ujibu chochote, kwa sababu sitahangaika kukujibu. Umeomba mstari, nimekupa mistari.
Sasa hangaika nayo mwenyewe!