Naomba ushauri jinsi ya kumuapproach aliyenitafutia kazi, nataka kuacha kazi

Safi sana mkuu.
 
Nature ya Kazi ni Kudeal na mikopo Sasa nimejitahidi kuendana na mfumo lakini najikuta nafsi inakataa ni kazi ambayo inataka roho mbaya afu usiwe msikilizaji na pressure kutoka juu ni kubwa sasa Mimi ni good listener inshort sipo tayari kuifanya
Piga kazi mzee usijekujuta shauri yako.

Watu wanataka walau hata pa kujishikiza na sio kukaa tu.

Jifunze mzee utaweza tu, binafsi huwa siamini kama kuna kitu siwez kufanya ambacho naona fika nakimufu ila ni vile tu hutaki kuipa tabu akili/kuhisi unadhalilika etc.

Life likikuchapa utaikumbuka hiyo kazi na kupata option na labda labda kibao.

Binafsi sikushauri uache kazi unless umepata mchongo mwingine.
 
Nashukuru mkuu. But believe me Kuna kazi nyingi huwezi kuzifanya.
 
Bwana mdogo usije ukawa umeingia Q-net na zile zinaitwa cryptocurrency zikakudanganya utasanda !! Nilivyobeba zege mgongoni hadi leo alama haziiishi !! Biashara nimefanya kinoma ila hazikua kulingana na mazingira !!
Nilikula msoto miaka miwili nilikua najituma sana ila mambo hayaendi (mpaka now nasemaga hela zinamfata zinayemtaka sio bidii tu)piga chini mademu wote maana niliona kuna kukwazana sana huko mbeleni kiroho safi hata kama ananipende aende 😃😃😃siku ya siku bhana kama utani si nikalamba shavu hiyo siku sikulala maana !! Sio kazi nzuri pia ila imerudisha kwenye ramani ! Nikitaka kukata tamaa najiambia kabisaaa "unalikumbuka zege la muhindi wewe" naangalia na vitu nilivyofanikiwa kupitia hapo nilipo ! Fresh

Maana kipindi kile napata usingizi kuanzia saa 6 usiku yaan saa nane unapaa tena nakosa hadi asubuhi nawaza nachomokaje hapa !!
Kama una option jikatae tu mwanangu 😃😃😃
 
Pole sana Kwa uliyoyapitia ndio maisha yenyewe

binafsi naimani kubwa na mind yangu
 
Pole sana Kwa uliyoyapitia ndio maisha yenyewe

binafsi naimani kubwa na mind yangu
Fresh we kama unajikubali haina noma !! We mpigie hata simu kwamba unajikataa achukie atajijua ! Haya ni maisha yako ! Ila ujiwekee pia na uhakika kwamba hakuna tena shida itakayowakutanisha !!

Pia umewaharibia wengine tukuchane tu ! Ukishaona maswala ya kazi unasita sita kwenda sema tu mapema au usiombe kupitishwa ! Kuna dogo hapo umemkosesha nafasi wakati ukoo mzima unamtegeme! Nafsi ikusute
 
Muacheni tu aache kwani maisha si yake
 
Hivi pamoja na serikali kuandaa taasisi kama ajira porto nk. kumbe mambo ya vimemo bado yapo? Huu mchezo sio mzuri, ni bora wewe umeona mapungufu yako, wewe achia tu hiyo nafasi na huyo aliyekutafutia atapata fundisho na hatarudia tena kufanya upumbavu kama huo.
 
Mimi nashauri kabla hujaacha kazi tafuta kwanza mume mwenye hela akuoe ili uwe comfortable maana hakunaga kazi rahisi. Watu kama nyie ni laana kwa taifa. HAMSAIDIKI. Ukiacha kazi utamharibia sana huyo dingi asiaminike pia utawaharibia wengine wasisaidiwe na huyo mzee mwenye utu wake. Tatizo ninaamini kwenye ndoa ya mke mmoja ningeweza kukutolea posa.
 
Back in a days nilitengewa bajeti kwenda kutafuta vijana wa kiume 20 Kwa ajili ya shughuli maalumu ambayo ni very masculine Mzee nikaingia vijijini kuwalaghai vijana kuwa Kuna kazi zenye malipo mazuri kampuni itagharamia sehemu ya kuishi na food ya kutosha kwa kipindi chote Cha kazi nikawabeba vijana wa watu mpaka kwenye kampuni.

Baada ya mwezi mmoja walibaki vijana watatu wengine walirudi makwao somo kubwa nilolijifunza ni kazi kama hujawahi kuifanya unakuwa huna Authority ya kusema kazi ni nzuri au ngumu.
 
Umeonyesha jinsi Gani ulivyo mweupe kichwani.? Mtu kukusaidia ndio Kuna mpa mamlaka ya kucontrol fikra zako na maamuzi Yako?

Kwa vile naogopa kuharibu heshima ya Mzee ndio nifanye kazi ambayo I'm not interested je siku nikisababisha loss kutokana na kuchukia kazi nani Atakuwa accountable?

Maisha ni machaguo it's doesn't means kufanya kazi(kuajiriwa) ndio kufanikiwa Kuna baadhi ya kazi zaweza kuwa ndio chanzo Cha anguko lako.

And don't think I'm young and stupid like you I'm grown man who can takes risk just to make dreams come true.
 

Hiyo ndio sababu wenye connection hawataki kuwapa Vijana wengi kazi Kwa sababu ya upuuzi Kama huu.
Wakati ukiomba mtu unavyolalama na kuomba msaada.
Mtu anakuambia Hana kazi, lakini unakazania kazi yoyote tuu.
Unapewa kazi unaleta utoto
 
Mimi nashauri kabla hujaacha kazi tafuta kwanza mume mwenye hela akuoe ili uwe comfortable maana hakunaga kazi rahisi. Watu kama nyie ni laana kwa taifa. HAMSAIDIKI. Ukiacha kazi utamharibia sana huyo dingi asiaminike pia utawaharibia wengine wasisaidiwe na huyo mzee mwenye utu wake. Tatizo ninaamini kwenye ndoa ya mke mmoja ningeweza kukutolea posa. Wewe ni aibu ya taifa. Umeandika ushuzi mtupu na kiingereza chako cha juhudi binafsi. Vijana wa kiume mnazidi kuharibika tu HAMUAMINIKI. Pumbavu sana. Kuna mwenzako aliacha kazi Kigoma ili apate tu nafasi ya kushinda klabuni pale jangwani. Nitakuunganisha nae ili akushauri.
 
Hiyo ndio sababu wenye connection hawataki kuwapa Vijana wengi kazi Kwa sababu ya upuuzi Kama huu.
Wakati ukiomba mtu unavyolalama na kuomba msaada.
Mtu anakuambia Hana kazi, lakini unakazania kazi yoyote tuu.
Unapewa kazi unaleta utoto
Yupo ambaye aliacha kazi Kigoma kwasababu tu anakuwa mbali na klabu yake. Huwa anashinda klabuni pale Jangwani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…