Naomba ushauri kuhusu biashara yangu inakoelekea inaenda kukata roho sio muda

Dah hii kweli
 
Nkamu umenikumbusha mbali sana, huo mchezo niliwahi kuchezewa dukani waliniwekea soda… 😂😂😂
Mteja wangu alikuja akaniambia naona umebadilisha biashara, namuuliza biashara gani ananiambia anaona vinywaji 😹😹

Kuna watu mafala sana
 
Mbagala kawaida me mwenyewe nipo mbagala nauza viatu vya kike nilikuwa nauzia ndani kule stendi ndogo nimepata hasara siuzi nyingi nikahamia puma kule hasara siuzi kabisa nataka kupakimbia kodi nimelipa miezi 4 nina wiki moja
Miezi minne ushakata tamaa?? 😹😹
Mwanzo ulikuwa unafanya biashara gani?
 
Anza kutafuta mama lishe na wale wapishi wanaopika kwenye masherehe, halafu mchele wa 1400 au ulitaka kuandika 2400?
 
Watu hawanunui wanapita tu tena wengi hela ya kula nakosa me nauza viatu vya kike ila eneo nilipo wote vya kiume
Hapo ndipo ulipokosea, ilitakiwa na wewe ungeweka biashara ile ile km ya wenzio, huo mtaa wateja washazoea wakija wakute viatu vya kiume, wewe umeweka vya kike ni ngumu..!

Km ulitaka kuuza vya kike basi ungeenda mtaa ambao wanauza vya kike na wewe ungeuza..!
 
Sawa kwa hiyo kuhama sahihi niache kodi
 
Anza kutafuta mama lishe na wale wapishi wanaopika kwenye masherehe, halafu mchele wa 1400 au ulitaka kuandika 2400?
unashangaa mchele kilo 1400 huamini au.. mbona ndio bei ya kuanzia sehemu nyingi tu dar huku gongo la mboto bei inaanzia 1500 kilo mchele umeshuka bei sana mkuu
 
Napambana ila napoteza tu kila siku mzee mpka kwenda kufungua ofis mtu unaona kaziii kwasabab unajua kabisa naenda kuuza mzgo ambao haunipii faida yani kama nacheza tu na mwisho wa mwezi watu wanalamba kodii zao daah
Bora wewe kinaeleweka,Faida utapata tuu mkuu tunakoelekea ni pazuri miezi ya sikuku na wakulima wanajiandaa na mashamba, mchele utapanda nawe utapata Faida kubwa,Mungu Mwema
 
Huyu anahangaika pale kuna ulozi mkubwa tu. Mbagala ile ina mambo mengi sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…