Naomba ushauri kuhusu biashara yangu inakoelekea inaenda kukata roho sio muda

Inawezekana unakonunua mchele wanakukata.

Pia angalia mzani wako, hebu pima mfano kilo tano kaombe mahali uzipime uone mzani wako.

Unless otherwise muuzaji wako anakukata
 
🀣🀣🀣🀣 Hii michezo ipo nkamu,unashangaa tu unasalimiwa shikamoo Bibi,hujui kumbe umewekewa sura ya kikongwe....watu ni wabad
 
[emoji14][emoji14][emoji14]
 
Achana na biashara kichaa hizo za wavivu , njoo Chunya tuumize kichwa kwenye dhahabu
 
🀣🀣🀣🀣 Hii michezo ipo nkamu,unashangaa tu unasalimiwa shikamoo Bibi,hujui kumbe umewekewa sura ya kikongwe....watu ni wabad
Wabongo kwa ulozi aisee , sijui kwanini hii teknolojia hawaitumii kutokomeza wahalifu mitaani na watekaji vibaka wa uvccm wanaotesa wananchi kwa kuwaua na kuwateka ovyo
Wanatumia kukomoana wao mitaani .
Ni kama wale washamba wa kule Haiti , nchi ile ina master wa uchawi mkali wa Voodoo ila shangaa nchi imejaa wahalifu na magenge ya wauaji mitaani wanaua watu na kuwatesa mitaani
 
Usibadili biashara,fanya matangazo hapo hapo kwa kutumia spika,ajiri watu wawapitie watu majumbani,shuleni.
 
Eneo, Eneo unafanya biashara katika eneo lenye umaskini kimbia apo huo wa 1600 utashangaa kuna maeneo unauzwa 2000,tafuta eneo zuri ndugu.
Hiyo ni sahihi nishafanya research sehem nyingine mchele bei zipo poa sana sina uhakika kweny mzunguko tu
 
Mimi nakushauri bila kupepesa macho, badilisha biashara au punguza mtaji wako kwenye hio biashara uanzishe nyingine. Biashara ya mchele pasua kichwa. Unaweza kumaliza mtaji.

Kama bado hujafanya maamuzi ya kuacha basi badili location ucheki.
Nashkur kk ntafanya hivo aisee
 
Umeongea point kaka nimejaribu njia zote zinadunda natoka naenda nkaaa maporini huko wiki nzima kutafuta vitu vizurii lakini wapiiiii naishia kuambulia patupu
Pole mkuu...

Ila unatakiwa ujue kwamba asilimia kubwa ya watu ambao wamefanikiwa kwenye maisha ya utafutaji hasa kupitia kwenye upande huo wa kibiashara ni kwamba wameweza kujiungamanisha na upande wa kiroho iwe kwa kujua au kwa kutokujua na iwe upande wa kiroho wa gizani au upande wa kiroho wa nuruni, huwa haijalishi Ila nguvu za umiliki huwa haziko upande huu wa damu na nyama bali zipo upande wako wa pili ambao ni upande wa kiroho.

Kwahiyo Kuna watu ambao walijaribu biashara nyingi sana ambazo zote hazikuwapa mafanikio Ila baadae walikuja kukutana na biashara moja tu ambayo walivyoamua kuifanya hapo hapo wakaanza Kuona mafanikio ambayo hawajawahi yaona kwenye biashara nyingi walizowahi kuzifanya na hii biashara ndio tunasema sasa kwamba inayo muunganiko wa moja kwa moja na upande wako wa kiroho Kwahiyo inakuunganisha pasipo wewe mwenyewe kujua.

Inawezekana hujaelewa hapo Ila nakuhakikishia kwamba biashara ni kama mila na desturi zilizopo kwenye makabila, kwamba Kuna mila inaaminiwa sana na kabila fulani na wanaifuata kwasababu inawapa matokeo wanayoyataka pindi wanapoifuata Ila wewe mtu wa kabila lingine ukienda kuifuata hiyo mila haitakupatia chochote unachotaka kwasababu wewe asili yako haiko huko Kwahiyo na wewe ukitaka ufanikiwe kwenye mambo ya kimila nilazima ufuate zile mila ambazo zinafungamana na asili yako.

Tukirudi kwenye biashara ni the same, biashara ambayo inampa faida kubwa sana rafiki yako wewe ukienda kuijaribu unaweza usifanikiwe hata kwa japo faida kidogo, sana sana utapoteza mtaji wote huko kwasababu hiyo biashara haifungamani na wewe kiasili ila biashara hiyo hiyo ambayo wewe hufanikiwi nayo unakuta Kuna rafiki yenu mwingine kwenye hiyo cycle yenu nae anajaribu kuifanya ghafla anafanikiwa, sasa wewe unaweza kujihisi unagundu na mikosi ila wala sio kweli ni vile tu haujui namna ya ulimwengu unavyofanya kazi.

Kuna biashara ambazo zinafungamana na watu fulani fulani na Kuna biashara ambazo hazifungamani na watu fulani fulani.

Najua ni mambo ambayo yanashangaza halafu yamekaa kufikirika fikirika sana, ila ndio asili ilivyo na ndio maana always unaambiwa dunia inaendeshwa na watu wenye nguvu, sasa watu wenye nguvu sio kwamba wako na misuli mingi, hapana ila watu wenye nguvu huwa wanajua namna universe inavyofanya kazi na ndio maana unaona matajiri wengi huwa wanawekeza pesa nyingi kwenye vistartup venye idea nyepesi sana wakati wangeamua wangeweza kununua hizo algorithm na kuzifanya wao wenyewe ila wanafanya hivi kwasababu wanajua sio kila biashara lazima wewe uwe main player lakini unaweza kutembelea migongo au nyota ya watu wengine kwa kuwekeza kwao kwenye zile biashara ambazo zinafungamana na wao moja kwa moja na ukaendelea kula share zako kwa kadri ya ulivyowekeza.

NB
Hii ni code nimewafungulia sasa unaweza ukapita nayo au ukaipita... Yesu mwenyewe alikua fundi selemala kwani unadhani hakuona kazi zingine za kufanya πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†.
 
Hiyo asili yangu ya biashara ntaijuaje...?!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…