Naomba ushauri wenu kuhusu biashara ya ufugaji wa kuku wa mayai

Safi sana uko vizuri.
 
Vip mfumo wa kutumia cage
 
Inategemea na nguvu yako, fanya a well calculated business, kulisha kuku 500 miezi 6 inataka msuli kidogo
Umenena vyema, lazima awe na mtaji kwa kuwalisha angalau kwa wiki 20-22 watakapokuwa wamechanganyia kutaga. Layers kutoka Silverland wanakula chakula gram 130-150 kwa siku. Hawa kuku hawana changamoto kubwa kwenye matunzo kama una mtaji na umepata abc za kutosha. Ili kuona faida yake angalau uwe na kuku 500 na kuendelea. Mabanda yakiwa yamejengwa kisasa na ukizingatia usafi, chanjo, na madawa hawatakupa shida kabisa.
 
Vip mfumo wa kutumia cage
Cage ni gharama sana mkuu, kama una eneo la kutosha hakuna ulazima. Cha msingi anawawekea viota vya kutagia na anaviwekea pumba haswa za mchele ambazo sisi huku tunabeba bure, gharama yako ni usafiri na watu wa kupakia tu. Nitashare picha ya hicho kiota, kinatengenezwa kwa mbao na kuwekewa partition, hii itazuia sana mayai kupasuka.
 
Inabidi nipate elimu jinsi ya kuandaa hivyo vyakula aisee
Ninazo formula, ila itabidi nipekue nishee nawe. Ila hata wenye mashine za kusaga wanazo hizo formula. Cha msingi ni muhimu mtu awepo mashineni wakati wanasaga hicho chakula ili uhakikishe vitu vyote muhimu vimewekwa. Kuna mashine wale vijana ni wezi kwelikweli, watapita na hizo vitamin, minerals wakapigie smart Gin, nk.
 
Gharama kwenye kuzinunua au kuzitumia kuhudumia kuku?
 
Nimekumbuka newcastle na gomboro
 
Naomba ushee nami hizo picha tafadhali
 
Kwenye mchanganuo wa gharama haujaweka gharama za maji, umeme na kibarua/msimamizi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…