Wakuu, Shkaamooni. Mimi ni kijana mdogo ambae niko kwenye ndoa tayari. Ndoa yangu ina miezi kadhaa tu, haijafikisha hata mwaka mmoja.
Wiki kadhaa nyuma tulikuwa tukipishana sana na mke wangu sababu ya mimi kuwa busy sana mpaka mida ya usiku mimi nipo busy na kazi.
Hii ikapelekea mimi na mke wangu tugombane mpaka malalamiko kufikia kwa wazazi.
Malalamiko ya mke wangu kwa wazazi wangu ni juu ya ubusy wangu na kupelekea kukosa muda na mke wangu, na mimi nikajitetea kwamba nina project zinazonibana sana nikashindwa hata kuwaza mambo mengine tofauti na project inayonikabili.
Nilitoa sababu hio japokuwa ndani ya nafsi yangu kuna malalamiko mengine ambayo nimeamua kufa nayo kiume siku hiyo.
Jambo la kwanza ni kuhusu hali ya mwenza wangu kuwa na matatizo ya hedhi, hili tatizo alikuwa nalo muda mrefu sana na mpaka wazazi wake waliwahi mwambia kuwa anaweza pata shida kwenye kutafuta mtoto. (hili aliniweka wazi baada ya kubleed kwa miezi miwili mfululizo).
Jambo la pili ni ubora wa shughuli. Yaani sipati kile nilichokitarajia.. ila hii sio tatizo kubwa kwangu as long as tabia zake zinaniridhisha.
Sasa mpaka naandika uzi huu.. Mzee(Baba yangu) aliniuliza swali ambalo limenipa hasira na kuniweka na mawazo sana. Ameniuliza kama nina tatizo la mwili nimwambie nisimfiche ( yaani kama sina nguvu za kiume nisifiche ).
Hili swali limenikwaza sana na limenipa hasira mpaka napatwa na mawazo ya kishetani. Najisemea au nikamtie mtoto wa mtu mimba ndo akili iwakae sawa hawa mana naona kama dharau hivi.
Naombeni ushauri nifanyeje kwenye hii situation?
Je ingekuwa wewe ungefanyaje au kama uliwahi pitia je ulikabiliana nalo vipi?