Naona Syria inaenda kuwa uwanja wa vita kati ya Iran na Israel; sijui Assad amekubalije nchi yake kila mtu kujikatia kipande chake

Israel na Iran ni nchi mbili ambazo ziko kwenye vita kwa muda mrefu ingawa ni vita isiyo rasmi (de facto war). Pengine wengi hawafahamu hili.

Iran imekuwa ikifadhili makundi ya wanamgambo yenye itikadi tofauti-tofauti pale mashariki ya kati ili kuishambulia Israel huku Israel nayo ikitumia majeshi yake na vyombo vya kijasusi kuishambulia Iran kwa namna mbalimbali ikiwemo kushambulia makundi ya wanamgambo ama kufanya mashambulizi ya kuhujumu (sabotage) mipango yake ya nyuklia ndani ya Iran.

Shambulizi lililofanywa na Israel katika eneo la ubalozi wa Iran pale Damascus ni muendelezo tu wa vita ya muda mrefu ya chini kwa chini.

Kwa mtazamo wako unafikiri kwamba Israel imeshambulia ubalozi wa Iran, ila kwa mtazamo wa kijeshi ukizingatia hizi nchi mbili ziko kwenye de facto war, ukweli (fact) ni kuwa, jeshi la Israel limeshambulia jeshi la Iran lililoweka kituo cha kijeshi katika eneo la ubalozi.

Jiulize maswali haya mawili ya msingi sana:

1) Majenerali wa IRGC waliouawa na Israel walikuwa wakifanya nini ubalozini?

2) Je, majenerali wa IRGC ndio mabalozi ama wanadiplomasia wa Iran?
 
Ndoto za mchana
 
Serious kabisa jeshi linachukua maamuzi ya kushambulia ubalozi wa taifa lengine wale watu ni vichaa wanaopewa backup na vichaa wenzao wa magharibi.
Naona wengi mna mtazamo kwamba kilichoshambuliwa ni ubalozi. Ni kweli kwamba mashambulizi yalifanywa katika eneo la ubalozi wa Iran. Ila tujiulize maswali haya mawili kwa kina:

1) Majenerali wa IRGC waliouawa na Israel walikuwa wakifanya nini ubalozini?

2) Je, majenerali wa IRGC ndio mabalozi ama wanadiplomasia wa Iran?
 
Watu msio na akili mnaongea as if Iran ana uwezo huo, huo msafara wa Iran utateketezwa kabla ya kufika Syria na US yuko front line soon utaona moto unawaka Tehran and Ayatollah atakamatwa mchana kweupe na kuuawa mkiona, sasa US and Israel ndio wakati walisubiri sana kuiteketeza Iran na middle East itatulia, ni plan ya miaka karibu 40 ya kuiteketeza Iran na hii plan ilipangwa kwa kuipunguza nguvu za Russia kijeshi kwa vita vya Ukraine, sasa Iran atapigwa peke yake kwani Russia hatamsaidia ana vita yake kali na Ukraine.,

Sasa plan imekamilika kumpiga Iran kwani hakuna wa kumsaidia, watu wengi hawajui US ni Israel and vice versa, kwani wayahudi ndio wanaongoza US na dunia hii kwa sasa, Iran inaenda kuangamia moja kwa moja na hicho ndio kipo Washington kuichakaza Iran na itakuwa kama Libya, Iraq, Afghanistan or Syria
 
🤣 marekani ameshasema hausiki na uchokozi wa Israeli kwahiyo Iran akiamua apige popote anapotaka
 
Huyo Iran kama anataka kupiga apige amalize hasira zake haya masuala ya wayahudi kushinda kwenye mahandaki , balozi 28 zimefungwa watu wanakosa huduma binafsi naona siyo sawa ni kuwajambisha wayahudi bila sababu ya msingi.
Week sasa ime isha mnashusha ngonjera tu mbona hampigi?????
 
Bwana Yesu Asifiwe.
 
Hicho unachokilalamikia ndicho anachofanya Israel dhidi ya palestina.

Kama wao hawataki kuanzishwa taifa la palestina basi ni halali na wao kufutwa kwenye uso wa dunia
 
Acha kujidanganya kuwa syria inaweza kuwa uwanja wa vita. Pale syria Russia ana masilahi yake na kitambo yupo pale kulinda masirahi yake

Israel kama anataka kufanya syria kuwa uwanja wa vita, basi atakuwa anafanya kosa lingine kubwa sana
 
Izrael hampigi mtu au kumshambulia sehemu bila kufanya tafiti

Irananajua alichokuwa anajifanya kwenye ubalozi kwa kufanya jengo hilo kuwa Kambi ya kijeshi na sehemu ya kuleta wanajeshi wa Iran kuwachanganya na magaidi wa palestina
 
Huo ubalozi unawakilishwa na wateule wa utawala uliopo madarakani
Lakini najiuliza Israel ilishambulia bila kuwa na uhakika wa ukiukwaji wa kidplimasia Kama operation za kijeshi NDANI ya ubolozi
 
Izrael hampigi mtu au kumshambulia sehemu bila kufanya tafiti

Irananajua alichokuwa anajifanya kwenye ubalozi kwa kufanya jengo hilo kuwa Kambi ya kijeshi na sehemu ya kuleta wanajeshi wa Iran kuwachanganya na magaidi wa palestina
Huna akili. Utetezi wa kijinga sana. Kwahiyo unahalalisha nchi kufanya mashambulizi ya kijinga kwa hisia
 
P
Kushambulia ubalozi wa taifa lengine kwa jeshi na serikali inayo jitambua ni sahihi ?
Je Kama ubalozi utakuwa sehemu ya kupangia mipango ya kumshambulia taifa jingine ukilipuliwa ni kosa
Kwa mfano Tiss iwe na taarifa za uhakika kwamba ubolozi wa Marekani inatumika kufanya mipango ya kijeshi kumshambulia Tanzania
Sisi tukawawahi kuwalipua ni kosa ?
 
Ila inaonyesha msafara mkubwa wa magari ya Iran kuelekea Syria
Dah….wat mna vituko sana. Wewe huo msafari wa magari ya Iran kuelekea Syria umeuona wapi? Unapita wapi?
Ule msafari wa wale wana mgambo wa Houth kuelekea Gaza uliishia wapi?
Nyie kile siku mnaibuka taarifa za vitu mnavyo tamani viwe badala ya kuleta taarifa za uhalisia uliopo.
 
Hata usipong'olewa mkuu
Kuna hatari ya kudhoofishwa Sana
Kama Asad
Busara ya Ayatollah ni kutulia
Maana mageneral wanafanya nini kwenye ubalozi ni wanadiplomasia
 
🤣 marekani ameshasema hausiki na uchokozi wa Israeli kwahiyo Iran akiamua apige popote anapotaka

Hiyo ni lugha ya diplomasia ya nchi zozote asionekane anaonea nchi zingine, kama huamini, subiri hii vita US ndio anaenda mpiga Iran na Iran anapotezwa moja kwa moja, mark my words..!!
 
Siku ukisikia USA nayo inatoa wakimbizi Isreal nayo inaicha ardhi za waislam na wanakimbilia kwa Germany
Inawekana us kutoa wakimbizi Ila ni ngumu sana
Ila Israel kuachia Tena Ardhi yake ni ngumu kwa nyakati haiwezekani kwa nyakati hizi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…