FRANC THE GREAT
JF-Expert Member
- May 27, 2016
- 5,500
- 8,060
Israel na Iran ni nchi mbili ambazo ziko kwenye vita kwa muda mrefu ingawa ni vita isiyo rasmi (de facto war). Pengine wengi hawafahamu hili.Kwa alichokifanya Israel si kwamba ameshambulia utawala wa Iran. Alichokifanya ni kuishambulia Iran. Hilo inabidi ulielewe.
Unachokifikiria wachambuzi wa historia wanasema ndilo kosa lilimgharimu USA wakati wa vita ya Korea kaskazini na Korea kusini. USA ilidhani raia wa China hawatoingia vitani nao kwa kuwa utawala wa China wa Mao unaonekana ukiwadidimiza raia wake.
Kumbe kwa wachina ni tofauti. Matatizo ya ndani ya nchi yao watayamaliza wenyewe ila ukivamia nchi yao wataungana na kupambana na wewe kwanza.
Hili ndilo wengi humu tunashindwa kulielewa: Wengi wanasema utawala wa Ayatollah utang'olewa. Lakini hawajui kuvamia ubalozi wa nchi nyengine kuna maanisha nini! Kwa ufupi Israel imefanya makosa makubwa sana. Kwa hii hali ni kuangalia busara ya Iran itaamua vipi! Na kwa kutaka kufahamu ni kosa kubwa angalia anachopitia Israel kwa sasa. Mara afunge balozi, nchi yote kaiweka kwenye hatari ya kivita n.k
Iran imekuwa ikifadhili makundi ya wanamgambo yenye itikadi tofauti-tofauti pale mashariki ya kati ili kuishambulia Israel huku Israel nayo ikitumia majeshi yake na vyombo vya kijasusi kuishambulia Iran kwa namna mbalimbali ikiwemo kushambulia makundi ya wanamgambo ama kufanya mashambulizi ya kuhujumu (sabotage) mipango yake ya nyuklia ndani ya Iran.
Shambulizi lililofanywa na Israel katika eneo la ubalozi wa Iran pale Damascus ni muendelezo tu wa vita ya muda mrefu ya chini kwa chini.
Kwa mtazamo wako unafikiri kwamba Israel imeshambulia ubalozi wa Iran, ila kwa mtazamo wa kijeshi ukizingatia hizi nchi mbili ziko kwenye de facto war, ukweli (fact) ni kuwa, jeshi la Israel limeshambulia jeshi la Iran lililoweka kituo cha kijeshi katika eneo la ubalozi.
Jiulize maswali haya mawili ya msingi sana:
1) Majenerali wa IRGC waliouawa na Israel walikuwa wakifanya nini ubalozini?
2) Je, majenerali wa IRGC ndio mabalozi ama wanadiplomasia wa Iran?