Nimesoma kwa makini sana kila ulichokileta hapa, ndugu. Detail kwa detail!
Moja ya changamoto ambazo nimeziona kwako ni lugha hasa kiingereza. Nitatumia makala uliyoileta wewe mwenyewe ili kukuonesha hiyo changamoto uliyonayo.
Kwanza kabisa: hakuna mahali nimetaja kitu kinachoitwa "central command". Hiki kitu umekuja nacho wewe. Na wala hiyo "central command" sio hoja ya kuthibitisha kwamba Hezbollah inatakiwa kuwa na hiyo "central command" mahali fulani ndipo ijiendeshe kijeshi mahali husika.
Hiyo "central command" ni nini hasa?!
Issue ni kwamba, umechanganya kati ya hiyo "central command" yako uliyoitaja na kitu kingine kinaitwa "command center". Ndio maana nimesema tatizo lugha!
Sasa nikusahihishe:
Command center ni kituo cha kijeshi ambacho hutumika kufanyia vikao vya maamuzi ya kijeshi ikiwemo kuratibu na hatimaye kufanikisha shughuli, mipango na mikakati ya kijeshi ama kivita. Na mara nyingi hizi command centers zinakuwa katika kambi za jeshi.
Turejee kwenye suala la kujiendesha kijeshi:
Kujiendesha kijeshi ni kufanya shughuli za kijeshi [kwa lugha rahisi]. Kwa kiingereza tunaita "operating militarily" ama "operate militarily". Hicho ndicho kitu Hezbollah inakifanya pale Syria. Kuna mahali kwenye post iliyopita nimetumia maneno "ina-operate kijeshi" kwa sababu nilishaanza kuhisi changamoto ya wewe kutonielewa.
Rudi kwenye makala (article) uliyoileta hapa:
View attachment 2959063
Zingatia maneno; "Hezbollah fighters have operated". Hilo neno "operated" ndio maana halisi ya kujiendesha kijeshi.
Hezbollah ina kambi za jeshi (training camps) na command centers pale Syria kwaajili ya kuratibu operesheni za kijeshi ikiwemo kusimamia supply lines za silaha kutoka Iran kuelekea Lebanon na pia kutoa mafunzo ya kivita kwa wanamgambo na wanajeshi wa jeshi la Syria pale Syria. Huko ni kujiendesha kijeshi nchini Syria.
Vyanzo vingine:
View attachment 2959067
Zingatia hayo mambo matatu hapo juu:
military bases, observation points and security groups.
Syria kwa Hezbollah ni upande wa ziada wa mapambano ya kijeshi dhidi ya Israel. Zingatia, ISRAEL. Soma ile makala uliyoileta wewe mwenyewe hapa!
View attachment 2959075
Zingatia sana hapo panaposema:
Hezbollah views its organization as the front line in the confrontation with Israel, and sees Syria is its rearguard.
Hizi hapa chini ni sababu za kwanini Hezbollah inamsaidia Assad pale Syria. Zingatia sana hapo panaposema:
Nasrallah continues to portray Hezbollah’s involvement in Syria as a confrontation with Israel, the West, and Sunni extremists.
Israel ndiye adui namba moja wa Hezbollah ndio maana Hezbollah imeweka kambi pale Syria kwa jina la "kumsaidia Assad". Soma article vizuri!
View attachment 2959100
Haya yote niliyoyaeleza [nikinukuu article uliyoileta] ndio sababu za kwanini Israel inafanya mashambulizi dhidi ya Iran, Hezbollah na makundi mengine ya wanamgambo pale Syria.
Kwa mara nyingine, asante kwa hiyo article uliyoileta hapa. Imesaidia kuuweka huu mjadala vizuri zaidi.