Naona vyuma vya China tutaanza kuvizoea sio muda. Ona ili Zeekr 9X SUV!

Umesema vyema, wengi bado wana mentality ya China ya miaka ya 1980-1990

CEOs wa kampuni za Ulaya wanakiri wana mengi ya kujifunza kutoka China kwenye EVs

Na imethibitika kuwa vyuma vya Mchina vinahimiri barabara za Afrika. 70%+ ya trucks na buses Tanzania ni brands za China

Sahihi SONY Bravia imeingia mkataba kwa sasa mchina TCL ndio watakuwa watengenezaji wa hizo TV
 
Kuna zile pikipiki za China, Sanlg na Haojooe zinabeba sana mkaa kupeleka Dar. Injini zake ndizo zimefanya pikipiki nyingi za Honda na Yamaha kuendelea kuwepo mitaani.

Kama vya China kweli havidumu, zile pikipiki zisingeweza kutoboa hata mwaka kwa namna zinavyotumika, maana zinapakia mzigo mkubwa na milima zinapanda bila shida.
 
Hii sio sababu mkuu zile pikipiki za kichina hazina uwezo wa kuhudumu kwa miaka 15 wakati makampuni mengine ni zaidi ya miaka 15 na tunanunua mitumba hii ni tofauti kubwa.
 

Nazungumza kitu ninachokifahamu kwa zaidi ya unavyofikiria. Na nimekutana na wataalam wa kichina katika shughuli mbalimbali za kimataifa.

Watu wengi hawajui kabisa kuhusu masuala ya kiuchumi ya China. Fahamu yafuatayo:
1. China ndiyo nchi inayoongoza kwa kuwa na makampuni mengi ya kigeni nchini mwake, hasa kutoka Ulaya, America na nchi chache za Asia kama Japan na HongKong.
2. Makampuni hayo mengi ya kigeni yakitengeneza bidhaa zake nchini China yanauza bidhaa zao kwenye mataifa yalikotoka. Na hizo bidhaa huwa na ubora sawa na kule yalikotoka.
3. Makamljni mengi ya kigeni yanaenda kuwekeza China kwa sababu gharama ya uzalishaji iko chini sana nchini China, na jambo la pili wachina wengi wenye uwezo kifedha hawapendi kununua bidhaa zilizotengenezwa kwenye viwanda vya wachina wenzao kwa sababu ya uduni wa quality and reliability.

4. Makampuni mengi yanayomilikiwa na wachina, soko la bidhaa zao ni kwenye mataifa maskini.

5. Miaka ya karibuni, makampuni mengi ya wachina yenye uwezo mkubwa wa kifedha yamekuwa yakitoa offer kubwa kupindukia kuyanunua makampuni ya kigeni ambayo tayari yana majina ya ubora ili kuweza kupata soko la Ulaya na Marekani.
6. China ndiyo nchi inayoongoza katika wizi wa tekinolojia, na imekuwa ikitumia gharama kubwa sana kuwapeleka kwenye mataifa ambayo inaamini yana tekinolojia za juu, hasa Marekani, Ujerumani na Japan. Na ikifanikiwa kuiba, kitu hicho hicho kilichokuwa kikiuzwa labda dola 10,000, yenyewe inaweza kuuza dola 2,000; japo haiwi na ubora kama wa mtengenezaji asilia lakini wengi watakuwa na uwezo wa kununua na kutumia.
7. Makampuni yote ya kigeni yanayopewa contracts za kazi nchi China, ni lazima contract ihusishe kazi iliyokusudiwa na transfer of technology. Na hilo limeisaidia sana China. Fikiria miaka ya nyuma reli SGR za China zilijengwa na wajerumani, kwenye package ya contract ya dola bilioni 31 ilihusisha na transfer of technology na training kwa wataalam wa China, leo China inajenga SGR kwenye mataifa mengine, hasa Afrika.

Sasa hivi kuna jitihada kubwa na programs mbalimbali za baadhi ha wachina kutaka kutengeneza bidhaa zenye ubora kama makampuni ya kigeni yaliyopo China ili na wao waweze kufaidika na masoko yenye imara na yenye nguvu, ya Ulaya na America. Sector ambazo wamefanikiwa angalo kwa kiasi fulani ni kwenye magari ya umeme na kwenye electronics kwa ujumla.
 
Ni swala la muda
 
Pikipiki za kazi hizo
 
Hii sio sababu mkuu zile pikipiki za kichina hazina uwezo wa kuhudumu kwa miaka 15 wakati makampuni mengine ni zaidi ya miaka 15 na tunanunua mitumba hii ni tofauti kubwa.
Sijawahi kuona YAMAHA, Suzuki wala Honda inayopiga kazi kama Haojue au Sanlg huko vijijini kwenye barabara mbovu
 
2. Makampuni hayo mengi ya kigeni yakitengeneza bidhaa zake nchini China yanauza bidhaa zao kwenye mataifa yalikotoka. Na hizo bidhaa huwa na ubora sawa na kule yalikotoka.
Moja ya sababu ya kuwekeza China ni ili kuwin soko la China nani alikwambia wanatengeneza tu ili wauze nje ya China?
 
3. Makamljni mengi ya kigeni yanaenda kuwekeza China kwa sababu gharama ya uzalishaji iko chini sana nchini China
Yeah kwa sababu ya uwepo wa supply chain, nishati, wataalamu, sera nzuri za China na soko vinawavutia kuwekeza
 
na jambo la pili wachina wengi wenye uwezo kifedha hawapendi kununua bidhaa zilizotengenezwa kwenye viwanda vya wachina wenzao kwa sababu ya uduni wa quality and reliability.
Si kweli, makampuni mengi kama ya kutengeneza magari yameanza kukimbia soko la China kwa sababu ya ushindani kutoka brands za ndani.

Hata magari ambayo ni luxury kutoka Magharibi wanakabili ushindani mkali kutoka kwa luxury zinazotengenezwa China

Hivi karibuni Samsung wamejitoa China kuuza home appliances, Wachina wananunua bidhaa zao
 
5. Miaka ya karibuni, makampuni mengi ya wachina yenye uwezo mkubwa wa kifedha yamekuwa yakitoa offer kubwa kupindukia kuyanunua makampuni ya kigeni ambayo tayari yana majina ya ubora ili kuweza kupata soko la Ulaya na Marekani.
Mengine yamenunuliwa kwa sababu yalikuwa na shida kifedha au ushindani
 

Ukikna bidhaa fulani ya Mchina inatamba Tanzania, usiamini kuwa kila mahali ni hivyo hivyo. Tanzania hatuna taasisi imara zinazoshughulika na ubora wa bidhaa.

Hapa Tanzania, nadhani karibia 90% ya mabasi yote ya abiria ya safari ndefu ni ya mchina, lakini usidhani hali ipo hivyo katika nchi. Hata hapo Afrika Kusini tu, mabasi mengi ya safari ndefu, siyo ya China.

Ulaya, mataifa kama Norway na Finland yanaendelea na uchunguzi kuhusiana na mabasi ya umeme ya kampuni ya Yutong kwamba yana switch ambazo wameziita ni killer switch, ambazo ni hatari kiusalama. USA inatarajia kupiga marufuku magari yote yanayotengenezwa China mwaka 2027 kwa sababu za kiusalama:

.Chinese-made electric buses are facing serious security scrutiny in Europe and Australia due to potential "kill switches" allowing remote deactivation by the manufacturer, posing significant infrastructure risks. Investigations have revealed that Yutong and other Chinese-manufactured buses could be remotely disabled.
 
Kwa nini na nyinyi msiibe kama ni rahisi?

Je, ulijua kuwa China ndio inaongoza kwa patents nyingi duniani na sasa ndiye kinara wa kumwaga kibunda kikubwa kwenye R&D?
 
Wajerumani ambao ni wagunduzi wa engine ya kwanza ya gari za kisasa, leo CEOs wa kampuni zao kubwa za magari na team za wataalamu wako China kujifunza modern features za EVs

Teknolojia haina mmiliki, tuko kwenye dunia ya innovations
 
Tayari wanauza bidhaa zenye ubora ndio maana Ulaya, Marekani na Oceania ni soko la bidhaa za China
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…