Naona vyuma vya China tutaanza kuvizoea sio muda. Ona ili Zeekr 9X SUV!

Naona vyuma vya China tutaanza kuvizoea sio muda. Ona ili Zeekr 9X SUV!

Kesi yangu mimi na Mchina ni moja, Sijawahi mwamini mie hapa kwenye reliability.😁
Toka aliponiuzia trekta ikatengeneza ufa kwenye engine block, na kuchanganya mafuta na maji, sinaga hamu nae.
Mchina anataka ununue kitu, ukitumie, kikulipe kwa muda mfupi ukanunue kingine.
Hahaha, na ndivyo inavyopaswa kuwa mkuu, shida ni kodi na umasikini wetu. Mfano hilo trekta ungelinunua bei ndogo, kwanini uhitaji ukae nalo miaka mingi? Miaka mi3 mpaka mi5 unavuta jipya.
 
Kwa matoleo yapi.. chini kabusa kuna vile vibata mbuzi, vile alitumia babu mpaka mjukuu anatumua vile tulibatiza jina tukaviita mchaga, kisha juu yake kuna kina DT na ndugu zake.
Hizo kazi zinazopiga hizo haojue zako, pikipiki miaka mi5 mingi inakuwa imekongoroka hatari ya mungu, pikipiki inachoka ukiimwagia mchuzi mbwa anaweba ibeba akijua mifupa. haitamaniki..
Tunataka ipige kazi na idumu.. kwenye ishu ya kudumu mchina ana changamoto kubwa kwenye product zake nyingi sana

Ila mchina binafsi namkubali sasa hivi, kwenye vyombo vya moto hatuhitaji tena gari la kukaa miaka 20 na bado naliuza used likae miaka 30 tena. Tech imeingia kwenye magari. Yawe kama simu tu, yauzwe cheap, yakae mda mfupi. miaka mi5 mi5 tubadili.
 
Hivi simu ni kweli zinauzwa cheap? Kuna mabadiliko ya bei kutoka simu bora za miaka ile na za sasa?
 
Yeah. Kwa mfano, Tesla M3 (from USA) ya 2020 sahivi iko poa. So tukisema ni reliable tunaamini.
Magari mengi kutoka China yamekua maarufu Tanzania hivi recently 2025/26, ngoja tusubir

Mfano ikiwa used 4-5 years bei itakua poa sana. Wanyonge tutazicheki.
Bado Chinese cars are disposable.

Miaka 15 hiyo gari itakuwa imechakaa hutaamini.

Bado Japanese cars are reliable after 20 years of use.
 
Yamaha na Suzuki zipo serikalini tu huwezi ona zimebeba mikaa pia hakuna mwananchi wa kawaida anayenunua hizo pikipiki. Bei yake ni kali sana.
Yamaaha/suzuki moja ni sawa na kununua kinglion 3
 
Kuna hii plugin-hybrid (engine + kuchaji) full sized SUV Zeekr 9X kitu cha 2025.
View attachment 3585717
Engine yake ni 2.0L turbo i4, battery la 55 kWh au 70 kWh, kwa pamoja (full tank + full charge) unaenda kilometa 1,200+
View attachment 3585718
Ni full SUV, kwahiyo kubwa karibia urefu wa mita 5.2, seat arrangement 2:2:2 so ni nzuri kwa familia kubwa.
View attachment 3585720
Kwa 0 km unaipata kwa 64,000 USD kabla ya usafiri kuja Tanzania na kodi (TRA). View attachment 3585723
Hope zikija Tanzania ni RHD.

Kwa taarifa tu ni kuwa; kwenye hizi gari za kutumia umeme China imeshika takriban 80% ya world market share.
na battery nzuri zaidi za magari ya kucharge duniani hutoka China....
Kwa hiyo miaka sio mingi sana China inaenda kudominate world market....ni suala la muda tu...
Lakini pia soko la karne hii linaenda na fasheni na innovation. Kwa hizi gari ndogo SUV & Saloon, Gari la kudumu miaka 15 litakuwa halina nafasi na ndio sababu hizi saloon car wazungu huziuza ndani ya miaka 5hivi....na kununua nyingine zilizopo kwenye fasheni
CHINA WAMESHASOMA HIYO GAP NA WANATEMBEA NAYO.....
 
Hiyo pikipiki gani?

Miaka mi3 tu, hizo zote zimekufa,
Swala liko palepale HAZIDUMU.
Miaka 3, hivi unajua Sanlg za wasafirisha mkaa nyingi wananunua zikiwa used?. Zile zina miaka si chini ya 10, kaa nao wale jamaa uwaulize.
 
Bado Chinese cars are disposable.

Miaka 15 hiyo gari itakuwa imechakaa hutaamini.

Bado Japanese cars are reliable after 20 years of use.
Na hiki ndio ninachoogopa.

Kweli China wako vizuri kwenye affordable products. Wakati makampuni mengine wanaotoa premiums, wao wanakupa “almost” samw product kwa 1/3 price.

Mfano, Smartphones ile 2012/13 zinafika. HTC, Sony, Samsung, Nokia, BlackBerry walikua wanatupa premiums ila bei zilikua zamoto. Alipoingia Tecno, tukaona ushindani. Ila tatizo likawa disposable. Kwanini, kwasababu anatumia cheap materials ndani na nje. Ingawa miaka 10 baadae tunaona China Smartphones sasa unaweza sema reliable, baada ya muda flani, Huawei, Xiaomi etc naona wamesha catchup na magiants.

Naamini kwenye magari pia ni same. Mapema sana kumpa credits za reliability.

Kuna case zilisikika Huawei na Xiaomi kwenye magari yao wanatumia SoC za simu na tablets. Ambazo inreality haziwezi kustahimili joto na heavy duty. Kwahiyo tuna expect baada ya muda flani gari inaanza kulag.
 
Hivi simu ni kweli zinauzwa cheap? Kuna mabadiliko ya bei kutoka simu bora za miaka ile na za sasa?
Yes mkuu, ukitaka kujua urahisi upo wapi unaangalia uzalishaji na idadi ya wamiliki sio bei ya kipindi kile na sasa sababu inflation na mambo kama hayo. Kwa sasa simu ni cheap, Simu kutegemeana na mnunuzi hata ukiwa na laki na ishirini unapata mpya kabisa.
 
Kwa taarifa tu ni kuwa; kwenye hizi gari za kutumia umeme China imeshika takriban 80% ya world market share.
na battery nzuri zaidi za magari ya kucharge duniani hutoka China....
Kwa hiyo miaka sio mingi sana China inaenda kudominate world market....ni suala la muda tu...
Lakini pia soko la karne hii linaenda na fasheni na innovation. Kwa hizi gari ndogo SUV & Saloon, Gari la kudumu miaka 15 litakuwa halina nafasi na ndio sababu hizi saloon car wazungu huziuza ndani ya miaka 5hivi....na kununua nyingine zilizopo kwenye fasheni
CHINA WAMESHASOMA HIYO GAP NA WANATEMBEA NAYO.....
Used market for EVs litakuwa very brutal.
 
Na hiki ndio ninachoogopa.

Kweli China wako vizuri kwenye affordable products. Wakati makampuni mengine wanaotoa premiums, wao wanakupa “almost” samw product kwa 1/3 price.

Mfano, Smartphones ile 2012/13 zinafika. HTC, Sony, Samsung, Nokia, BlackBerry walikua wanatupa premiums ila bei zilikua zamoto. Alipoingia Tecno, tukaona ushindani. Ila tatizo likawa disposable. Kwanini, kwasababu anatumia cheap materials ndani na nje. Ingawa miaka 10 baadae tunaona China Smartphones sasa unaweza sema reliable, baada ya muda flani, Huawei, Xiaomi etc naona wamesha catchup na magiants.

Naamini kwenye magari pia ni same. Mapema sana kumpa credits za reliability.

Kuna case zilisikika Huawei na Xiaomi kwenye magari yao wanatumia SoC za simu na tablets. Ambazo inreality haziwezi kustahimili joto na heavy duty. Kwahiyo tuna expect baada ya muda flani gari inaanza kul
Ni mapema sana kutoa hukumu.

Muda utatuambia.
 
IMG-20260511-WA0001.jpg

Wanadai havidumu, wenye nchi zao huko wanaujua mziki wa Mchina.
 
Wanaogopa ushindani, nothing else. Hakuna sehemu waliposema issue ni durability wanajua tu Mchina akiingia soko la magari yao ya ndani litashuka
Nilimaanisha wabongo wenzetu ndiyo hudai vya mchina havidumu, huku wenye nchi kubwa (USA & Ulaya) wanamjua vizuri mchina.
 
America ya Kusini na middle East wameanza kutumia gari za Kichina kwa miaka kadhaa sasa na wamezikubali.

Hapa hapa Bongo kuna Cherry gari za Kichina ambazo ukinunua wanakupa warranty ya miaka 10 au 1 million kilometres, hiyo warranty huipati hata kwa mjapan unaponunua gari mpya!

Kuna brands kama JMC anatoa pick up zinakimbizana na Hilux bampa to bampa.

Ukiwa na hela chukua tu chuma uishi/ uendeshe kisasa...

Cha muhimu chukua gari ambayo kampuni yake ina official dealership hapa Bongo... Mchina yuko mbele sana ya muda, mengine umasikini wetu tu! CIAO!
 
Hawa jamaa hawana gari za level ya raum,ist,rumion na spacio maana hivyo vyuma hapo bajeti yake sio masikhara na hapo bado kalkuleta ya TRA.
 
Back
Top Bottom