Napata shaka, kuna kikundi ndani ya CCM kinaratibu kumkwamisha Rais Samia 2025

Sawa mama ake mdogo Samia..

Hivi bado hujajua nchii hii ina umri gani toka ipate uhuru
 
Yaani Rais anaagiza tu ‘Fulani akamatwe’……‘Fulani aachiwe’.

So wrong on multiple levels.
 
Yaani Rais anaagiza tu ‘Fulani akamatwe’……‘Fulani aachiwe’.

So wrong on multiple levels.
Kama DPP ambaye ni presidential appointee anaweza kuagiza nani afutiwe mashtaka, bila explanation, rais ana instruments za kufanya hivyo, hata kama ni kwa kumtumia DPP.

Similarly kwa IGP.

Suppose Rais, kupitia nguvu zake za kupata habari kitaasisi, anaona hapa watu wanaonewa kwa sababu Polisi wanajipendekeza kwangu wanafikiri mimi nataka wapinzani waandamwe, na mimi sitaki wapinzani waandamwe, hapo unataka Rais akae kimya?
 
Rais ana prosecutorial discretion kama DPP?
 
Rais ana prosecutorial discretion kama DPP?
Rais anaweza ku consult na appointees wake wote wakiwamo DPP, AG, IGP.

Akawauliza, jamani, hapa vipi, mbona wapinzani wanakamatwakamatwa? Wamevunja sheria gani?

Akaambiwa mheshimiwa, hapa hamna sheria iliyovunjwa, ni Polisi tu wanajipendekeza kwako, wamesikia kauli yako fulani, wameitafsiri kama umeagiza wapinzani wakamatwe.

Rais akasema mimi sijaagiza wakamatwe. Kama ni hilo tu, sitaki wakamatwe on my account. Kwanza inaniharibia image ya nchi.

Makamanda wakapiga saluti. Wakawaachia wapinzani.

Ndivyo alivyofanya Kikwete hivyo. Si kwamba aliamrisha tu.

Nataja hili kwa watu wanao mu excuse rais wa sasa kwamba hana responsibility. Kwamba this is just a police matter.

Jambo linapotajwa na BBC World Servive na Al-Jazeera linakuwa suala la kuhusu brand ya nchi tayari. Kama wapinzani wamefanya jinai, sawa. Lakini kama ni kesi za kubambikiana tu, rais hatakiwi kukaa kimya.

Rais hajakosa option hapa. Tuna precedent ya Kikwete alikataa serikali yake kukamatakamata watu bila sheria wala mantiki.
 
Haya ni maoni yangu.

Nawe una yako.

Uhuru wa kusema ni pamoja na kuchagua cha kusema, lini na mahali gani kisemwe.

Kama unaona saluni kunakufaa wewe peleka disinformation yako huko.

Nukta.
Pumbavu
 
Typical banana republic stuff!

No rule of law. No separation of powers.

No respect for the constitution.

The president is not supposed to exert undue influence on such matters.

Law enforcement officers are not supposed to bring trumped up charges against people for political reasons.

Hatujielewi kabisa sisi!!!
 
Actually, kama polisi wanapeleka nchi kuwa banana republic kwa kukamata wapinzani wasio makosa, halafu rais akawarudisha mstarini hivyo, rais atakuwa anazuia nchi isiende kuwa banana republic. Siyo anapeleka nchi kuwa banana republic.

Rais ana constitutional instruments na discretion ya ku consult, advise na get advise from DPP, AG, IGP. No?

Wewe unataka Rais aone nchi inaungua akae kimya tu kwa sababu ya kuogopa kuonekana anaingilia appointees wake? Wakati anaweza kurekebisha mambo?
 
Sikia dogo hayo hayaepukiki yalikuwepo na yatakuwepo tangu enzi za Yesu!! hkn jipya!! ndo maana ya Taasisi ya Urais!! sasa Rais samia kuwepo pale ndo maana yupo kiutendaji tumejipanga!!! lazima sisi Ngano km taasisi ya Rais, tuishi na Magugu ndani ya wana ccm hayakwepeki hayo!! hata wende kuzimu yapo!

Km Mungu tu anapingwa na Shetani aliye muumba!! sometimes hata Binadamu dongo tu km wewe unampinga na kusema kuwa Hayupo!! na km hayupo inamaana hakusaidii!! lkn bado anakulinda tu!!

sasa nakuuliza Rais Samia yeye nani? mpaka asiwe na hao watu? Yesu tu pamoja na ukuu wote ule lkn aliishi na Msaliti!! akatukanwa, akatemewa mate lkn akasema Forgive them!! some of thema alikula na!!

hata wewe hapo unaweza kupingwa na mkeo mnae lala nae kitanda kimoja na usifanye kitu!! lkn ukaendelea kuishi nae! ukamnunulia na nguo ukamuita Baby utakula nini? chipthiii! na km utahitaji asiye kupinga tu!! wewe hufai kuwa mwana ume!!

Mara ngapi watu wamepigwa na watoto zao wa kuwazaa kwani waliwaacha??? waliishi. na wengine kusamehewa!! hao wa hivyo wapo waache wajinafasi!!! huoni Nyerere alimtoroshea Ulaya Father Thom maksudi tu!!

Watoto wake bado wakala Bata Bongo mpaka Leo mfano ni ilee Hospital ya Maruku Hospital Mikoroshini ile ni ya mtoto wa Father Thom! Adui mkubwa wa Nyerere!! tena alitaka kumuua yule!! Utanunia wangapi?? utafukuza? wangapi? utaua wangapi?

Muacheni mama!!
 
Marais ndo huwa wanazifanya nchi ziwe banana republic kwa kukiuka katiba, kuingilia majukumu yasiyo yao, nk, kwa kutumia state organs kama polisi na majeshi!
 
Marais ndo huwa wanazifanya nchi ziwe banana republic kwa kukiuka katiba, kuingilia majukumu yasiyo yao, nk, kwa kutumia state organs kama polisi na majeshi!
Hata kama hilo linakuwa hivyo mostly.

Lakini rais akiona polisi wanakamatakamata wapinzani bila sababu, wakifikiri hivyo ndivyo rais anavyotaka, rais hana wajibu hata wa kusema tu hataki wapinzani wakamatwe bila makosa kwa polisi kufikiri hivyo ndivyo rais anavyotaka?

Kwa sababu sasa hivi watu wana mu excuse rais kwamba hawa ni polisi tu wanajipendekeza, rais hajaamuru wapinzani wakamatwe.

Sasa, if that is the case, kwq nini rais asiseme tu stop already, not in my name?
 
Yawezekana hao waliokamatwa wana makosa kweli…..

Na Rais alishasema watu wasiwe wanabimbikiwa kesi….jambo ambalo sisi wapenda haki tumekuwa yuko Lise a kwa muda mrefu!
 
Yawezekana hao waliokamatwa wana makosa kweli…..

Na Rais alishasema watu wasiwe wanabimbikiwa kesi….jambo ambalo sisi wapenda haki tumekuwa yuko Lise a kwa muda mrefu!
Kuna context ya logical argument ya kumu excuse rais inayohusiana na rais kuongea na appointees wake inayofuatiliwa hapa kwa watu waliokwisha concede kwamba polisi wamekosea, lakini wamekosea wenyewe bila kuamrishwa na rais.

Sasa mimi ndiyo nauliza. Kama ni hivyo, huyo rais hawezi kuongea na appointees wake wasiwafunge kimakosa hao wapinzani?

Hii logical thread ni tofauti kabisa na assumption yako kwamba wapinzani wamekamatwa kihalali, ambayo nishaisema kama ni hivyo, wapinzani wana jinai, kinachotokea sasa hivi ni sawa tu.
 
Kama polisi wamekosea si itaonekana mahakamani kwenye kesi….

Kwa nini Rais aingilie mchakato wakati mchakato una hatua zake zilizopo kisheria?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…