Napinga hoja ya kuwaombea wafu, maombi hayo hayafanyiwi kazi

Sasa walioua watu Oct 29,walitumwa na shetani kwamba wakiua na kumletea shetani damu, ndipo watatawala vyema,

Hiyo ni mmoja ya ibada ya wafu,

Sasa hii ikome mara moja
Shetani hayupo mkuu.

Ndiyo maana hujaweza kuthibitisha Shetani yupo.

Shetani na Mungu ni wahusika katika hadithi ya kutungwa na watu.

Ukisema wametumwa na Shetani unawaondolea uwajibikaji fulani.

Kama unajua Kiingereza soma ulichonukuu kimeelezea kirefu maana ya misa hizi.

Naona kama umenukuu bila ya kuelewa au hata kusoma.

Kama hujui Kiingereza hilo nalo ni tatizo linalofanya tusiweze kuelewana.
 
Sasa ulienda kuombea wafu na hukujua kwamba anayepokea ibada ya wafu ni shetani,

Huoni kwamba una shida mahala?
 
Sasa ulienda kuombea wafu na hukujua kwamba anayepokea ibada ya wafu ni shetani,

Huoni kwamba una shida mahala?

Mimi sijaenda kuombea wafu nimeenda kufariji mfiwa, huelewi wapi?

Shetani hayupo, Mungu hayupo.

Hizi ni hadithi za watu za imani na utamaduni tu.

Kama unabisha, thibitisha Mungu yupo na Shetani yupo hapa.

Hilo bandiko #77 ulilonukuu umelielewa?

Unajua kusoma Kiingereza?

Au hujaweza kusoma kabisa kwa sababu hujui kusoma Kiingereza?
 
Sasa hii ikome mara moja
Huna mamlaka yakumuamuru yeyote chini ya hili jua unless unajua ukifa mwili wako utazikwa na roho yako hujui iendako na kwa imani yangu nimefundishwa kuombea waliokufa na watakaokufa leo kwa hiyo hata wewe ukifa jua kuna watu wanaendelea kukuombea utake usitake.
 
Mbna tunaambiwa tumswalie mtume , kumbe tunakosea ?
 
Waliokufundisha Imani potofu ya kuombea wafu walikwambia NENO au kifungu kipi kwenye katiba kuu za Imani hiyo hasa Biblia?
 
Mbna tunaambiwa tumswalie mtume , kumbe tunakosea ?
Ni ibada ya wafu,

Hiyo alikufa akazikwa,

Ila Yesu ni hai, alifufuka, ni hai hivyo tunamwomba kiusahihi.
 
Ni ibada ya wafu,

Hiyo alikufa akazikwa,

Ila Yesu ni hai, alifufuka, ni hai hivyo tunamwomba kiusahihi.
Bandiko #77 hapo juu limeelezea hili suala kirefu.

Kwa anthropology, kwa sociology, kwa philosophy, kwa psychology, kwa science.

Hujajibu hoja hizi, hata moja.

Nafikiri tatizo lako ni elimu ndogo, hujui hata Kiingereza.

Unapambana bita ya kidini kwa hasira kutanguliza imani yako bila savoir faire.

Bila adabu ya kujua pahali gani, muda gani, naruhusiwa kusema hoja gani.

Unabwatuka kupinga kuombea wafu kwenye misa ya wenzio kanisani.

Unaonekana kichaa.

Hujui wapi unatakiwa kuweka mpambano wa kitheolojia, na wapi hutakiwi.
 
Yani uandike ujinga Kwa kiingereza na uamini kwamba utaeleweka?

Ujinga ni ni ujinga tu hata ukiandikwa Kwa kiingereza.

Zingatia hili, ibada ya wafu ni machukizo Kwa Mungu.
 

Kweli Nimesoma jumbe yako yote nimekulewa vizuri sana
Kimsingi umetoa ufafanuzi mzuri zaidi jamvini leo sikuwahi kujua vizuri uwezo wako kichwani kama leo upo vizuri sana nimependa
fafanuzi yako hongera sana ✍️

Lkn swali lipo pamoja na nimekuelewa vizuri jumbe
yako yote !!!

Lkn kujumuika Kwenye Misa yenye makandokando ya Kisiasa je lengo kuu
La jumbe yako litawezekana mana tayali Misa imekuwa kama yakisiasa
Kwenda kwako kunaweza kutengeneza kitu tofauti na kujenga udugu ujirani ❗

kwenda kwako kunaweza kukutoa Kwenye mshikamano na wengine
Sababu nimetaja misuguano ya kisiasa imegubika MISA yenyewe!!!
Mitaani Polisi wengi yote ni hiyo MISA

NI MISA yenye viashiria vya Kisiasa ndani yake
Kati ya Chadema Na CCM ❗

Ni Wazi misa ya Uchadema zaidi manake tayali kuna utengano tayali

sasa dhana ya kujenga undugu nawasiwasi
huwezi kuipata kwa MISA hii yasasa

lkn pia tukumbuke kuna Polisi 16 wameuwawa na Waandamanaji wale leo wanafanyiwa MISA

Kwaiyo utaona ni MISA yenye wasiwasi mwingi MISA sio rafiki na kujenga Ndugu mana vilio vyao vipo kimtazamo wa Siasa

Wazo lako na utetezi wako mzuri sana
lkn kama ingekuwa ni MISA ya kawaida jamaa kafiwa na mzazi rafiki nk wana kwaya wamepata ajali njiani!! sasa kuna MISA yao !!!

Hapo kujenga kungekuwepo %100
 
Yani uandike ujinga Kwa kiingereza na uamini kwamba utaeleweka?

Ujinga ni ni ujinga tu hata ukiandikwa Kwa kiingereza.

Zingatia hili, ibada ya wafu ni machukizo Kwa Mungu.
Wewe hujui Kiingereza, umejuaje hayo mambo yaliyoandikwa Kiingereza ni ujinga?

Pia, wewe ni mjinga kwa lugha yoyote.

Tena naona si mjinga tu, maana mjinga ukimuelewesha anaelewa, wewe ni mpumbavu.

Hata kwa Kiswahili nimekuelezea haya mambo, lakini hujayaelewa na hutaki kiyaelewa.

Dunia ni kubwa kuliko imani yako ya kijinga tu hiyo..
 
Hakipo ulichoelewa,

Niamini nakwambia😄
 
Mada jadiliwa imeletwa Kwa kiswahili.

Sasa kuchangia Kwa kiingereza ilhali wasomao ni waswahili huoni huo ni ujinga?

Mwl Nyerere aliwahi sema, nanukuu: Fikra sahihi huletwa Kwa lugha sahihi.

Sasa lugha sahihi ni kiswahili.
 
Hakipo ulichoelewa,

Niamini nakwambia😄
Nikwamini wewe
kwamba
sijamwelewa 🤠

Nimemwelewa lkn dhana yake yote kakosea kuiweka kwenye MISA yasasa yenye migogoro ya Kisiasa

Yeye naww tofauti yenu ndogo sana kiuwelewa

Nyinyi ni wamoja kabisa tofauti yenu ndogo
ni jinsi wewe kumwelewa yule kiranga

Kasema kwake yeye hakuna Mungu kabisa sembuse MISA yoyote
Lkn yupo kutafuta kutunza undugu ujirani
wajane
yumkin wabint mana kwenye mikusanyiko kuna fursa nyingi tu ikiwemo kwenye Misa!!

Fursa zipo kwa binadamu sio🤠

lkn Haamini chochote kwenye MISA na YESU mwenyewe!!!!

Naww mtazamo wako ni wanafanya MISA ya Shetani kuombea wafu

Kwaiyo nikama mnamitazamo ya aina moja
tofauti kidogo wewe japo kwako unaamini
uwepo wa MUNGU lkn
unapinga MISA ya wafu ✅

yeye huko hayupo kabisa kwenye MUNGU ‼️
 
Mada jadiliwa imeletwa Kwa kiswahili.

Sasa kuchangia Kwa kiingereza ilhali wasomao ni waswahili huoni huo ni ujinga?

Mwl Nyerere aliwahi sema, nanukuu: Fikra sahihi huletwa Kwa lugha sahihi.

Sasa lugha sahihi ni kiswahili.

Ktk hili nakuunga mkono kwa %100 jukwaa la kiswahili tusitoke kwenye Lugha yetu adhimu

tukitoka wengi watakosa kuelimika kwa kile tunakiweka jukwaani !

wewe endelea kumjibu kwa kiswahili utaeleweka zaidi ✍️
 
Kumbe ulichoelewa wewe ni kuwa,

Wauwaji wote wa raia wasio na hatia Oct 29 walaaniwe sindio?

Huo ni msimamo thabiti kabisa.
 
Mkuu,

Hakuna misa isiyo ya kisiasa, kwa sababu dini yenyewe ni siasa.

Yani mchungajibakiombea amani nchi tu, tayari hiyo ni siasa.

Mchungaji akikubali kutolipa kodi serikalini tu awe na special status kama kanisa tu, tayari hiyo ni siasa.

Mchungaji akishakubali kuhimiza waumini wajisajiki katika mpango fulaninwa maendeleonwa serikali tu, tayari hiyo ni siasa.

Ushaelewa hilo?

Ukizama sana kuangalia dini ni nini, dini ni siasa ya kale iliyovikwa joho la utakatifu wa Mungu asiyethibitishika.

Angalia falme zote kubwa, Egypt, Uajemi, Mesopotamia, Middle East, Ugiriki, Roma, China, zimetambaa na dini. Hakuna ufalme unaojengwa bila dini. Dini ndiyo inaweka siasa za kiutamaduni za nchi kuweza kutawalika.

Tunapenda kutenganisha dini na siasa kwa kiasi fulani, lakini dini haiwezi kutenganishwa na siasa kabisa. Ndiyo maana Samia Muislamu lakini kaenda mpaka Vatican, juzi hapa Mwigulu alikuwa amekaa na viongizi wa Anglikana Uingereza

Sasa basi, mimi sitapenda kuitumia dini vibaya katika siasa. Mfano, kupiga kampeni za kisiasa kwenye makanisa sitaolpenda. Hili ni jambo linaloweza kuleta mgawanhiko na vita vya kidini.

Lakini, kuna namna dini inaweza kutumika vizuri katika siasa. Mfano, kwenye kudai haki na uhuru, hata kwenye dini kuna mifano ya manabii waliowasema Wafalme kuhusu mabaya waliyoyafanya.

Afrika Kusini wakati wa utawala wa kibaguzi wa Makaburu, makanisa yalitumika sana kupinga siasa za ubaguzi wa rangi. Ma Askofu kama Desmond Tutu na Alan Boesak walipinga sana ubaguzi wa tangi.

Ndiyo maana watu wenye akili zao wa Kamati ya Nobel walimpa nishani ya Nobel ya Amani Askofu Desmond Tutu mwaka 1984. Alisimamia haki.

Mimi wala sioni suala la mauaji ya watu Tanzania ni suala la CHADEMA, sioni siasa hapa, kwa maana ya politics, naona siasa kwa maana ya governance, hili ni tatizo la uongozi wa nchi.

Nimewekea mkazo sababu za kifalsafa. Kwamba naamini katika haki ya watu kuishi, kama sehemu ya haki za binadamu. Sihitaji kuwa CHADEMA kuamini hili. Miminsi CHADEMA. Nimewakosoa sana CHADEMA hapa.

Sasa, haki ya watu kuishi ilivunjwa October 29 2025? Of course ilivunjwa. Napinga uvunjwaji huo.

Sihitaji kuwa CHADEMA kupinga hilo. In fact kuna watu wengi tu wa CCM wanapinga hilo. Waliouawa si CHADEMA peke yao, wameuawa Watanzania kibao. Na hata wangeuawa CHADEMA tu, bado nao ni Watanzania, naweza kupinga CHADEMA kuuawa bila ya mimi kuwa CHADEMA.

Kwa nini unaona jambo la watu kuuawa, watu wasio na hatia wamefuatwa mpaka majumbani mwao, watoto wanaangalia mpira wamefuatwa kwenye vibanda vya kuangalia mpira wameuawa, mifano kemkem mnaijua watu wameuawa hata hawako kwenye maandamano, hata si CHADEMA, kwa nini unaona hilo ni suala la siasa za CHADEMA?
 
Waliokufundisha Imani potofu ya kuombea wafu walikwambia NENO au kifungu kipi kwenye katiba kuu za Imani hiyo hasa Biblia?
Pasipo na shaka huu umekuwa utamaduni wa Kikatoliki na inategemea unatumia maandiko gani kusimamia unachokitetea ukisema tuache basi umeingilia maisha yetu ya kiroho maana toka enzi na enzi tumekuwa tukiwaombea. 2 Makabayo 12:43-46 na Mungu bado anatubariki wakatoliki kila leo tuna ibada kila asubuhi watu lazma waombee wapendwa wao waliotangulia kama hamuwezi basi mkachome na picha za ndugu zenu ili msiwakumbuke.
 
Ktk hili nakuunga mkono kwa %100 jukwaa la kiswahili tusitoke kwenye Lugha yetu adhimu

tukitoka wengi watakosa kuelimika kwa kile tunakiweka jukwaani !

wewe endelea kumjibu kwa kiswahili utaeleweka zaidi ✍️
Lakini kama pia hujui kiingereza,

Nenda ukasome Kwa faida yako.

Muhimu ni kulaani wauaji wa October 29 ili nao liwapate jambo.
 
Ulielewa alichomanisha Yesu kama Mungu ni wa walio hai basi na wewe haumo kwenye hiyo list yake ya YAKOBO,ISAKA NA IBRAHIMU
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…