Nashauri Rais awekwe mbali au apunguziwe access na mitandao ya kijamii

Kwangu ni ushauri wa hovyo, akiwekwa mbali Lile genge linalomzunguka litampa matango pori zaidi.Kwangu utendaji wa rais wa kila siku pia umma ushirikishwa kwa njia mbalimbali Kama vile opinion polls kwa Mambo mbalimbali ya serikali na taasisi zake.Uwazi ni muhimu
 
Hii ni sasa; hiyo ilikuwa...

Enzi hii mitandao haiepukiki, mtu yeyote, hata rais hawezi kukwepa teknologia.

Ndio sababu inaitwa "mitandao"; ipo kila sehemu na anayeidharau atadharaulika.

Ungeeleweka sana katika ushauri wako, kwamba Rais awe 'Savvy/smart', sio kila kitu kionekanacho mtandaoni kinafaa kuzolewa.

Na ili asielemewe, hana budi kuwa na timu imara kabisa ya wasaidizi wanaojua kutumia mitandao kwa manufaa zaidi. Hawa wasiwe watu wa mlengo mmoja tu, wawe ni watu wenye uelewa mpana. Kazi yake kubwa/muhimu ni kuwatambua na kuwapata watu wa namna hiyo. Wasiwe watu wenye mawazo ya aina moja.

Huwezi kumweka mtu kama YEHODAYA au JohntheBabtist anayeimba CHADEMA siku nzima kwenye kundi kama hilo.

Wao watachuja na kutupilia mbali takataka, na kumfikishia mwenyewe vito maridhawa vilivyomo kwenye mitandao.

Wewe ulikuwa na "a few cents"; hizi ni "my two cents."
 
Kama watoa maoni ni watanzania, na mitandao inafanikisha hutoaji wa maoni kwa ufanisi zaidi, na katiba inataka wananchi kutoa maoni kuhusu maisha yao, kwa nini mitandao isimfikie?
 
Yaani ccm waliowengi wanapambana kumbadilisha mama ili awe Kama mwenda zake, haiwezekani mnajisumbua bure, mama Samia ni rais wa watanzania wote ana haki ya kuinteract nao muda wowote.Rais kuwa karibu na wananchi ni muhimu
 
Maamuzi binafsi maana yake nini? Kabla ya kufanya maamuzi yeyote lazima uwe na information. Mitandao ya kijamii ina msaidia kupata information na feedback hivyo kumsaidia kufanya maamuzi sahihi.
 
Mzee umenuna yule empty head wa UVCCM kutumbuliwa?

Sent from my Nokia 8.1 using JamiiForums mobile app
 
Isingekuwa mitandao jana asingetengua ule uteuzi wa uvccm aliyewekwa tpdc.

Yaani mataga kasoma sunday school yohana university anataka akaongoze shirika la petroli ili wakaibe vitalu vya gesi na mafuta.
Embu tuliza papa muache mama afanye anavyotaka
 
Sehemu pekee iliyobaki kwa jamii kutoa dukuduku ni kwenye mitandao ya jamii
Mama asipopita humu anaweza asijue uelekeo wetu kama taifa
 
Well said, mfano mzuri ni akina Trump na Uhuru Kenyatta
 
Dunia imebadilika sn alafu yeye anataka tubaki kwenye analog nawakati watu wapo kwenye digital
 
Mtaalam unataka raisi wetu aishi Karne ya 16 ,Ila wananchi wake waishi Karne ya 21?
 
Nakubaliana na wewe maana hatuna hata bunge this time, hili ni bunge huru kabisa
Mkuu huu ubabe wa kunyimana taarifa kuna watu wananufaika nao,
ila uzuri digital age haibahatishi na internet never forgets
Mama akichanganya teule zake na opinion za humu anaweza kuja na combination ya viongozi wazuri walio neutral.
 
Suala ni kudhibiti taarifa nyeti zisiwafikie watu kama Kigogo2014.

Haiwezekani mtu huyo aruhusiwa kuwa na "sensitive" au "clasified information" bila shida.

Wakiweza dhibiti hio na ikaonekana, basi hatuna usalama wa taarifa nyeti za serikali.

Inakuwa kama tupo porini majangiri nao wajiulia tu wanyama watakavyo na kukimbia na nyaraka za serikali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…