Nashauri safari za mabasi kutembea saa 24 zisitishwe, vifo vitamaliza watu

Nashauri safari za mabasi kutembea saa 24 zisitishwe, vifo vitamaliza watu

Ajali haina kinga.

Unaweza ukafa hata ndotoni.

Unaota umefumania mke, unapata heart attack ndotoni unajifia zako kimyakimya😂
 
Lindi huko kuna basi imeondoka na watu 14 na haikuwa usiku,

Mimi bado naona tunakwamisha maendeleo kuzuia usafiri wa usiku wakati wenzetu wanakuwa na ajira mbili kwa wakati mmoja na wanafanya kazi hadi masaa 18.

MImi nimemaliza shughulinzangu dar saa 12 jioni unanizuia nisiende dodoma usiku naishia kulala na badala ambayo asubuhi ningekuwa dodoma nafanya issue nyingine naishia kuwa barabarani.

Nia sahihi ni kuboresha ufuatiliaji kama vile madereva wazembe na kuweka checkpoint n.k
Kabisaaa Kiongozi.. Hata Allys imepata ajali Saa Kumi na Moja Hiyo Siyo Usiku.. SAFARI za Usiku safiii sana
 
Lakini umesema inasemekana which means yr not sure!
Sikuwepo lakini aliyekuwepo sehemu ile ndio aliyepost comment yake akiitaja na ile basi iliyokuwa mbele ya Ally’s !!
Sehemu ilipotokea ajali ni tambarare na barabara imenyooka hakuna kona wala hakuna mlima !!
Unaweza kujiuliza ni vipi huyo dereva wa Ally’s hakukiona hicho kichwa cha Treni kinakuja kukatiza barabarani ??
Jibu la rahisi ni moja tu dereva alikuwa busy akiitazama ile basi iliyokuwa mbele yake ndio maana akasahau kuwa amefika kwenye railway’s crossing !!
 
Inasemekana mabasi mawili yalikuwa yanafukuzana mpaka hapo kwenye njia ya Treni yule aliyekuwa mbele kidogo aliwahi kupita huyu wa Ally’s akachelewa kidogo ndio akakutana na hiyo dhahama !!
Jiulize ipo haja gani ya kufukuzana ilihali wote wamejaza abiria ??!!
Daa aisee hebu fikiria wanashindana na abiria wamekaa kimya tu
Wengine huwa wanashangilia
Sasa hapo kwanini wanaita ajali?
Hiyo ni makusudi kabisa na dereva wote kama huyo yuko hai wangekuwa wanafungiliwa kesi za mauwaji na kula jela maisha
Kuna watu wana bet kwenye roho za watu
 
Kwa hiyo Ili kudhibiti vifo yapaswa kushughulikia uzembe na si safari za usiku, tupo pamoja bro.[emoji38]
Kama inawezekana kufuatiliwa nyendo zao madereva usiku inawezekana ajali zisitokee. !
Wasiwasi wangu ni kwamba imeshindikana kuwadhibiti madereva wasiendeshe mabasi zaidi ya 80 kph.
Hapo ndipo ilipo shida !!
 
Daa aisee hebu fikiria wanashindana na abiria wamekaa kimya tu
Wengine huwa wanashangilia
Sasa hapo kwanini wanaita ajali?
Hiyo ni makusudi kabisa na dereva wote kama huyo yuko hai wangekuwa wanafungiliwa kesi za mauwaji na kula jela maisha
Kuna watu wana bet kwenye roho za watu
Dereva amefariki on the spot!
 
Nchi zote za Africa Mashariki na Kusini mwa.Afrika mabus yanatembea usiku na mchana yameanza tu watu wanataka turudi kutembea mchana tu.Mabus kutembea masaa 24 yanafanya uchumi wa nchi ufunguke zaidi kwa mtu mmoja.mmoja na taifa kwa jumla.Kikubwa Madereva wazingatie sheria za usalama barabarani.Mabus yapo mengi panda lenye usalama na ukiona dereva ayupo vizuri toa tarifa kwenye vizuizi vya police.
 
TATIZO KUBWA ZAIDI Dereva kuendesha gari zaidi ya 1,000km peke yake.
Hii ni hatari kubwa.

Last week nimetoka mpanda na bus la AN CLASSIC, saa 12 kamili asubuhi hadi Dar saa 8 usiku, aliendesha Dereva mmoja, umbali wa km 1,188, hii ni hatari kubwa mnoo
Duh 🙌🙄 unatembea kaka angu
 
Gari lingekua lako ungefanya service ukifika dar na ukifika moro unafanya ungeweza. Mbona unaongea vitu vya ajabu sana.
Gari hizo zina ratba yake ya service sio kila siku. Unadhani service ni kuweka mafuta.
Unajua ifike mahali wana jf kama hujui uliza.. Gari hujawahi miliki unaanza leta stry za service every return day. Daah
Anajua service ni kama kuosha gari likipata tope
 
Kuruhusu basi zitembee masaa 24 kiukweli ni hatari sana hasa majira ya usiku.

Oya we wahuni wa mabasi usiku wanamwaga moto siyo poa wale jamaa niliwahi kuzishuhudia gari za mwanza Dar hasa zikiwa zinaenda mwanza majira ya usiku bus inapita kasi hata jina la ubavuni huwezi kulisoma, kweye kuovertake anaweza kukaa kulia na akazikata hata gari 10 bila tahadhari, alafu huwa hawarudi kushoto wanatembea na mstari wa kati
 
Mleta mada upo sahihi safari za usiku Zinaleta adhari nyingi kuliko mchana Hata hizo ajali za alfajiri au mchana ni sababu ya kusafiri usiku .

Dereva hapumziki vya kutosha usiku na unakuta kampuni nyingine wabahili kuweka madereva Wawili .
Mfano hai nilisafiri na Dar Lux mwanza - Dar kidogo tupate ajali dereva ametoka Dar Mpaka mwanza akageuza kurudi Dar akachoka akampatia gari rafiki yake asiyejua njia matokeo tukaparamia tuta wakati mvua inanyesha na huko njiani tulikosakosa malori mengi yapo full mzuka na mataa full Kama Treni .
Aiseee🙌
 
Back
Top Bottom