Natafuta Audio Clip ya zaidi ya Dk 5 ambayo Rais Samia anazungumza Kiingereza

Mtu keshakuwa rais, ni ishara kuwa tumechelewa. Haya masuala ya lugha kama ni muhimu sana tuyaainishe kwenye katiba. Na kuweka vigezo vya lugha kwenye fomu ya wagombea ikiwa ni sambamba na ulazima wa kushiriki midahalo kwa lugha husika!
Mpaka tufike huko, kwa sasa twende hivyo hivyo make hata lugha ya taifa haijulikani ni ipi.
 
Kwanza si kweli ,Putin anajua English,pili Russia hujifunza darasani jwa lugha yao sasa hawa wetu wamejifunza English tangu darasa la tatu hadi Phd ila hata kutamka neno enterpreneur hawezi

na sio enterpreneur ni entrepreneur[emoji3061]
 
Alifeli huyo ,Kasoma kwa kuunga unga.


Sasa ukweli nikwamba, hiyo nidalili tosha kua KICHWAN HAMNA KITU.
Wengi tu wamesoma kwa kuunga unga lakini kichwani wako vizuri sana. Watu wanakatisha masomo kwa sababu nyingi tuu. Hata stress nyingine zinachangia mtu kufeli ingawa uwezo anao. Tusimdhihaki mtu kwa kusoma kwa kuungaunga. Mtu huyo anastahili sifa ya kutokukubali kushindwa mpaka akatimiza malengo yake. Hivi karibuni tumeona wasomi wetu wenye Ph.D na uprofesa walivyo watupu. Makaratasi hayana maana tena.

Amandla...
 
Msikilize Nyerere kwenye mdahalo wa ana kwa ana. Interviews zake nyingi haziptikani sasa kwa sababu ya technoloy ya wakati huo.



Msikilize Mkapa ana kwa ana; huyu zipo nyingi sana kwa vile technology iliianza kukomaa wakati wa utawala wake


Msikilize Kikwete ana kwa ana hapa. Pamoja na technology wakati wa utawala wake. Siyo interviews nyingi zinazopatikana za papo kwa papo.


Msikilize Magufuli ana kwa ana. Huyu hakufanya interview kabisa wakati wa utawala wake.

 
Tufanye nini ili kusahihisha makosa yaliyofanyika kuwakosa watu wa aina ya Nyerere na Mkapa
 
Mbona hujamtaja Alhaji Mwinyi
 
Kweli hi Ni africa , mpaka mwaka 2022 na Karne hii bado tuna mawazo ya Nani muongeaji mzuri wa kiingereza.
 
Reactions: Tui
I’m always game. Nipigie tu simu tulonge hata masaa mawili au hata ukipenda siku nzima…
Nisingependa kuzungumza kwani sikijui lkn nataka kusikia cha kwako. Nadhani nitasikia Kiingereza cha Kisukuma, Kinyamwezi au Kikurya. Samia yeye anapiga RP hata kama ni cha kuandikiwa.
 
Reactions: Tui
Mada iliyojaa fikra kale za kitumwa na isiyo na adabu!🙏🙏
 
Hizo nchi ambazo wanatumia lugha zao kufundishia huwa kuna somo la english na lengo ni kuwafundisha kujua english, sasa iweje mtu asijue english wakati ni katika vitu alivyofundishwa shuleni?
 
Acha kuwa na fikra za kitumwa we mtu,sijui nani ameturoga sisi watu weusi
 
Tufanye nini ili kusahihisha makosa yaliyofanyika kuwakosa watu wa aina ya Nyerere na Mkapa
Ni hao tu wachache ndio wanaosifiwa sana humu hali ya kuwa tuna wazee kibao tu waliyosoma zamani na akina Nyerere na Mkapa, inafikirisha.
 
Kweli hi Ni africa , mpaka mwaka 2022 na Karne hii bado tuna mawazo ya Nani muongeaji mzuri wa kiingereza.
Ni kwamba elimu yetu tunafundishiwa kwa kutumia english na hivyo english imekuwa ni kipimo cha moja kwa moja cha kiwango cha elimu ya mtu kwa maana kama kawa huwezi kuzungumza vizuri kiingereza tafsiri yake hukuwa unaelewa masomo darasani.
 
Kwahiyo, unamanisha. Hawezi kuongea au unqaona kingereza Ni kigumu Sana?mbona Idd Amini alikuwa anaongea hivyo hivyo1?
 
Benjamin mkapa apewe heshima yake kwenye upande wa kuongea kiingereza kilichonyooka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…