Mkuu mie nakushauri anza na Fuso Tandam ndio utapiga pesa zaid. Ninakushauri hvo kwa kuwa hapa home tuna Scania tatu na Fuso mbili ila Fuso ndio zinapiga kazi kuliko Scania.
Na pia km ni Scania kwa wewe unaeanza sikushauri kwa kuwa ni sumbufu sana hasa ikishaanza kuchoka. Scania za kukutoa umaskini ni zile model za kizaman.
Na pia wanaokushauri kuhusu magari ya abiria naomba usiwasikilize kabisaa, maana yana changamoto nyingi sana. Mie binafsi nina Nissan Caravan mbili ila ni kichefu chefu kitupu.
NB: nimekushauri kutokana na uzoefu wangu wa kuishi na hayo magari kwa muda mrefu.
Kabla hujanunua nenda cheki na wazoefu wa logistics kama golden fleet ujiingize kwenye michongo yao nje ya hapo utalia kilio ambacho hujawahi kulia maisha yakoNimepata kama mil 100 baada ya kuvuna vanila huko Bukoba. Sasa nahitaji nijiingize kwenye biashara ya usafirishaji na wazo langu ni kununua scania kama kwenye picha
Nimepanga kuanza na moja kutokana na kiasi nilicho nacho
Naomba wenye uzoefu, kama biashara ikienda vizuri, kwa mwezi naweza ingiza kiasi gani?
View attachment 1484199
Ulianza vizuri sana, mwishoni umeongea madudu.Kama kilimo kimekupa pesa hizo nakushauri uendeleze tu kilimo ongeza hekta na pia nunua matrekta ya kulimia na kuvunia you dnont need kuivest kwenye biashara za watumia ndago. ... ila kwa Sound yako unaonehsa mtu wa Fix na Mipango mingi isiyotekelezeka... Alamsiki.
Kama kilimo kimekupa pesa hizo nakushauri uendeleze tu kilimo ongeza hekta na pia nunua matrekta ya kulimia na kuvunia you dnont need kuivest kwenye biashara za watumia ndago. ... ila kwa Sound yako unaonehsa mtu wa Fix na Mipango mingi isiyotekelezeka... Alamsiki.
Basi itakuwa biashara zote za usafirishaji zina changamoto Sana, me sikuwahi kuwa na gari kubwa la biashara Ila nimewahi miliki Bajaj na pikipiki kadhaa, aiseee aisikwambie mtu.....yaani ni pasua kichwa vby mno!
Kwanini kubeba mkaa? Nifumbue hapo
Mkuu tunaomba bei zake kuanzia kipisi mpka flatbedGari ambazo nina uzoefu nazo ni Howo na Shacman.
Ngoja nianze na Howo .
Howo ni miongoni mwa Gari za Kichina nzuri sana hasa kwenye utumiaji wa mafuta .Ukitaka kununu gari kama hii ni vema ukanunua Brand new .Maana bei ya mpya inashabiana na Bei za Scania used.Faida ya Howo mpya ni kuwa ina utumiaji mzuri wa mafuta hasi kulingana Horse Power (HP) yake ni 371. Katika biashara ya magari kitengo cha mafuta ni chagamoto so unapoata gari inayokula mafuta vizuri inapungiza gharama za uendeshaji. Pili Howo ikiwa mpya na ukapata dereva mzuri na mzoefu itakuchukua muda mrefu sana kupata hitilafu za mara kwa mara.Kwa kifupoi haina breakown za mara kwa mara na itakuchukua miaka Mitano mpaka 8 kuanza kusumbua.Kwa hiyo miaka kama utakuwa umeitumia vizuri utakuwa umeshrushisha hela yako na umeshanunua nyingine tena .
Upatikanaji wa spare ni rahisi kwa Tanzania ka sasa kuna mawakala wengi wa SINOTRUCK hapa Bongo so spare si tatizo.Pia spare zake bei affordable
Hasara za Howo.
Life span ya hizi gari ni fupi ukiliganisha na gari kama Scania .So ni vizuri kuitunza vizuri ili na yenyewe ikutunze pia.Service za mara kwa mara ni muhimu .
Ni muhimu ni kuwa mafundi wazuri na wanajua gari si bora fundi. Ikupendeza mara moja moja uwaite wenyewe wachina waicheki.
Gari za Shacam.
Ni gari ngumu na zenye nguvu sana, Nguvu kubwa inatoka kuwa na Horse Power kubwa kuna za 420HP na 440 HP .HP kubwa inasababisha ulaji mkubwa wa mafuta .
Fiada za Shacman ni pamoja na kuwa na nguvu kubwa gari kama hiii ni ngumu kukwama sehemu za rough Roads.Hii inaweza kupita sehemu ngumu kwa mfani mvua inanyesha huko migodini ni ngumu sana kukwama.
Inawe uwezo wa kubeba mzigo mikubwa kwa mfano inaweza kuungwa na trailer ya Lowbed na ikabeba mzigo heavy sana.
Hasara ya Shacman
Utumiaji mkubwa wa mafuta huchangia gharama za kiu edeshaji kuwa kubwa.
Life span yake pia si ndefu kama ilivuo gari nyingi za kichina.
Mwanza huduma sio mdogo yule, niliongelea hawa wanao chipukiaHahahaha kwamba akina luhuye, hunge, Texas, sigori, mwanza huduma na wenzao wanafanya ujinga kutembea tupu?
Wale gari zao ni kwa ajili ya mizigo yao na wameridhika na pesa wanayopata kwenye cement mkuu..
Ukiona gari imebeba cement ujue tajiri amekunja 11m, na unaeza kuta hata gari 4 zinapeleka sehem moja!
Hayo mambo ya madagaa dere ndo na yeye anajitafutia ugali
Sent from my SM-J105H using JamiiForums mobile app
Kampuni kubwa nyingi wanafanya hivyo, wanaokoa weseKuna kampuni kama sikosei ni Overland walikuwa wakitoka Zambia kama wanarudi tupu basi gari moja itabeba horse za gari 2, na nyingine itabeba tela za gari 2.
Hapo atakuwa amepunguza hesabu ya gari 4 kurudi tupu, na zitahesabika ni gari 2 zimerudi tupu.
Kampuni kubwa nyingi wanafanya hivyo, wanaokoa wese
Tunampoteza wapi? hakuna mtu amemwambia afanye hilo , lakn pia kwakua tunategemea biashara ikue si vibaya tukajua hawa wakubwa wao wanafanyajeJamani mnampoteza. Yeye sio kampuni hivyo mifano ya kampuni haitamsaidia.
Anachonitaji ni mbinu tunazotumia watu binafsi kwenye biashara ya malori katika kuajiri, kutengeneza gari, kutafuta mizigo na kusimamia biashara ya malori.
Natumaini umekosea kidogo au takwimu zako ni za miaka mingi nyuma.Mkuu sina uhakika na bei ila niongelee upande wangu huwa tunanunua Fuso ya kawaida yan single diff ambayo inakuwa bado nzma kabsa kuanzia milion 22 hadi 28, halafu tunaipeleka garage Moshi kwenda kuongeza chassis na kuwa Tandam.
Pia inarembwa na kufanyiwa kila kitu hadi ikitoka hapo inakuwa km mpya. Cost zote inaweza kusimamia milion 42 hadi 50 na gari inakuwa imesimama balaa
NB: hyo cost ya milion 42 had 50 ni kuanzia gharama ya kununua gari hadi kufanyia kila ktu.
Kipisi cha million 25????? Itakua napitwa na mengi, naomba uniunganishe na muuzaji wa hivyo vipisi vya bei hiyo kiongozi vinahitajika vitatu chap viwe 113, 93 au 94 poa tuHapana Tandam ipo juu ya kipisi, kwa maana kipisi kilichosimamia kucha unachukua kuanzia milion 25 hadi 32.
Hali kadhalika Tandam kuna wengne wananunua hadi million 70, 80, had 90.
Hiii Si MchezoooJifunze kuwa na moyo wa chuma kwanza, ukiskia ata mtoto wako ameugua unasema sawa uku ukiendelea kunywa kahawa.
Apo utafanikiwa kwenye vyuma vya moto
Uzi unamadini huu.basi tu lakini nyuzi kama hizi ni za kuzitunza hazina kabisa.uzi safi
Hujakosea mkuu, ila tu gari ambayo wewe unainunua kwa milion 30 mie naweza kuipata kwa milion 20.Natumaini umekosea kidogo au takwimu zako ni za miaka mingi nyuma.
Kiuhalisia na kikawaida huwezi kuipeleka fuso ya mil 25 eti ukaiwekee tandem kwani hiyo ni bei ya fuso iliyochoka. Inatakiwa na inashauriwa ununue fuso yako kinanda yaani saaafi kabisa agiza hata ya mil 60 sasa ndo uipeleke gereji ikafanyiwe mambo, ikitoka hapo tayari thamani yake inakua kwenye million 80-100 hivi. Huu ndo uhalisia wa SASA mwaka 2020