Natakiwa kumfukuza kazi muajiriwa aliekuwa kwenye kampuni kwa miaka 17, Nifanyeje?

Natakiwa kumfukuza kazi muajiriwa aliekuwa kwenye kampuni kwa miaka 17, Nifanyeje?

Unyama wa private sector. Kufukuzana ni sekunde… unadamka kuwahi kazini, kumbe Boss na menejiment yake wamepanga kukupa End of contract 🥹
mkuu on another angle inaweza kuwa baraka pia..huyo mtu amekaa 17yrs inawezekana ana ujuzi na maarifa ya kujitegemea na kufungua busness/investment zake ambazo zitakuwa kubwa na kusaidia wengi..but labda hana confidence ya kutoka kwenye comfort zone au anasitasita kufanya maamuzi..then Mungu anaamua kumsaidia aondoke hata kwa kufukuzwa ili aweze kufanya hayo makubwa!..haya mambo yapo na waliofanikiwa wengi wana hizi backgrounds!
 
Habari wana JF, Mimi ni HR wa kampuni fulani kwa miaka 2 sasa. Nimepewa order na maboss zangu kumfukuza mfanyakazi ambae amefanya kazi kwenye kampuni hii kwa miaka 17. Amefanya kosa ambalo ni la kusamehewa tu ukiangalia na muda aliojitoa kwenye kampuni hii.

Bado hajui chochote na kwangu imekua ngumu kumwambia, NIFANYEJE wadau?
Kumfukuza mtu kazi hapana jamani...

Hakuna Warning letter apewe? Displinary Committee je?
 
KWa wewe hapo uko kwenye wakat mgum sana ku intervene utalazimika tuu kutekeleza.

Kuna mshkaji wangu yeye alikuaga System admin taasis fulani hivii na siku moja akainyaka juu juu email ya maboss/wakurugenzi kuhusu kumuondoa kazini mfanyakaz mmoja mtu mzima kwa hila tuu.Na mpango ulikua mdau huyo lazima achomolewe na ikiwezekana atenezewe zengwe(hii ilikuja fahamika baadae sana).

Mshkaji wangu alichofanya akai print ile email kesho akamtafuta yule mdau private kitaani akampa A TO Z na akamshauri afanye juu chini kujiondoa kabla hajafukuzwa ili asiharibiwe reputation yake kupata kaz mahala pengine na asikose stahiki zake..

Mpaka kesho mdau anamshukuru jamaa angu
 
Habari wana JF, Mimi ni HR wa kampuni fulani kwa miaka 2 sasa. Nimepewa order na maboss zangu kumfukuza mfanyakazi ambae amefanya kazi kwenye kampuni hii kwa miaka 17. Amefanya kosa ambalo ni la kusamehewa tu ukiangalia na muda aliojitoa kwenye kampuni hii.

Bado hajui chochote na kwangu imekua ngumu kumwambia, NIFANYEJE wadau?
Soma mkataba vizuri, itawagharimu huko mbeleni! Mkimfukuza kindezi atakimbilia CMA na huko kama hamtamlipa pesa yake vizuri atawabwaga! Rudia kusoma mkataba vizuri pamoja na sheria ya mahusiano kazini ya mwaka 2004!
 
Asishangae na yeye baada ya miezi 6 mbele anakunjiwa sura anaambiwa akae pembeni aingie mtu mwingine kwenye nafasi yake
Hahaa sekta binafsi ya kidwanzi sana chapchap wanakupiga chini

Wakubwa wanakutafutia makosa halafu wanakusanua hawaridhishwi na utendaji wako wa kazi
 
Subiri kurogwa tu... Maana inaonekana mwamba ana kitu ndio maana kafika mbali 17 years sio mchezo ktk kampuni... Utarogwa hadi kizaz chake kijacho... WORRY OUT FANYA KAZI NAKUTISHA
 
Back
Top Bottom