Nauli hizi za SGR nani atapanda? Kutoka Dar - Moro Tsh 24,000?

Mie nadhani hiyo feasibility study km ilifanyika vizuri lazima ingekuwa imejibu haya maswali.
Study iliyofanywa na world Bank ili recommend against this project.
Tumefika hapa na huu ndio uhalisia.
Tukipunguza hii nauli kwa subsidy kuna wananchi wa Nanjilinji watalipia hizi huduma unnecessarily.
 
Wana CCM TUNAPANDA
 
Tanzania hatukujenga reli ije kuwa Huduma bali ilete faida..

Ukisema iwe Huduma huo Ni upumbavu wa kuchagua vipaombele kwa mda ambao sio sahihi..

Ukisema Bei iwe chini au sawa na Basi ndio kusema tuchukue Kodi kuja kuwalipia nyie msafiri bure ,huu utakuwa Ni upuuzi wa Hali ya Juu na matumizi mabaya kabisa ya Kodi yetu..

Barabara zipi zinazoharibika kwa mizigo hapa Tanzania? Kuna uzembe tuu wa kuwa na njia nyingi za Barabara matokeo yake mrundikano njia chache..

Mwisho aliyeamua kujenga sgr kwa Pesa za Umma Ni mpumbavu wa kiwango Cha mwisho,Leo hii hayo Matilioni yengewekezwa kwenye Barabara zingenyenyua Uchumi wa Nchi haraka Sana kuliko huu ujinga wa sgr..

Na wajinga wengi ikiwemo wewe akili yako inawaza prestige kuliko economic significance.
 
Hakuna Cha feasibility study iliyofanyika zaidi ya prestige ya Jiwe kwa taarifa yako..

Niliwaambia hapa watabadili gia waanze kusema sgr Ni Huduma..

Sasa unajiuliza Kama Ni Huduma he watu walikuwa na hamu Sana ya kufika Dar haraka? Yaani tuanze ku allocate Pesa Tena kuendeshea limradi linaloleta hasara..
 
Yale makopo yana uwezo wa kutumia 60mins?
Hayawezi kabisa mkuu, hata akisema atembee top speed non-stop. Kumbuka kuna vituo lukuki njiani. Labda 2 hrs ukijumlisha na muda wa kusimama vituoni
 
Okay am glad hilo tumelimaliza haya mambo ni Huduma.., Sasa Je ? Hivi unajua Private Sectors / Business ni answerable kwa shareholders wao wala hawafanyi kazi ya kanisa ? Hawapo pale kutoa huduma bali kutengeneza as much money as possible (kwahio usitegemee msaada kutoka kwao) na sekta ambazo competition ni ngumu kufanyika hata privatization ikifanyika more times than not bei hazishuki na bado mwananchi atatoa kodi / pesa iwapo private sector haitapata faida ili kufidia the difference...

Haya unasema ziendeshwe vipi kibiashara au kijamaa ? Kuendesha kijamaa ni vipi unaweza kunipa mfano ? Kama unamaanisha ni kwa Serikali kutoa ruzuku basi dunia nzima inaendeshwa kijamaa linapokuja suala la hizi sekta za huduma..., Na sio hivyo tu hata Benki ambazo ni Too Big to Fail nazo ni Ujamaa sababu wakipata faida shareholders wanakula chao hasara ikipatikana wananchi ndio wanalipia ili uchumi usishuke (refer Global Financial Crisis huko Marekani)

Alafu kabla hatujafika mbali naomba nikwambia am all for competition and free market..., hivi unajua bila Serikali kuwapangia daladala bei kwamba isizidi kiasi fulani ingeshazidi ? Sasa mimi in my way of thinking Serikali haipaswi kuingilia biashara za watu na investment zao, hususan likija suala la bei (sababu they know their investment better) ila katika hio free market sababu na sisi UMMA tuna akili na tunalipia hizi huduma kutoka kwenye kodi zetu kwanini hio mwendokasi isiendeshwe kwa ufanisi na kutoa bei ambazo hao latra ndio wanaona zinaendena na uhalisia na kuwaacha watu na biashara zao wapange bei kulingana na soko wanavyoona ?

Vilevile hata hizo kampuni binafsi za usafiri huko nje unaweza kusema pia zinaendeshwa kwa watu kutumia kodi zao ili mwekezaji alipwe fidia / ruzuku pale ambapo anaona route haina faida - kwahio kuliko kuendesha / kushindana na kupata kinachopatikana na kutumia pesa zetu kulipa watu (private) ili wapate faida hapa equation inabadilika (operations costs + profits for shareholders + Subsidy from Government)=Mtumiaji kugharamikia badala yake ingekuwa (operation costs)=Mtumiaji kugharamikia + government subsidy
Ndogo kwako ni ipi mkuu; mimi nimekupa ndogo kwangu lazima iendane na gharama za uzalishaji na uwezo wa mtu wa kawaida kulipia na kipindi ambacho mtu wa kawaida anashindwa kuna ruzuku inatoka (sababu hio ruzuku ni kama kumpa mwanao mtaji ili azalishe zaidi; kwa wafanyakazi kuwahi makazini au kupata umeme wa uhakika au kuoga na kuacha kunuka kikwapa ni faida kwa nchi...)
Sasa mkuu kama tunazungumzia kinachoendelea na sio jinsi ya kuweza kuboresha hatuna tofauti na wale mababu zetu waliosema wanadiscuss people au events na sio ideas...; Hakuna mtu ambae haoni kinachoendelea kwamba ndivyo sivyo.., ila hio kazi ya ku-report tunawaachia kina Pascal Mayalla wafanye kazi yao wengine sisi hapa tunaongelea mawazo / fikra zetu no matter kama zitafanyika au kutofanyika katika kizazi chetu
Mfano wako wala haufanani...

Nakuambia unaishi kwenye fantansy world kwa sababu uhalisia unauona lakini unajifanya huuoni!!
Kilichopo kama ningeona kipo sawa wala nisingepoteza muda hapa huenda ningekuwa naongelea game la leo usiku au nina-cross check kama ideas za sasa can be made better..., hivyo ndivyo nilivyo na sababu naona ndio maana kila siku natupia comment chache kuhusu walamba asali ndio maana nikaleta uzi wa kufanya Tanesco iwe a better company
(not that it will..., but I think its possible am just putting my views on paper to be criticized and refined) au Jinsi serikali inavyoboronga na kufanya bundles ziwe bei kubwa kutokana na kuingilia kampuni za simu Sakata la Bundles - Suluhisho

Unaona hapo nauli to Morogoro 24K... twice as much-- na huo ndo uhalisia wenyewe na sio "how should be"

Na hata wakisema washushe, maybe to 10K... je, itakuwa imekidhi tafsiri yako ya huduma?!
Tafsiri sio yangu tafsiri itatokana na gharama ya uendeshaji na uwezo wa mlipaji..., vilevile sababu ni hasara kwa hili dude kutokubeba watu wengi na watu wanavyokuwa wengi zaidi ndio huduma gharama ya uendeshaji ina-make sense tofauti na basi (hivyo the only alternative which makes economical sense) ni kuweka bei ambayo itajaza watu kulingana na capacity iliyopo yaani waweke mabehewa mengi as practical possible kulingana na watu waliopo kwa bei wanayoweza without breaking their banks
 
Hiyo ni bei ya nauli walizopendekeza wao trc then latra watakusanya maoni ya wadau ili wacrosscheck pande zote kupata bei sahihi ya mlaji. Kama mlaji napendekeza nauli ya dar moro iwe 6000
Yaleyale ya mwendo kasi serikali hapo inapendekeza viwango vidogo then trc watapokea kishingo upande basi taratibu huduma zitaanza kuzorota mwishowe mambo yanakuwa ovyooo kabisa maana trc watazingizia gharama ni kubwa na nauli ni ndogo mno..
 
Katika sehemu tuliingizwa mkenge na kiongozi wa nchi ni huu mradi. Tutapata maumivu mpk huko kiama kwa huu mradi.
 
Tanzania hatukujenga reli ije kuwa Huduma bali ilete faida..
faida kwa nani na vipi ? na faida ipi ? Monetary yaani Shirika lipate mapato zaidi au faida ya watu kuweza kufika point B kwa gharama nafuu ?
Ukisema iwe Huduma huo Ni upumbavu wa kuchagua vipaombele kwa mda ambao sio sahihi..
Huu ni muda wa kufanya nini na huduma zipi mwananchi anayezipata kwa sasa ? Na hii huduma ya usafiri wakati wake sahihi ni upi ? na kama ni kosa limefanyika / lilifanyika suluhisho ni kuweka bei ambayo sio rafiki kwa mwananchi wa kawaida hence kukosa yote yaani (monetary na socially)?
Ukisema Bei iwe chini au sawa na Basi ndio kusema tuchukue Kodi kuja kuwalipia nyie msafiri bure ,huu utakuwa Ni upuuzi wa Hali ya Juu na matumizi mabaya kabisa ya Kodi yetu..
Wateja wakiwa wengi sana kati ya basi na train ipi ina gharama kubwa ya uendeshaji ?
Barabara zipi zinazoharibika kwa mizigo hapa Tanzania? Kuna uzembe tuu wa kuwa na njia nyingi za Barabara matokeo yake mrundikano njia chache..
unamaanisha ya kuwa na njia nyingi au chache ? Kama nyingi tuongeze njia zaidi ? Hizo njia hazina gharama ya kuzitengeneza na kuzifanyia repair ? Na usafirishaji wa mizigo mizito kipi ni cost effective train au magari / malori ?
This is another argument ambayo sioni faida ya kuongelea hapa huenda miaka kumi ijayo tukawa tunasema aliyeingia mikataba na hao wachina na sijui kina nani alikuwa mjinga wa kutupwa..., that's a blame game ambayo kwa leo nadhani nina more constructive issues za kufanya..., Na kama tungetaka kama nchi kuondoa uwezo wa mtu mmoja kuamua aliyepo sasa asingekubali kuendelea na Sheria inayomruhusu kufanya anachotaka
 
Kwani bei za United Kingdom za British Rail against mabus Express zikoje? Hizi ndiyo matokeo ya kushabikia vitu bila ku analyse na sasa bado SG Hydro Electric power station
 
Siku zote nasemaga fisiemu ni mzigo mzito sana kwa watanzania
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…