Nauli hizi za SGR nani atapanda? Kutoka Dar - Moro Tsh 24,000?

Nauli hizi za SGR nani atapanda? Kutoka Dar - Moro Tsh 24,000?

View attachment 2440365
Hata kama ni mapendekezo sidhani kama mlifikiria au kuwaza kwa kinagaubaga, huko Anatorglo mnaenda kupaka mafuta ili kung'arisha hiyo nauli na si vinginevyo.

Ukute mmeshaandaa wazungumzaji wenu wa kutetea hiyo nauli na hapo ndiyo watakuwa wengi ukumbini.
Mhuu mradi utakufa kabla ya kuanza. Hapo Abood lazima achekelee sana. Mtu alipe 2.5x ya nauli basi kwa kisa gani? Upuuzi mtupu
 
Hakuna sehem usafiri wa treni ni nafuu. Kifo cha mwendokasi ni matokeo ya nauli ndogo hivyo kushindwa kuleta magari mengi na huduma kuwa mbovu.
Hata wanaofanya biashara za daladala nauli ni ndogo ndio maana uwekezaji hafifu.
Tuanze kuishi kwenye uhalisia.
 
Ukiona hivyo huo usafiri siyo wa mwananchi wa hali ya chini. Umemlenga mwananchi wa hali ya juu
Kwahiyo huo sio usafiri wa Wamachinga ndio waliokuwa wakipiga Vigelegele Nderemo Vifijo na Hoihoi kwenye hotuba za Mwendazake.
 
Running cost ya hii kitu ni kiasi gani ?

Navyojua mimi economy of scale kama inajaza watu wengi kuliko mabasi, na inatajaa sio kutembea tupu basi bei inaweza kushuka maradufu kuliko basi na bado pesa ya uendeshaji na chenji ikapatikana...

Wasisahau hii ni huduma na sio mradi wa kujitajilisha..., ni yuleyule mlipa tozo ndio anakamuliwa na huku
 
Hii sio rahisi kama unavyodhani. Duniani kote mabasi ni nafuu kuliko treni
 
Ni halali hiyo nauli kama kwa dk 60 upo moro
Kwamba sababu ya mwendo gharama imeongezeka au uhalali unauelezea vipi ? Operation Cost ya hii kitu ni kiasi gani ?

Na wakiingia watu watano ukapeleka dude tupu si ni hasara kuliko kuongeza behewa nyingine hata tisa na kupeleka watu lukuki...

Ofcourse wanaweza kuongeza behewa la presidential na wakachaji hata milioni kumi kama kuna wateja kama wewe mtapatikana
 
Hii sio rahisi kama unavyodhani. Duniani kote mabasi ni nafuu kuliko treni
Acha Story mkuu mabasi yanakuwa nafuu kulingana na watu / idadi ya wanaosafiri..., sababu kama volume ni kubwa unaweza kuhitaji mabasi hata kumi wakati huku una train moja... ?

Ila kama wateja ni wawili ofcourse basi ni nafuu hapo naongelea running costs (ila unafuu wa mlipaji sijui unaongelea nini) sababu safari za Tube duniani kote sijaona zinafanywa na mabasi (virtually impossible) ukiongezea na traffic congestion...
 
Acha Story mkuu mabasi yanakuwa nafuu kulingana na watu / idadi ya wanaosafiri..., sababu kama volume ni kubwa unaweza kuhitaji mabasi hata kumi wakati huku una train moja... ?

Ila kama wateja ni wawili ofcourse basi ni nafuu hapo naongelea running costs (ila unafuu wa mlipaji ijui unaongelea nini) sababu safari za Tube duniani kote sijaona zinafanywa na mabasi (virtually impossible) ukiongezea na traffic congestion...
Usiangalie running costs tu. What about investment cost? Analipa nani huo mkopo?
Hilo behewa ni kiasi gani? Reli imejengwa kw gharama gani. Tafuta mji wowote mfano London kwenda Manchester kwa basi na treni, then tuongee. Taarifa zipo kwenye mtandao
 
Back
Top Bottom