Nauli hizi za SGR nani atapanda? Kutoka Dar - Moro Tsh 24,000?

Nauli hizi za SGR nani atapanda? Kutoka Dar - Moro Tsh 24,000?

View attachment 2440365
Hata kama ni mapendekezo sidhani kama mlifikiria au kuwaza kwa kinagaubaga, huko Anatorglo mnaenda kupaka mafuta ili kung'arisha hiyo nauli na si vinginevyo.

Ukute mmeshaandaa wazungumzaji wenu wa kutetea hiyo nauli na hapo ndiyo watakuwa wengi ukumbini.
Lengo lao ni kuihujumu tu hiyo treni bila shaka. Maana nauli ikiwa chini, mabasi yao yatakosa abiria.
 
Kama ni saa

Yaan ushakalili kwamba Bei ya tren ni ndogo kuliko basi..haiko hivyo inadepend na huduma unayopewa.leo hii Azam marine wanachaji 25000 had 30000 Kwa usafir Zanzibar.. Kwa mwendo wa saa moja na nusu. NeNda mwanza hadi ukerewe masaa matatu hadi manne, nauli haizid 8000/ Kwa Meli.
Watanzania ni watu wa kulalamika
 
Hakuna sehem usafiri wa treni ni nafuu. Kifo cha mwendokasi ni matokeo ya nauli ndogo hivyo kushindwa kuleta magari mengi na huduma kuwa mbovu.
Hata wanaofanya biashara za daladala nauli ni ndogo ndio maana uwekezaji hafifu.
Tuanze kuishi kwenye uhalisia.
Mwendo kasi imekufa lini? Unajua inaingiza kiasi gani kwa siku?
 
Kwamba sababu ya mwendo gharama imeongezeka au uhalali unauelezea vipi ? Operation Cost ya hii kitu ni kiasi gani ?

Na wakiingia watu watano ukapeleka dude tupu si ni hasara kuliko kuongeza behewa nyingine hata tisa na kupeleka watu lukuki...

Ofcourse wanaweza kuongeza behewa la presidential na wakachaji hata milioni kumi kama kuna wateja kama wewe mtapatikana
Ujue ATC inajaza pamoja na bei zao kuwa kubwa?
 
Usiangalie running costs tu. What about investment cost? Analipa nani huo mkopo?
Hilo behewa ni kiasi gani? Reli imejengwa kw gharama gani.
Aisee duh... , hii ni hatari bin balaa kwahio unadhani huo mkopo hata wasipopata hata sumni wewe, mimi na wananchi wote hatutalipa ?

Unajua kitu economy of scale ? ukisema uweke laki laki, watu wakapanda wanne kwa wiki huo mkopo ndio utalipa ? au useme elfu 30 na train kujaa kila wakati ipi ina afadhali ?

Pili Unajua kwanini Train nyingi hata UK zimeshindwa kubinafsishwa kwa faida ? Sababu hii ni huduma kuna sehemu sio profitable kwenda ila kuna watu wanaishi na inabidi wafikiwe hivyo inapelekea hata serikali kutoa ruzuku (kwa private companies ili wanende huko) au kuamua ku-renationalize baada ya privatization (impact ya usafiri kama vile ilivyo umeme na maji ni kubwa) hivyo profit kwa jamii sio monetary pekee
Tafuta mji wowote mfano London kwenda Manchester kwa basi na treni, then tuongee. Taarifa zipo kwenye mtandao
Duh aisee hii ni hatari sana..., hivi unajua kuna kipindi ulikuwa unaweza kutoka Birmingham UK mpaka London kwa Pound moja ? (Hio ni system kama aliyokuwa anafanya Fast Jet / Budget Airlines) kuliko kwenda bodi tupu ni bora ukachukua watu kwa bei ndogo (ingawa mule ndani pia kuna watu wanatoa pesa zaidi)...

Pia ndio maana nikasema hivi unajua Tube System inayobeba commuters kila siku kwenda makazini n.k. isingeweza kufanywa na mabasi (virtually impossible) na huko tunakokwenda sio ajabu mji kama Dar mtu anakaa Morogoro anafanya kazi Dar kwahio huu usafiri kwake ukawa hata mara mbili kwa siku kwenda na kurudi...
 
Back
Top Bottom