DOKEZO NBS toeni tamko: Ulipaji wa pesa za semina za Sensa kuna uhuni unafanyika

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Maana kama kamati za sensa za mikoa na wilaya hajiwai lamba posho vipi hawa wengine?

Nimejaribu kuwaza 1.3M zidisha kwa makarani 250,000 nchi nzima. Mwigulu ana hiyo hela kweli?
Anaikosaje wakati nchi hii tajiri sana! Magu alikuwa sahihi, nchi ina pesa hii, tatizo letu ni vipaumbele tu. Wanasiasa wanakula mkwanja wa kujipimia tu yani! Keki [emoji513] ya taifa inaliwa na wachache!
 
Zoezi la postcode liliharibika hivi hivi. Hadi leo mahali napoishi namba za vibao zimeandikwa kwa mkaa ukutani. Waliofanyakazi ya posti kodi wanadai zaidi ya laki moja posho yao ilifia huko huko halmashauri X
Hakuna zoezi la kitaifa limewahi kwenda vizuri kama lilivyopangwa. Tuna ulafi na tamaa ya pesa ajabu. Bajeti iliyopangwa haifiki chini kwa mlengwa kama ilivyo. Kila inapopita inapigwa panga! Mwisho wake zoezi linaishia njiani!
 
Mnadai malipo wakati hata hamjatuhesabu jamani.
 
Shida ipo Kwa wanazoezi pia.Nyuzi zingine MTU anakurupuka kalipwa laki 950 bado anadai 650.Kauli ilipaswa iwe moja,kama hakuna walikolipwa nchi ijue,sio MTU unajikurupusha kujidanganya umelipwa huku unajua unajidanganya mwenyewe.
 
zoezi limeingiliwa na rushwa, dhuluma na uonevu mkubwa kuanzia kwenye usaili hadi semina yenyewe. Mungu waondolee kiburi watu kama hawa. Serikali iko vizuri tatizo watendaji wake ni hovyo kabisa, wabinafsi sana.
 
Billion 350+ ni pesa ndogo kuelekezwa kwenye malipo tu achilia mbali vifaa na logistics zingine? Kwa Nchi maskini kuelekeza mapesa yote hayo kwa kazi ya mwezi unaita hela ndogo? Hahahaha you cant be serious!!
Nahapa hajawahesabu wale wakubwa kuanzia mwenyekt wa sensa taifa na kamisaa kushuka had kwawawezeshaj wa sensa
 
Huku nyasa leo awamu ya pili imelipwa, jumla had sasa lak 4
 
Ukweli nchi hii bado haijapata Viongozi ila ina kusanyiko la wajinga waliojipa jukumu la kuongoza wenye akili.
Katika hali ya kawaida tu, unawezaji kuwaweka watu bila posho yao kwa siku tena ukijua wengi wao ni wale wasiokuwa na ajira halafu unategemea matokea chanya... Mfumo wetu wa kupata Viongozi ni wa dhambi sana kiasi kwamba tunapata Viongozi wasiokuwa na huruma na wengi wakiwa wezi wakubwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…