Pre GE2025 Nchi imerudi mfumo wa Chama kimoja, Magufuli kaacha utamaduni mbaya kwenye siasa, itachukua miaka 20 kumpata kiongozi kama Kikwete

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Tatizo lenu kubwa mmeshikwa akili Magufuli alikuwa mbaya. Mnasahau Magufuli alifanya vitu vyote kwa maslahi ya CCM, nyie ndio mlikuwa mnasema mama anaupiga mwingine.
Kama hamtajitazama na kuangalia wapi mnakosea mtaendelea kupambana na marehemu.
CCM gani? Ilikuwa maslahi yake binafsi na kundi lake. CCM inatumika kama tool!
 
Kwakuwa watu wa taifa la gizani akili zao zimekuwa giza acha waendelee kuwa gizani kwani ndicho walichochagua.
 
Hoja yako ni nzito Sana ilipaswa iwe mada kabisa
 
Hoja yako ni nzito Inafaa kufanyiwa lamination
 
Kwahiyo sisi kazi yetu ni kulaumu tu wale waliokwisha kwenda mbele za Haki kwa kile walichokikosea ??!!
😳🙄😀😅😂 !
 
Shida inaanzia kwa upinzani wenyewe hili wakilijua itawasaidia sana kama wataendelea kukaza fuvu ikulu wataisikia kwenye radio na bahati mbaya sana hawana wafuasi wakuhoji nyendo zao kwa maana yakujenga
 
Wapinzani wenyewe katiba yao hawaifuati sijui tofauti yao na CCM iko wapi
 
Umeongea hoja kubwa sana shida kubwa wengi wao ni mashabiki wa vyama zaidi ya nchi
 
Shida inaanzia kwa upinzani wenyewe hili wakilijua itawasaidia sana kama wataendelea kukaza fuvu ikulu wataisikia kwenye radio na bahati mbaya sana hawana wafuasi wakuhoji nyendo zao kwa maana yakujenga
Viongozi wa upinzani wengi ni wababaishaji tu. Hamna watu pale.

Hakuna mtu aliyeserious atapoteza muda wake kuandamana na wanaharakati. Hizo nyakati zimeshapita.

Watu wanataka kusikia ubora wa sera na utekelezaji wake.

Hata dola sidhani kama itahangaika na wewe kama upo kwa ajili ya kuuza sera zako na sio kuibua hofu na kusambaza uongo.

Kwa bahati mbaya wapinzani hawana wanasiasa bali wana wajasiriamali tu katika siasa.

Kama wanataka kulisaidia hili Taifa wabadilike.
 
Ni muda mfupi tu mifumo hiyo itasambaratika. Usifikiri itachukuwa miaka yote hiyo. Mungu amesikia kilio cha watu wake na atajibu. Sasa ole wao wote wanaofanya uonevu maana mambo yatawageuka!
 
Tatizo ni mfumo. Na sasa mifumo hiyo itasambaratishwa na Mungu. Lakini swali ni hili je mko tayari?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…