Sahihi kabisa ndio kitu ambacho nimemwambia hata member mmoja kwenye huu Uzi hapa....
Kuwa watu wanachoangalia ni uwezo wa kiongozi kubadilisha maisha yao katika muelekeo chanya ambapo ni kuletewa maendeleo haijalishi kiongozi huyo ni dekteta au mtu wa demokrasia.
Uwe ni mpenda demokrasia umeachia uhuru wa kisiasa kwamba watu wanatukana wanavyotaka, lakini kama hakuna maendeleo au taifa linajikongoja na wizi umetamalaki bila ya watu kuchukuliwa hatua yoyote, basi utaishia kudharaulika na demokrasia yako hiyo.
Pia vile vile unaweza kuwa ni mdikteta ila watu wanaona kazi unayoifanya na taifa linasonga mbele, hakuna atakayekumbuka hata kama Yuko chini ya utawala wa kidikteta.
Asilimia kubwa ya Hawa wajuaji waliopo humu wanaopiga kelele kuhusu demokrasia si kweli kwamba wanahitaji kiongozi mwana demokrasia, Bali wanataka kiongozi dhaifu atakayeruhusu upuuzi mwingi ikiwemo ufisadi kwa mwamvuli wa demokrasia.