Nchi inapigwa, kutwa nzima ni Mada za Yanga na Simba
Serikali ya awamu ya tano ndiyo muasisi wa hoja nyepesi kwenye redio na TV,ukiminya uhuru wa nyombo vya habari hayo ndio matokeo yake.
mkuu labda umeongea hivyi kwa interest zako binafsi,lakini kipindi cha huyu mzee ndio kipindi ambacho watu wengi walihamasika kusikiliza na kuangalia taarifa za habari na watu kufahamu maendeleo ya miradi mbali mbali ya nchi.
 
Mshairi wa Warumi wa kale Juvenal aliandika katika kitabu chake cha kejeli "Satirws" kuwa , ukitaka kuwatawala watu wa kawaida, unatakiwa kuwapatia mkate na michezo.

Yani mikate wale wasipate njaa, halafu wakishiba wape michezo waburudike.

Hawatauliza mambo ya msingi ya nchi inavyokwenda.

Ndicho kinachotokea Tanzania.

Katika kitabu cha maisha ya Nyerrere kuna mfano wa Nyerere kapewa ushauri na washauri wake rasmi wachumi, lakini akauacha ushauri ule akawafuata wazee wa Yanga wakampa ushauri tofauti, akaufuata ule ushauri wa Mzee wa Yanga Tabu Mangala.

Mimi mwenyewe nishawahi kuona mtu wa usalama wa taifa anakuwa rais wa Yanga.

Ina maana serikali imejiingiza kwenye michezo na inatumia michezo kisiasa.

Like Juvenal.said, it's bread and circuses.
Hakika
 
Generation Z yetu ukibahatikana kuingia kwenye vichwa vyao utakutana na hivi vitu;

1.Chama

2.Pacome Aziz Ki

3. Iphone simu kali kupita Tecno

4. Ist sio gari.

5. Chura ndio habari ya mjini.

6. We Zombie haujui

7 . Mapiano

8. .......

Jaribu kumuuliza Bashe ni Waziri wa nini halielewi. Hajui huko bungeni kuna wahafidhina wanapeleta hoja boom lifutwe yenyewe hayana habari. Siku yakikosa boom yanaanza kuwalilia wanaharakati wawasemee. Yapo yapo tu.

"Aina hii ya vijana wana mchango mdogo katika Taifa"

Late Magufuli.
Na haya ndio mambo watawala wanapenda
 
Kuileta hapa na wanajf kuchangia inatosha? Hii nchi bado ina safari ndefu sana.
Yeye ameileta hapa sisi tunatakiwa kuchukua hatua zaidi, watu wakatoa mawazo na kuyafanyia kazi tuondokane na huu upumbavu
 
Mtaji wa wanasiasa wa DANGANYIKA ni ujinga wetu sisi WADANGANYIKA
 
Mimi ni mpenzi wa mpira lakini naunga mkono hoja, watanzania tumetekwa na mambo ya kijinga ya Simba na yanga, kama vile hatuna vitu vya msingi vya kujadili, mbaya zaidi Hadi akina mama, Utaskia mara chama, mara sijui kibu.....Simba na yanga ni tatizo kwenye vichwa vyetu
 
Yeye ameileta hapa sisi tunatakiwa kuchukua hatua zaidi, watu wakatoa mawazo na kuyafanyia kazi tuondokane na huu upumbavu

Huko ni kutaka wengine waumie kwaajili yetu. Hii ndo changamoto namba1 ya hii nchi kila mtu ni keyboeard warrior akimlaumu mwingine kwanini hajafanya yani wengine waumie huku yeye katulia tu sababu alitweet au kuandika JF. Nobody got time for that. Kama anaona wengine wajinga kwa kutokufanya kitu aanze yeye, real action sio kuandika tu. Hiyo kila mtu anaweza. Wakenya wangeamua kuishia twitter leo wasingekua wanapiga msosi bungeni
 
Mimi ni mpenzi wa mpira lakini naunga mkono hoja, watanzania tumetekwa na mambo ya kijinga ya Simba na yanga, kama vile hatuna vitu vya msingi vya kujadili, mbaya zaidi Hadi akina mama, Utaskia mara chama, mara sijui kibu.....Simba na yanga ni tatizo kwenye vichwa vyetu
Ni hatari sana mkuu, vijana kutwa nzima ni Maada za wakina Chama mala Azizi k
 
Na hao viongozi wenu wanajua mnavyopenda,utaskia tu amechangia sijui nini yanga.

Wanajua kiwapumbaza.
 
Au ni hii Kahawa chungu tunayokunywa ndio inatufanya tuwe Mazoba bin Mazezeta tumebakia kulogana usiku na mchana.
 
Na hao viongozi wenu wanajua mnavyopenda,utaskia tu amechangia sijui nini yanga.

Wanajua kiwapumbaza.
,[emoji23] waziri mkubwa kama.wa fedha anasimama kusema yanga iwekwe kwenye noti za fedha zetu
 
Back
Top Bottom