Nchi inapigwa, kutwa nzima ni Mada za Yanga na Simba
Kuna muda mambo yanayoendelea bongo yanakera hadi unatamani utembeze bakora kwa wabongo labda akili zitawakaa sawa.sasa hivi stori za vijana wa bongo ni chama sijui pacome sijui kibu d na upuuzi mwingine.kinachoendelea bungeni hakiwahusu,mikodi ya hovyo hovyo na mambo mengine ya kipuuzi yanayopitishwa hawanan muda nayo......yaani inakera sana.
 
Hii ni zaidi ya ujinga mkuu, ni ujinga wa kutisha
Ni kama umeniwahi kuliongelea hili, nami nilikuwa na mpango wa kuliongelea. Katika pita pita zangu, 96% ya sehemu ninazopita basi ukiona mikusanyiko ujue mada inayoongelewa ni mpira, hasa hasa ushabiki wa Yanga na Simba.
 
Mshairi wa Warumi wa kale Juvenal aliandika katika kitabu chake cha kejeli "Satires" kuwa , ukitaka kuwatawala watu wa kawaida, unatakiwa kuwapatia mkate na michezo.

Yani mikate wale wasipate njaa, halafu wakishiba wape michezo waburudike.

Hawatauliza mambo ya msingi ya nchi inavyokwenda.

Ndicho kinachotokea Tanzania.

Katika kitabu cha maisha ya Nyerere kuna mfano wa Nyerere kapewa ushauri na washauri wake rasmi wachumi, lakini akauacha ushauri ule akawafuata wazee wa Yanga wakampa ushauri tofauti, akaufuata ule ushauri wa Mzee wa Yanga Tabu Mangala.

Mimi mwenyewe nishawahi kuona mtu wa usalama wa taifa anakuwa rais wa Yanga.

Ina maana serikali imejiingiza kwenye michezo na inatumia michezo kisiasa.

Like Juvenal.said, it's bread and circuses.
Fact!
 
Kweli kabisa kabisa 🙄
 
Mna majibu mepesi sana kwa maswali magumu. Kila mtu akiishia kuandika mtandaoni tu itasolve nini? Mnajibu matusi kwa swali dogo tu then mnashangaa wengine kufuatilia michezo? Nyie nyani hamuoni kundule.
Ulitaka vipi mkuu?
 
Serikali ya awamu ya tano ndiyo muasisi wa hoja nyepesi kwenye redio na TV,ukiminya uhuru wa nyombo vya habari hayo ndio matokeo yake.
Profile picture yako tu inatupa sababu kwanini umeamua kutoa hii comment isioendana hata kidogo na mada husika.

Yaani marehemu baba yako alikuwa mwizi na katika harakati zake za wizi alifanikiwa kukusanya mali nyingi sana ambazo mpaka sasa nyinyi watoto wake bado mnazifaidi, halafu leo hii mimi mmoja wa watu waliobiwa na marehemu baba yenu nimeviona vitu alivyoniibia na nimekuja kuvidai halafu wewe kwa kujiamini kabisa eti unaniambia hivyo vitu aliyeviiba ni marehemu baba yangu na mimi sina kosa lolote hivyo basi acha niendelee kuvitumia na wala hautakiwi kufanya jambo lolote maana muhusika mkuu hayupo....

Mantiki ni kwa vile Magufuli alivuruga kabisa utaratibu mzima wa utoaji wa habari, basi awamu hii ya samia ni haki iendelee kuishi kwenye huu uozo uliopo pasipo kufanya juhudi zozote za kuurekebisha just kwa sababu unatoa advantage kwa watawala sio???
 
mkuu labda umeongea hivyi kwa interest zako binafsi,lakini kipindi cha huyu mzee ndio kipindi ambacho watu wengi walihamasika kusikiliza na kuangalia taarifa za habari na watu kufahamu maendeleo ya miradi mbali mbali ya nchi.
Mtu mwenyewe kweny avatar yake kuna picha ya Kikwete, kuna haja hata ya kujiuliza kwanini ameamua kuskip awamu hii ya Samia na kutoa lawama kwenye awamu ya tano kwa upuuzi ambao unarekebishika hata ndani ya awamu hii ya samia?

Hawa walamba asali, wala rushwa,wazembe makazini,wachonga vyeti feki,wapenda shortcuts na machawa ni watu wa ovyo ambao akili zao ziko makalioni.
 
Mshairi wa Warumi wa kale Juvenal aliandika katika kitabu chake cha kejeli "Satires" kuwa , ukitaka kuwatawala watu wa kawaida, unatakiwa kuwapatia mkate na michezo.

Yani mikate wale wasipate njaa, halafu wakishiba wape michezo waburudike.

Hawatauliza mambo ya msingi ya nchi inavyokwenda.

Ndicho kinachotokea Tanzania.

Katika kitabu cha maisha ya Nyerere kuna mfano wa Nyerere kapewa ushauri na washauri wake rasmi wachumi, lakini akauacha ushauri ule akawafuata wazee wa Yanga wakampa ushauri tofauti, akaufuata ule ushauri wa Mzee wa Yanga Tabu Mangala.

Mimi mwenyewe nishawahi kuona mtu wa usalama wa taifa anakuwa rais wa Yanga.

Ina maana serikali imejiingiza kwenye michezo na inatumia michezo kisiasa.

Like Juvenal.said, it's bread and circuses.
Maelezo mazuri sana mkuu.

Hata michezo ya kubashiri, kamari au betting ilikuwepo tokea karne hizo za Roman circus.
Sasa hivi Kuna pombe zinaitwa visungura na nyinginezo zinaharibu sana vijana.
Ukimkosa kijana kwenye ulevi wa pombe, shisha, bangi n.k utampata kwenye betting au Simba na yanga bila kusahau movie za kituruki na kikorea (promo kubwa ya Madam President).
Inasikitisha sana.
 
Tanzania ni nchi ya Kipuuzi sana fikiria kutwa nzima,vituo vya Radio na Television maada ni Mpira yaani hata Brazili sio hivyo, Brazili wanao penda mpira bado hatujawafikia.

Hakuna Maada nyingine utaisikia kwenye hivi vituo zaidi ya Yanga na Simba kutwa nzima, wanaanza kujadili mpira kuanzia asubuhi hadi usiku.

Vijiwe vya kahawa the same, mtu unakuta kachoka mbaya ila kelele hizo za Yanga na Simba utamtaka.

Sasa wale walioko kwenye muungano wa OPEC ya kufilisi nchi wao wanajitoea mali za nchi. nchi inapigwa wajinga kutwa nzima n Maaada za Yanga na Simba.
Mwambie mzee Mbowe aanzishe Radio ya cdm itakayokuwa inaongelea unachokitaka
 
Tanzania ni nchi ya Kipuuzi sana fikiria kutwa nzima,vituo vya Radio na Television maada ni Mpira yaani hata Brazili sio hivyo, Brazili wanao penda mpira bado hatujawafikia.

Hakuna Maada nyingine utaisikia kwenye hivi vituo zaidi ya Yanga na Simba kutwa nzima, wanaanza kujadili mpira kuanzia asubuhi hadi usiku.

Vijiwe vya kahawa the same, mtu unakuta kachoka mbaya ila kelele hizo za Yanga na Simba utamtaka.

Sasa wale walioko kwenye muungano wa OPEC ya kufilisi nchi wao wanajitoea mali za nchi. nchi inapigwa wajinga kutwa nzima n Maaada za Yanga na Simba.
Usichojua ni kuwa utawala ni kwa ajili ya kugawana rasilimali za Taifa. Pale kenya wale waandamanaji hawataambulia kitu lkn tabaka la wenye nacho wataambulia kitu. Tayari nakada wa upinzani wamepata uwaziri, unadhani wakiokuwa front wataambulia kitu?

Bora tuendelee na maisha yetu maadamu tunakula na kulala
 
Wewe umechukua hatua gani kiongozi au unasubiri wengine waumie kwaajili yako?
Halafu wakisha umia, wataambulia nini? Wakenya wachache wanagawana nchi, waandamanaji wanapiga miayo tu. Si bora sisi?
 
Wengi wameshajikatia tamaa au kuridhika na maisha yao mkuu, hicho ndicho kilichobakia cha maana zaidi kwao.
Hata viongozi wa siasa nao wanatembea humo.
Mfano Libya, walivuna nini?
 
Maisha yakiwa magumu, watu huamua kuambatana na yake mambo yanayowapa furaha kwa unafuu....🤔🤔
 
Back
Top Bottom