Mshairi wa Warumi wa kale Juvenal aliandika katika kitabu chake cha kejeli "Satires" kuwa , ukitaka kuwatawala watu wa kawaida, unatakiwa kuwapatia mkate na michezo.
Yani mikate wale wasipate njaa, halafu wakishiba wape michezo waburudike.
Hawatauliza mambo ya msingi ya nchi inavyokwenda.
Ndicho kinachotokea Tanzania.
Katika kitabu cha maisha ya Nyerere kuna mfano wa Nyerere kapewa ushauri na washauri wake rasmi wachumi, lakini akauacha ushauri ule akawafuata wazee wa Yanga wakampa ushauri tofauti, akaufuata ule ushauri wa Mzee wa Yanga Tabu Mangala.
Mimi mwenyewe nishawahi kuona mtu wa usalama wa taifa anakuwa rais wa Yanga.
Ina maana serikali imejiingiza kwenye michezo na inatumia michezo kisiasa.
Like Juvenal.said, it's bread and circuses.