Nchi masikini haiwezi kuendelea ikiongozwa kidemokrasia

Wewe unaongea kama peasants wote walivyoongea katika historia. Kwa sababu aliishi wakati wa ujamaa, basi kwake ndiyo mfumo bora kabisa, aliyeishi enzi za utumwa naye aliona hakuna mfumo bora kama huo. Aliyeishi kwenye ukabaila naye anaona huo ndiyo mfumo, aliyeishi kwenye ubepari naye huo ndiyo mfumo bora kabisa, na wewe kwa sababu unaishi zama za demokrasia, na wewe kwako ndiyo mfumo bora kabisa. Usiwe fuata upepo.

Mfumo usioweza kuzitoa nchi kwenye umaskini unasemaje ni best? Ni mfumo wa hovyo, ni kitu cha anasa kwa nchi tajiri kisichokuwa na manufaa yoyote, hata kwao.Kitawafelisha maana demokrasia inaenda sambamba na welfare ya kiwango cha juu. Na welfare inaenda sambamba na kodi kubwa na mikopo.

Demokrasia haina tofauti na ujamaa, ni mzuri kwenye makaratasi, lakini kiuhalisia una matatizo makubwa.
 
Africa ndilo bara lenye madikteta wengi na nchi chache za kidemokrasia ila ndilo bara maskini kupita yote pia.
Shida siyo kukosa demokrasia au udikteta. Shida ni sera mbovu za kiuchumi, na hasa kuingia kwenye soko huria kichwakichwa.
 
Nyumba nayo inafanya uchaguzi? Tangu lini? 😜
Nyumba ina taasisi mbali mbali zinazotumika katika kuminya uhuru na haki ya wanaoishi katika nyumba hiyo? Acha kuleta mifano buti isiyohusu kitu.

Wewe umewahi ona nyumba inaendeshwa kidemokrasia?

Na uelewe kuwa kukosa demokrasia haimaanishi kupiga, kuua na mambo mengine uliyotaja hapo juu.
 
Udikteta ni shida kubwa na ndiyo chanzo cha sera MUFILISI kama kujenga chato Airport, kununua ndege etc. Kama siyo udikteta hayo yote Bungeni yangepigwa chini katika Bunge huru.

Shida siyo kukosa demokrasia au udikteta. Shida ni sera mbovu za kiuchumi, na hasa kuingia kwenye soko huria kichwakichwa.
 
Tujibu kwa mifano Pia, je General Park wa Korea? Vipi Kuhusu Lee Kuan Yew na Singapore? Vipi kuhusu CCP na China?

Ingekuwa Demokrasia ndio msingi wa Maendeleo duniani, basi Marekani wasingemuweka madarakani dikteta Pinochet na kumtoa mwanademokrasia Allende.
 
Udikteta ni shida kubwa na ndiyo chanzo cha sera MUFILISI kama kujenga chato Airport, kununua ndege etc. Kama siyo udikteta hayo yote Bungeni yangepigwa chini katika Bunge huru.
Yalikuwa ni mambo ya hovyo. Na pengine yaliletwa na demokrasia, ni kawaida kwa viongozi wa kidemokrasia kupeleka maendeleo kwa wale waliowapigia kura kwa wingi japo na madikteta hufanya hivyo.

Ila nielewe kuwa siungi mkono udikteta, na sijadai kuwa nina alternative ya demokrasia. Nimeweka tu mapungufu yake, na kama mfumo hauwezi kututoa kwenye umaskini, hayo ni mapungufu makubwa sana, ni kama haufai.
 
Makuwadi wa soko huria daima wanahubiri kuwa Demokrasia hii ya Kiliberali ndio msingi wa Maendeleo ya kiuchumi. Lakini historia inaonyesha Demokrasia haileti maendeleo ya kiuchumi bali ni zao la Maendeleo ya kiuchumi na huimarisha zaidi Maendeleo.

Na logic yake ni nyepesi tu, ili taifa lolote liendelee kiuchumi, ni lazima lilinde uzalishaji wa ndani, ni lazima liweke kodi kali kwa washindani, ni lazima lidhibiti mipaka yake na uingizwaji wa bidhaa shindani na lazima lihimize ufanya kazi kwa kujitoa. Sasa haya yote huchukua miaka takribani 30 kuyatenda na kufikia Maendeleo hayo. Katika mchakato huo kuna maadui wa nje na ndani, ambao hutumia watu na mbinu mbalimbali kuvuruga, pia yanasababisha uhaba wa bidhaa fulani fulani ambazo kwa mwanzo kuyumbisha ustawi wa jamii. So, haya huweza kutumiwa kuleta chokochoko na kuvuruga michakato hiyo. Ndio hufanya watawala wa wakati husika kuwa wakali na wababe (madikteta). Na hawa huwa ni madikteta wanaojenga jamii (Benevolent dictators). Ndio njia walizopitia Singapore, Korea kusini, China, Vietnam n.k. Baada ya kuendelea kiuchumi, jamii yenyewe automatically inakuwa na mapambano na uhitaji wa Demokrasia hii ya Kiliberali.

Kichotokea Afrika huku, Hii Demokrasia tunayolazimishwa kuitumia, haina lengo la kuleta Maendeleo, bali ni nyenzo ya wezi wa dunia kuiba huku.
 
Nchi maskini nyingi zina wananchi wajinga wengi kuliko wananchi wenye faida za kujenga taifa.
 
Nchi maskini nyingi zina wananchi wajinga wengi kuliko wananchi wenye faida za kujenga taifa.
Maana yake itabidi kiongozi atekeleze zaidi sera za kuwapendelea wajinga(serq A kijinga😀)maana kama ni wengi maana yake hata kwenye sanduku la kura ni wengi, usipowatimizia matakwa yao utatoka. Na hakuna anayetaka kutoka.
 
Mambo ya hovyo yaliyoletwa na demokrasia lakini huna mifano ya hayo mambo ya hovyo yaliyosababishwa na demokrasia!? 😳😳

 
Makuwadi wa soko huria daima wanahubiri kuwa Demokrasia hii ya Kiliberali ndio msingi wa Maendeleo ya kiuchumi. Lakini historia inaonyesha Demokrasia haileti maendeleo ya kiuchumi bali ni zao la Maendeleo ya kiuchumi na huimarisha zaidi Maendeleo.
Mkuu natumaini kuna watu watakuelewa. Niongezee mfano mmoja wa karibuni. Nchi za Africa mashariki mwaka 2015 zilikubaliana kuwa mwaka 2019 zipige marufuku uagizaji wa nguo na viatu vya mitumba. Lengo ni kukuza uwezo wa ndani wa kuzalisha vitu hivyo. Rais Trump akasema kuwa nchi itakayopiga ban mitumba anaitoa kwenye AGOA. Viongozi wote wakafyata, ni Kagame peke yake(anayesifika kwa kutokuwa mwanademokrasia) ndiyo akabaki na msimamo. Ni wazi kuwa wengine hawa walijua kutolewa AGOA kungeleta makelele mengi kutoka kwa 'wanademokrasia' kwenye nchi zao. Mwisho wa siku mpango mzuri wa maendeleo umekufa kibudu.

Demokrasia na soko huria ni nyenzo za ukoloni mamboleo.
 
Hilo neno Pathetic. Law brain capacity!!
umenitukana mimi ama ni signature yako!!
 
Taja nchi iliyoendelea huku ikiwa na demokrasia wkt inaendelea.
 
Dah....wachache sana watakuelewa....hasa wale wasiotumia kilevi Cha magharibi 🤣🤣🤣🤣🤭
 
Uchumi haupo hivyo eti mnafanya harakati za maendeleo alafu pesa zionekane mtaani, watu walitoa machozi jasho na damu kufika walipo, huwezi kujenga nyumba nzuri wakati una kipato cha kawaida zen at the same time ukawa una spend. Uchumi gn mmesoma waafrika?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…