Nchi za Afrika zagawanyika katika upigaji kura kuhusiana na Vita vya Russia na Ukraine, Tanzania yachagua kutofungamana na upande wowote

Nchi za Afrika zagawanyika katika upigaji kura kuhusiana na Vita vya Russia na Ukraine, Tanzania yachagua kutofungamana na upande wowote

Jaman tume abstain



🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
Iviii kumbe ile NAM ya shuleniiii bd ipogo nkajua ikogo shuleni tyu
Kura ile haikuwa ina maana ya alignment na nchi yoyote, ilikuwa ni kura ya kulaani kitendo cha taifa moja kutoheshimu mipaka inayotambuliwa na umoja wa mataifa na kufanya kuvamizi wa kijeshi dhidi taifa jingine. Dunia ya leo ambapo vita baridi imekwisha hakuna tena swala na non-alignement, ndiyo maana makampuni ya marekani yamekuwa yanafanya biashara urusi. Ni Putin ndiye bado anaota vita baridi na anataka kuturudisha huko.

Uchimbaji wa mafuta Urusi unaompa kiburi umefanywa na makampuni ya nchi za Magharibi baada ya cold war kuisha: BP, ExxonMobil, Chevron, Shell, Halliburton, TotalEnergy BASF na mengineyo. Uchimbaji ulianza miaka hii ya 2000 tu, makampuni hayo yakisimamisha production ya Mafuta, Urusi itaangukia pua tena kiuchumi. Hawana industrial products zozote wanazouza kwenye soko la kimataifa zaidi ya silaha tu, ambazo soko lake limepungua sana siku za hivi karibuni.
 
Nakumbuka kuvamiwa kwa Libya tulipinga,lakin hata hatukutuma hata wanajeshi waliokalibia kustaafu
 
issues si uoga wala sitetei. Ila kuna nchi zimekaa kimya na zina uwezo kuliko tz.
Si ujinga but ni busara
Wenye busara hutoa neno ili liponye!
Kuna msemo unasema wenye hekima wakinyamaza wapumbavu huongezeka. Sasa sisi tumenyamaza hatueleweki
 
Tanzania imepiga kura na kusema yenyewe yenyewe uko upande wowote ambako upepo utakakokwenda na yenyewe ipo; abstention, yaani haina msimamo!
to abstain maana yake imebaki neutral, haipo upande wowote, yaani haikupiga kura.
 
Tanzania imepiga kura na kusema yenyewe yenyewe uko upande wowote ambako upepo utakakokwenda na yenyewe ipo; abstention, yaani haina msimamo!
Kwa maneno mengine Tanzania haifungmani na upande wowote, na huu ndiyo msimamo wa Tanzania tangu tupate uhuru, kwa hiyo kwa masuala yanayohusiana na vita kati ya east na west, huwa haiungi mkono upande wowote.
 
Kama hii ndiyo diplomasia yetu kweli, basi Tanzania imetia aibu sana. Proud sana kwa wa majirani Kenya ambapo balozi wao alitoa fundisho linalohusu kuheshimu mipaka.
Hapana. Kenya hatoi fundisho lolote hapa, bali anazo sababu maalum za kufanya hivyo, sababu ambazo sidhani kuwa zinampa heshima ya kuwa "mtoa fundisho".
Kenya anamgogoro wa mpaka na Somalia, ambao anatishia vita pamoja na kwamba mahakama ya kimataifa ilitoa uamzi juu ya swala hilo.

Na kenya huyo huyo alishapeleka majeshi yake Somalia enzi za Kibaki; na hadi leo wapo huko huko.
 
Zanzibar sijaiona [emoji41][emoji41][emoji41]








Ova
Zanzibar hawezi kujihusisha na mambo madogo madogo kama haya ambayo anamtuma kijana wake (Tanzania) ayashughulikie, huku yeye akila kuku kwa mrija!
 
Sio kwamba Tanzania haina msimamo, huo ndio msimamo wake...!
 
Kenya wao wanasema eti ni America na wanaishi kiamerika amerika kuanzia lugha na tamaduni zingine
 
Ni kweli Tanzania katika msimamo wake kuhusu sera za nchi za magharibi na mashariki huwa haifungamani na upande wowote tangu tupate uhuru mwaka 1961. Hiyo ndiyo taarifa kwa vijana wa kizazi hiki ambao wengi hawajui hilo.
Sio kwamba Tanzania haina msimamo, huo ndio msimamo wake...!
 
Back
Top Bottom